Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Linazidi kuwa kubwa kwa sababu ya upeo wako mdogo usiojua immanenct critique ni nini.

Na hilo ni tatizo lako wewe, sio langu mimi.
Kwa hiyo kwa vigezo vyako kutokujua immanent critique ni kuwa na upeo mdogo?
 
Kwa hiyo hauwezi kunijibu kwa sababu sijui immanenct critique?
Nikikujibu, kunielewa kwako kudogo hata jibu langu linakuwa halina maana.

Ni kama nianze kumfundisha sisimizi calculus kwa lengo la kumuelewesha Poincare's conjecture ili tuitumie katika ku solve equations za Calabi Yau manifold katika the eleventh spatial dimension and third temporal axis of string theory!
 
Tz mbuwezo: 27272850 said:
Kuna mahusiano gani hapo?
Mungu mwenye uwezo wote,upendo wote na ujuzi wote asingemuumba mtu mwenye uelewa mdogo wa mambo.
Katika hali ya kawaida wewe mzazi una mtoto anayekuwa wa mwisho kila mara shuleni kwenye mitihani na kuzomewa ila wakati huohuo wewe mzazi wake unao uwezo wa kumfanya aweze kuwa miongoni mwa washindi Ila umetulia tu,bado tutakuamini kuwa una upendo wote kwa mwanao!?

Utakuwa natofauti gani na yule mwandishi wa Afrika kusini aliyejiua baada ya kusongwa na kumbukumbu mbaya kwa muda mrefu ya alipokuwa Sudan wakati wa njaa kama ripota alipoacha kutoa msaada kwa mtoto mdogo aliyekuwa na njaa kali hadi kutembea anashindwa.Akatokea ndege tai na kumla mtoto yule umbali kidogo tu na mwandishi huyu alipokuwa,huku akishuhudia kuanzia mwanzo mtoto akijikokota,ndege yule anatokea,anaanza kumdonoa donoa na hatimaye kumzikia tumboni!?

Hapa upendo wa ripota huyu unaachaje kuutilia mashaka wakati hata kama angepiga ndulu tu angeokoa maisha ya dogo!?
 
Nikikujibu, kunielewa kwako kudogo hata jibu langu linakuwa halina maana.

Ni kama nianze kumfundisha sisimizi calculus kwa lengo la kumuelewesha Poincare's conjecture ili tuitumie katika ku solve equations za Calabi Yau manifold katika the eleventh spatial dimension and third temporal axis of string theory!

Hahahaaaaa!!! Si kwa nondo hizi aise,sijutii kusoma sayansi!!

Kuna mercenary mmoja alivamia huu uzi juzi na kijipande chake cha quantum theory toka wikipedia,naona toka aseme anakwenda kulala hajaonekana mpaka leo.Sijui bado kalala!!

Mshana Jr, yuko wapi jamaa yako aliyesema amevurugwa na kipa wa Liverpool!?
 
Hahahaaaaa!!! Si kwa nondo hizi aise,sijutii kusoma sayansi!!

Kuna mercenary mmoja alivamia huu juzi na kijipande chake cha quantum theory toka wikipedia,naona toka aseme anakwenda kulala hajaonekana mpaka leo.Sijui bado kalala!!

Mshana Jr, yuko wapi jamaa yako aliyesema amevurugwa na kipa wa Liverpool!?
Jamaa yangu kwa muktadha UPI? Hebu nifafanulie hapo
 
Nikikujibu, kunielewa kwako kudogo hata jibu langu linakuwa halina maana.

Ni kama nianze kumfundisha sisimizi calculus kwa lengo la kumuelewesha Poincare's conjecture ili tuitumie katika ku solve equations za Calabi Yau manifold katika the eleventh spatial dimension and third temporal axis of string theory!
[emoji3] [emoji3] [emoji3] kisomo cha kukariri misamiati na kuiweka bila mpangilio usioleweka almradi tu uonekane unajua
 
Nikikujibu, kunielewa kwako kudogo hata jibu langu linakuwa halina maana.

