Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Ni kweli kujibu nilkichokuuliza kwamba kwenye kitu ulichoandika mwenyewe kunahitaji uelewa wa imminent critique?
Sio suala la kuonyesha unajua nini na uelewa wako ni wa kiwango gani, kama havisaidii au havina mchango vinapohitajika hakuna tija yeyote.
Sasa kama huelewei immanent critique mjadala unaweza kukuchanganya.

Naweza kuanza ku argue kwamba Mungu hayupo, kwa kusema "Ikiwa Mungu yupo...", ukasema nishaanza kwa kukubali Mungu yupo.

Sioni tija ya kujibizana na wewe. Unahitaji kukuza uelewa wako kwanza.
 
Nikikujibu, kunielewa kwako kudogo hata jibu langu linakuwa halina maana.

Ni kama nianze kumfundisha sisimizi calculus kwa lengo la kumuelewesha Poincare's conjecture ili tuitumie katika ku solve equations za Calabi Yau manifold katika the eleventh spatial dimension and third temporal axis of string theory!
Punguza mbwembwe jamaa duh[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mungu wako angekuwepo, usingekuwa na haja ya kuniomba chochote.

Unaniomba kwa sababu hayupo, unaelewa hilo?
Nimeeleza kuwa mimi sio mungu hivyo sina sifa ya ujuzi wote na uwezo wote,na kwa maana hiyo kuomba kwangu kunaonesha kwamba sina hizo sifa lau ningekuwa nazo nisingeomba.
 
Sasa kama huelewei immanent critique mjadala unaweza kukuchanganya.

Naweza kuanza ku argue kwamba Mungu hayupo, kwa kusema "Ikiwa Mungu yupo...", ukasema nishaanza kwa kukubali Mungu yupo.

Sioni tija ya kujibizana na wewe. Unahitaji kukuza uelewa wako kwanza.

Nani amekwambia ili ujadili jambo lazima uelewe immanent critique.

Wewe kwa uelewa wako mkubwa na kuijua immanent critique unaona hiyo sentensi iko sawa?

Kwenye sentensibyako ya mwanzo uliweka neno ikiwa?

Nilikutolea mfano wa Kiranga, haukuweza kujibu zaidi ya kulingiza na kulazimisha kuna mambo hayajaandikwa, ukaja na contradiction, na sasa umeleta immanent critique...

Mbaya zaidi, nilitaja kiwango cha uelewa tokea mwanzo, ukapinga sasa nashangaa tunarudi hukohuko.

Naomba nisiendelee kujibizana na wewe.
 
Hivi kumbe maneno yanaweza kuthibitisha?

Nimekuuliza mara kwa mara kwamba Mungu amedanganya? Unajibu amedanganya na kuleta maandiko.

Kwa kuwa unadai Mungu AMEDANGANYA, alikudanganya namna gani?

Ulichokileta hapa ni vitabu kisha unasema Mungu amedanganya.

Unaweza kuthibitisha alivyokudanganya? (Japo wakati huohuo unadai hayupo).
Navyosema mungu yupo ili niendane na akili zako japokuwa huyo mungu ni hadithi biblia na hiyo quran totaly shizophrenia
 
Nimekwambia mkuu kuwa nimezaliwa kwenye jamii ambayo inamjua mungu,kwa maana hiyo tangu udogo wangu nimelelewa katika misingi hiyo hadi kukuwa kwangu.
Mkuu hilo tatizo umekuwa muislam au mkristo kwa ajili ya wazazi wako wamekuwa hivyo iyo inamaanisha kuwa ni sawa upo ktk utamaduni fulani ni ngumu kuacha
 
Huo ndio utetezi wako wa Mungu kudanganya?

Nimekuuliza Mungu amedanganyaje?
Huna hoja hueleweki unazunguka kama circula motion najua unafanya hivyo kwakuwa huwezi ondoa uwongo wa mungu ambaye hata hajui kama mchana na usiku unatokana na dunia kujizungusha
 
Navyosema mungu yupo ili niendane na akili zako japokuwa huyo mungu ni hadithi biblia na hiyo quran totaly shizophrenia

Hauna na wala hautakuja kuwa na uwezo wa kuendana na akili zangu.
Unaelewa upeo au uwezo wa akili yangu?

Turudi kwenye ulichokiandika wewe mwenyewe, kwamba Mungu "amedanganya" nakuuliza amedanganyaje, unataja vitabu.

Unaweza kutetea hoja yako kwamba Mungu "amedanganya?"

Kuna mahali umesema "maneno yangu yana thibitisha..." nimekuuliza, maneno yanaweza kuthibitisha jambo?
 
