Kisa cha Rafiki yangu Kutajirika na Kufariki kinahuzunisha

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Jamaa tulimaliza naye shule mwaka 1996 form four. Mimi nikaendelea na masomo na kufanikiwa kumaliza chuo.

Nlikuja kutana nate tena mwaka 2003 akiwa anahangaika na maisha kwa kufanya biashara ndogo ndogo. Aliendelea nazo mpaka mwaka 2019 ambapo maisha yake yalibadilika sana. Akaja kuwa na pesa nyingi na maisha mazuri. Akiwa na maduka ya spares na hardwares kariakoo.

Maisha yalimnyookea hasa. Akawa anawalamba wadada wa mjini wanaopenda pesa kama masikhara. Hawa waigizaji na wasanii mbalimbali. Kiufupi madada wa mjini kawalamba sana. Na alikuwa anasema yeye hapendi kutumia kinga.

Mwaka huu amefariki. Nimeumua sana na ndipo nilipofahamu kisa na mkasa wa Utajiri na kifo chake. Toka kwa mkewe mwenyewe.

Anasema jamaa alienda kwa mganga kusaka utajiri Mkoa flani. Huko aliambiwa kuna njia kadhaa za kupata utajiri.

Moja aliambiwa amtoe mama yake kafara. Jamaa aligoma sababu anasema alimpenda mama yake na alitoka naye mbali sana. So ikawa haifai.

Ya pili ikawa amtoe kafara mkewe hii nayo ikawa changamoto kwake walikuwa na watoto wanne wenye mapenzi sana na mama yao na yeye mwenyewe akakataa.

Ya tatu akaambiwa ni ya kumtumia kuku jogoo. Huyu kuku jogoo alilekezwa akamnunue sokoni. Akiwa na sifa kadhaa. Kisha aende naye kwa mganga. Kweli alifanikiwa kumpata kuku husika na kumpeleka kwa mganga.

Mganga akamsomea dua yule kuku na kumwambia jamaa akakae naye kwa siku tatu kisha arudi naye kwa mganga. Aje amlishe punje. Na kuwa idadi ya zile punje ndiyo itakuwa idadi ya miaka ambayo jamaa ataishi.

Jamaa alivyopewa yule Jogoo akaenda naye kwake na kumfungia kwenye banda bila kumlisha kwa siku tatu. Lengo lilikuwa ni kumfanya jogoo awe na njaa sana ili akienda kwa Mganga akale punje nyingi.

Baada ya siku tatu akamchukua jogoo aliyekuwa amedhoofu sana na kumpeleka kwa mganga. Akamfikisha kwa mganja ambaye alichukua punje nyingi za nafaka kuweka mbele yake. Jogoo alijitahidi kuamka akipepesuka na kwenda kudonoa, punje ya kwanza, ya pili, ya tatu. Akakaa.

Wakasubiri waone akienda tena kula. Jogo hakuweza akawa ndo amemaliza.jamaa hakuamini macho yake. Akajaribu sana kumbembeleza jogoo ale tena. Jogoo hakuweza hata inuka. Ikawa ndo zoezi limeishia hapo.

Kweli jamaa alitajirika sana. Akawa na maduka mengi n.k. but juzi juzi hapa wanasema alilalamika tu kichwa kinamuuma. Then akaenda kulala. Hakuamka tena. But miezi kadhaa aliamua msimulia mkewe mkasa huo na mke ndiye ambaye amekuja share kwangu. Bahati mbaya na mke naye ameambukizwa Ukimwi na jamaa ambaye alishajikatia tamaa akawa anagonga pekululu.

Nimesikitika sana kwa hili jambo.
 
kina maswali yamsingi ya kukuuliza.

Ulokutana nae 2019 akiwa yupo vizuri I min anahela so jamaa Kama ni kwenda kwa mganga tuseme alienda 2020

Kilimkuta nini Hadi akaenda kwa mganga wakati alikuwa freshi kiuchumi au tamaa hakutosheka? kwako kashasha.
 
Amepata hitaji la moyo wake nanshindwa kujua wewe unaumia na kifo chake au aina ya kifo alichokufa. .
 
Kwani haifai kula bata miaka miwili alafu niwe nakesha madhabuhuni nikiomba na kusali kuvunja hizo nguvu ili maisha yaendelee hata kama ntafilisika nikama kukonda kwa simba hawezi lingana na paka kuna masalia yatabaki kwa nguvu za maombi
 
Bata Gegedu hairuhusiwi kumpeleka maana nina uhakika atameza punje zote
 
Back
Top Bottom