Ni kama nianze kumfundisha sisimizi calculus kwa lengo la kumuelewesha Poincare's conjecture ili tuitumie katika ku solve equations za Calabi Yau manifold katika the eleventh spatial dimension and third temporal axis of string theory!
Mr. Kiranga , unaonekana upo vizuri sana kwenye physics, ni kama vile Mr. mshana alivo vizuri kwenye ulozi. Yote hayo, sisi watazamaji tuna jifunza vitu vipya!! [emoji119][emoji119]
 
Asante sana utamfanya ajisikie vizuri sana... Kiranga kuna compliment yako huku japo umeshindwa kabisa kujibu kama una AKILI ama huna AKILI..
Physics sikuipenda kama kuna mtu ni mjuzi hongera zakwe
 
Mkuu hujui ya kwamba elimu inapatikana popote na sio shule?nipe elimu mkuu.
Formal education inapatikana shuleni, labda kama unamaanisha kinyume na hiyo, ndio akupatie!!

Nijuavyo mimi watu wote tuna informal education, by default!

Sasa kama unataka elimu lazima uende shuleni bro, kinyume na hapo tayari elimu unayo (informal education).
 
Asante sana utamfanya ajisikie vizuri sana... Kiranga kuna compliment yako huku japo umeshindwa kabisa kujibu kama una AKILI ama huna AKILI..
Physics sikuipenda kama kuna mtu ni mjuzi hongera zakwe
Pengine Kiranga na wengine kama kina Immanuel, wanaweza kawa na imani kuwa Mungu yupo iwapo labda mtaziondoa zile sifa za upendo wote, uwezo wote, na nguvu zote, maana ndio contradiction nyingi wanaziona kutokea hapo!!
 
Mungu mwenye uwezo wote,upendo wote na ujuzi wote asingemuumba mtu mwenye uelewa mdogo wa mambo.
Katika hali ya kawaida wewe mzazi una mtoto anayekuwa wa mwisho kila mara shuleni kwenye mitihani na kuzomewa ila wakati huohuo wewe mzazi wake unao uwezo wa kumfanya aweze kuwa miongoni mwa washindi Ila umetulia tu,bado tutakuamini kuwa una upendo wote kwa mwanao!?

Utakuwa natofauti gani na yule mwandishi wa Afrika kusini aliyejiua baada ya kusongwa na kumbukumbu mbaya kwa muda mrefu ya alipokuwa Sudan wakati wa njaa kama ripota alipoacha kutoa msaada kwa mtoto mdogo aliyekuwa na njaa kali hadi kutembea anashindwa.Akatokea ndege tai na kumla mtoto yule umbali kidogo tu na mwandishi huyu alipokuwa,huku akishuhudia kuanzia mwanzo mtoto akijikokota,ndege yule anatokea,anaanza kumdonoa donoa na hatimaye kumzikia tumboni!?

Hapa upendo wa ripota huyu unaachaje kuutilia mashaka wakati hata kama angepiga ndulu tu angeokoa maisha ya dogo!?
Kwahiyo unataka kusema mungu hana uwezo wote,uwezo wake una mipaka hawezi kuumba vyovyote vile ajisikiavyo?

Hivyo ndiyo unamaanisha ama?
 
Pengine Kiranga na wengine kama kina Immanuel, wanaweza kawa na imani kuwa Mungu yupo iwapo labda mtaziondoa zile sifa za upendo wote, uwezo wote, na nguvu zote, maana ndio contradiction nyingi wanaziona kutokea hapo!!
Ukisoma vitabu vizuri utakuta simulizi za watu wa nyuma huko wakiadhibiwa na mungu,na mungu akijisifu kwa ukali.
Lakini pua kuna wengine huamini kuna moto huko mwisho wa siku kwa wale waliyotenda maovu.

Sasa mtu anapokuja na suala la sifa ya upole tu kwa mungu na kuanza kutaja iki sijui kisingekuwepo kisa upole wa mungu unashindwa kujua unamsaidiaje,kufa ni jambo la lazima ila mtu anakwambia mungu mwenye upendo hawezi kuruhusu watu wake wafe.
 
Back
Top Bottom