Ndugu
Mshana Jr , kwa upana wa neno 'akili' ni bora ukaweka mipaka ya ufafanuzi wa neno hilo!
Kwa ujumla na kwa maana sisisi, akili ni uwezo wa kufikiri na kukumbuka!!
Na neno hilo lina maana zingine, mfano:
Akili ni nywele, kila mtu ana zake. Kwamba kwa sababu kila mtu sharti awe na nywele(popote pale kwenye mwili wake), hivyo kila mtu ana akili.
Na pia, akili ni mali, na hapa si kila mtu ana mali, hiyo ina maana kwamba si kila mtu ana akili.
Hata kule kijijini kwetu, kuna mtu anaitwa Akili Mali.
Kwa hiyo, neno akili lina maana nyingi, na zote ziko sahihi kulingana na muktadha husika!!
Unapotaka maana ya Akili, kwa ufafanuzi kuwa akili ni akili, hapo mtu ana haki ya kusema chochote kuhusiana na akili, na bado akawa yupo sahihi!!
Kwa mfano, mtu anaweza jibu, Akili ni diwani wa kata ya kalebejo huko bukoba, mila mipaka ya jibu atakuwa yupo sahihi.
Je bwana Jr, unataka maana ya akili kwa muktadha upi!?