Kabla ya kufika mbali kote huko, inabidi mtu a define akili ni nini.
Mtu anaweza kuniuliza "Wewe ni Mkristo?".
Swali hilo likawa gumu kwangu kujibu.
Nimebatizwa kwenye Ukristo na hakuna siku nilikoenda kanisani kusema najitoa Ukristo - kwa hiyo kwa definition ya watu waliobatizwa Ukristoni, waliolelewa familia ya Ukristo ,wenye majina ya Kikristo, mimi ni Mkristo.
Lakini pia, Mkristo ina tafsiri nyingine, kwamba mtu anayemuamini Yesu Kristo na kumfanya kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kwa tafsiri hiyo mimi si Mkristo.
Sasa mtu akiniuliza "Wewe Mkristo?", kabla sijamjibu, inabidi nimuulize, unaposema "Mkristo" una maana gani? Hilo neno lina tafsiri nyingi sana.
Ndicho ninachojaribu kufanya kwa Mshana hapa.
Kaniuliza kama nina "akili".
Neno "akili" lina tafsiri nyingi sana. Sasa, ili kuondoa mkanganyiko, namuomba anipe tafsiri ya neno hilo anayoitumia, anaposema "akili" ana maana gani?
Kusudi nikimjibu nijikite kwenye tafsiri aliyoisema.
Sasa hata mtu aliyeuliza swali hajui anauliza nini.
Mimi nitawezaje kumjibu?