Tangu nikiwa mdogo nyumbani miaka kama mitatu na kuendelea..ila ni habari za Mungu mkuu na sio mungu
Hilo ndio tatizo mkuu mtoto wa miaka mitatu ana uwelewa gani mpaka abebeshwe habari kama hizo nimegundua nyinyi mmekuwa waislam au wakristo kwa ajili ya wazazi wenu ina maana ww ukristo au uislam ni kama utamaduni kwako ngumu kuacha ht kama kuna uwongo kiasi gani
 
Tangu mwanzo, nimeandika Mungu kwa sifa, sijaandika kwa dini.

Nimeandika "Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote".

Kama umekubali huyu hayupo, na unaamini yupo mwingine, mlete tumjadili.

Kuna watu wanaamini Beyonce ni Mungu wao, kwa vigezo vyao. Inawezekana na wewe ni mmoja wao.
Mimi ninaamini kuwa Mungu yupo, kwa uthibitisho kuwa, ulimwengu wote huu tuuonao leo chanzo ni yeye!!

Kwamba kwa sababu ulimwengu upo, basi kunaaliyeuanzisha/kilichouanzisha. Basi kwangu mimi huyo/hicho ndiyo Mungu.

Lakini habari zake ambazo ndiyo rasmi, zisizo na uthibitisho usio na shaka, mimi sina.

Na haiwezekani kwangu mimi Mungu eti akawa Beyonce kwa mafano. Kwa kufanya hivyo nitakuwa nimetengeneza contradiction kubwa. Yaani beyonce aliyezaliwa mwaka 1981, ndiyo awe Mungu aliyeuanzisha huu ulimwengu zaidi ya mamia billions iliyopita, haiwezekani!!
 
Pengine Kiranga na wengine kama kina Immanuel, wanaweza kawa na imani kuwa Mungu yupo iwapo labda mtaziondoa zile sifa za upendo wote, uwezo wote, na nguvu zote, maana ndio contradiction nyingi wanaziona kutokea hapo!!
Kuwepo na contradictions wanazoziona wao (mitazano ya kawaida ya binadamu yeyote) hakuondoi ukweli na uhalisia wa uwepo wa Mungu mkuu.. Na by the way wanashikilia ka segiment kadogo mno katika volume kubwa ya uwepo wa Mungu
 
Huna hoja hueleweki unazunguka kama circula motion najua unafanya hivyo kwakuwa huwezi ondoa uwongo wa mungu ambaye hata hajui kama mchana na usiku unatokana na dunia kujizungusha

Wewe unaesema Mungu "amedanganya" wakati huohuo hayupo. Nakuuliza amedanganyaje?

Unaleta maelezo na vitabu. Unaelewa tofauti ya mtu kutenda jambo na kupata maelezo ya huyo mtu?

Ungesema maelezo juu ya Mungu yamedanganya. Kusema yeye kadanganya ina maana tofauti kabisa.

Sasa wewe ulieshindwa kilichokufanya uandike Mungu kafanganya ndio una hoja? Iko wapi hoja yako?
 
Inabidi walale tu.

Maana tukija kwenye kujibu hoja kwa hoja,kwa mantiki, hakuna anayeweza kupinga ukweli.

Na mimi nikionekana mjanja sana,mjuzi sana, mwerevu sana etc, napata sifa za bure.

Mini sifa yangu kubwa ni kusimamia ukweli, hata pale ambapo si mjuzi sana.
Kiranga ukweli ninini... Na unasimamia ukweli gani?
 
Hapana.

Mimi sijasema najua.

Mimi nimesema sijui.

Nimesema sijui chanzo cha ulimwengu ni nini.

Nimesema sijui chanzo cha maisha ya dunia hii ni nini.

Wewe umesema unajua.

Umesema unajua chanzo cha ulimwengu ni Mungu.

Umesemaunajua chanzo cha maisha ya dunia hii ni Mungu.

Mimi nimesema sijui.

Wewe umesema unajua.

Tafadhali usijaribu kunifanya mimi ndiye najifanya najua, wakati nimesema sijui,na nimesema ni muhimu tutafute majibu ili tujue, na wewe umesema unajua.Umesema unajua chanzo cha yote ni Mungu.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] haya mapya sana kwangu.. Hebu angalia usijekuwa umemnukuu mwingine kwa bahati mbaya..... Mimi na wewe mjadala wetu haukufika huko kwakuwa kuna swali la akili ulikwepa kabisa kulijibu....
Hata hivyo nakupongeza sasa umekuwa mnyenyekevu na tutaongea lugha moja
 
hii kali mshana kiranga anaakili ndio maana hajajibu maana ya akili na akijibu maana ya akili bhasi mjadala utaisha na ww ukitaka kujuua huyu jamaa anaakili wtu kadhaa wamejaribu kutoa maana ya akili lakini hajazikubali anataka ya kwako tuu.. na ww ukijibu atakuongezea maswali ambayo yatataka yatataka ufafanuzi....kuna wakati unamuliza swali anakuuliza swali ni nini...mm nimegundua kumuelezea mungu yupo ni ngumu sana ila hoja za hayupo ni nyingi na zinanguvu..mjadala uishe
Umempa kick ya bure ila kwakuwa ndio mtazamo wako sina shida na hilo....
Umesema ana akili sana ndio maana akakataa kujibu kama ana akili ama hana? Are you serious?
Ameniuliza akili ninini nimejibu mara 20 na najibu kwa mara nyingine tena AKILI ni AKILI... Hili ndilo jibu langu bila kujali ni sahihi ama si sahihi
Kama jibu la akili ni AKILI ni sahihi hakuna shida kama jibu la AKILI ni AKILI sio sahihi je jibu sahihi ni lipi? Unaweza pia kumsaidia kujibu
 
Si unaona Sasa! Kumbe unazungusha tu lakini mahali pa kupatikana jibu pako hapahapa. Typical us!

Read everything possible.
A personal interpretation towards one's point of view
 
mpatto

Tena mkuu kama utachunguza vizuri utagundua kuwa hata jinsi atheists humu wanavyoziwakilisha hoja zao kuhusu mungu zimeegea sana kutoka kwenye mafundisho ya biblia.

Labda pengine kwa kuwa mtu kama Kiranga ametokea huko.
Na ndio maana nasema mara zote Kiranga sio atheist original... Ni mkristo aliyekengeuka imani... Na ndio 'ma atheist' tulio nao JF
 
Tz mbongo ,

Mimi nadhani tufanye hivii,

Kwa sababu lengo kuu la uzi huu (hasa sisi third parties(tusio na upande)) ni kujifunza na kushare experiences, basi nitoe rai kwa wachangiaji wakuu (Kiranga , Mshana Jr et al) tujadili uwepo wa mungu bila kuegemea katika maandiko fulani ya dini fulani, kwa sababu, dini ziko nyingi na ninafikiri sio lengo la mwenye uzi ku critesize dini ya mtu!!
Tutaweza kujadili tu endapo swali la una AKILI ana huna AKILI litapata majibu.. Astronomer the great alinijibu na nikampongeza
 
Tutaweza kujadili tu endapo swali la una AKILI ana huna AKILI litapata majibu.. Astronomer the great alinijibu na nikampongeza

Acha filibustering fafanua maana ya akili ni nini,kwani hicho ndicho watu wanasubiri kwa hamu kutoka kwako.
 
Hahaha haya, kumbe huna proof hata moja, basi endelea kuamini, acha kuchamba wenzako ambao wanaamini tofauti na wewe. Ni msimamo tofauti tu, sio wote wanafatafata tu mambo yasiyo na proof. Na unavyomsema jamaa kua anafuata wikipedia huku imeandikwa na binadamu, unasahau kua vitu vilivyoandikwa kwenye wikipedia tunaweza kuviprove, wewe unatumia simu unapost JF dunia nzima tunaona, hiyo ni proof enough kua tunachofanya tunakijua hatuendi kwa imani, tunaenda kwa proof.

Twende mdogo mdogo
1. Umeuliza swali nami nimekujibu
2. Jibu langu pengine halijakufurahisha sana.. Mpaka umetumia neno KUCHAMBA WENZAKO! hapa umepotoka vibaya sijamchamba mtu bali tumeendelea kubishana kwa hoja
3. Umesema kila mtu ana imani yake hii inaweza kukugharimu maelezo ya kina kama nikiamua kukuuliza kama Atheism ni imani ama sio imani..
4. Kitu kinachoitwa imani hakina ithibati za kidunia kwakuwa ni cha kiroho....
5. Umezungumzia kuhusu smart phone... Hapa nimepapenda mno na labda unijibu kama unaweza kujua kwa hakika kwanini tunaweza kuwasiliana mimi na wewe kupitia hizi simu janja....
Je ni hizi vitu tulivyoshika na kubofya ndio vinafanya tuwasiliane?
Vipi kuhusu chaji
Vipi kuhusu network
Vipi kuhusu bundle
Vipi kuhusu software
Vipi kuhusu number ya simu
Vipi kuhusu IP address
Vipi kuhusu User ID
Mpaka tunaweza kuwasiliana hivi ni mchakato mrefu usioonekana... Zaidi ya
Siku tulizoshika mikononi
Maandishi tunayoandika
Minara ya simu nknk
Kwenye kila kitu kuna software na hardware...
Software haina ithibati ama proof ya kuonekana kwa macho so the God, hardware inaweza kuonekana kwa macho, na ukaipima kwa vipimo, ukaipa uzito na ujazo, ukaipa rangi nk
Na hapa ndio tunapopishana uelewano
 
Back
Top Bottom