Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

kwa kujua kuwa watu hawapendi kuitwa wapumbavu ndio maana likatumika neno hilo ili watu wasihoji... kwa akili ya kawaida tu ikiwa mtu anahitaji ushahidi juu ya uwepo wa Mungu anakuwajen mpumbavu? nadhani mpumbavu ni yule anayeamini kibubusa kisa tu anaogopa kuitwa mpumbavu ikiwa hataamini.
Jenga hoja kwa mambo ya msingi Chief, Mtu asemaye hakuna Mungu si hoja, ni hitimisho. Kuuliza habari za uwepo wa Mungu hata mfalme Nebkadneza alihoji, Hakuna mahali anaitwa mpumbavu kwa kuhoji kwake.
 
Hakika huwa namuheshimu sana Mshana Jr lakini sijajua ni nIini kimempata hata kufikia hatua ya kujidharirisha namna hii mbele ya halaiki hii ya wana jamiiforums. Nimefuatilia kwa kina mjadala huu ila sijaona kitu cha tofauti kilicholetwa na ndugu Mshana zaidi ya porojo zilezile dhaifu ambazo Kiranga amekuwa akizivuruga vuruga humu.
Sasa hapa Mshana kauliza swali akitaka kujua kama Kiranga ana akili au laa, na Kiranga ameuliza hizo akili ni kitu gani? mjadala ndio umeishia hapo....

Mshana hataki kutoa jibu sababu anajua akitoa tu jibu basi swali lake la mwanzo linakosa mashiko. Mshana bila shaka angejibiwa ndio basi angeuliza unaamini vipi kuwa una akili hali ya kuwa hujawahi kuziona? Na angehitimisha kuwa hata kwa uwepo wa Mungu ni vivyo hivyo kwa maana haonekani ila tunaamini kuwa yupo. Hii hoja dhaifu sana.

Akili sio kitu tangible kama ilivyo figo au ini. Akili ni matokeo ya mchakato fulani unaotendeka ndani ya ubongo ambao kisayansi unaelezeka vizuri tu. Na huu mchakato huweza kuathiriwa na mambo mengi kama mazingira, lishe na mambo mengine. Sasa matokeo ya huu mchakato hubainishwa na tabia za nje za mtu husika hapa inahusu maamuzi, Kauli, muonekano na mambo mengine mengi ambao yakiwa tofauti na matarajio ya wengi tunaweza kuhitimisha kuwa huyu hana akili, yaani mchakato katika ubongo wake umeleta matokeo yasiyotarajiwa yapo chini ya kiwango ila hapa niweke angalizo kwamba huenda huyo anayeonekana hana akili ndiye mwenye akili ila tu akili zake zipo viwango vya juu sana kuliko uwezo wa walio wengi wanaomtazama.

Kulingana na hilo Kiranga ana akili na hili tunalipima kutokana na hoja zake japo sikubaliani nae kwamba hakuna Mungu ila akili zake zimefanya hoja zake ziwe hazijibiki. Mungu yupo ila kuna mapungufu makubwa sana katika hivi vitabu vinavyojaribu kumuelezea. Vinajipinga vyenyewe kabla hata havijapingwa, vinajichanganya. Na hii kusema sijui ili kuvielewa ni lazima kuwa na imani ni sawa na kuwema ili kuvielewa hupaswi kuwa na fikra huru, unapaswa uwe zwazwa kwanza ndipo uvielewe sasa hapo ndipo ninapojiuliza Mungu alitupa uwezo wa kufikiria wa kazi gani kama hataki tuhusishe fikra huru tunapotaka kumuelewa yeye?

Mshana jipange upya maana bado hujafikia uwezo wa kukabiliana na fikra za Kiranga, tukubaliane tu katika hilo mkuu.
Mkuu umefunguka vizuri sana.

Naona ni bora nikaendeleza mjadala na wewe, labda naweza ku gain mawilimatatu.

Maana mjadala na Mshana umekwisha pale aliposhindwa kujibu swali la "akili ni nini?"

Kwa hiyo sioni kamatutaendelea zaidi.

Labda nikuulize.

Umesema vizuri kwamba huyu Mungu wa kwenye vitabu ana mapungufu, mapungufu ambayo nimekuwa nikiyataja mara nyingi hapa.

Kwa hiyo, najisikia furaha kujibizana nawe mtu mwenye mawazo huru na unayeweza kuona mapungufu hayo.

Lakini pia umesema unatofati na mimi bado - kitu ambacho si jambo baya, hatuwezi kukubaliana kila kitu na wote tukabaki wakweli. Umesemaunaamini Mungu yupo, ila si hiuyu wa kwenye vitabu.

1. Kitu gani kinakufanya uridhike Mungu yupo?
2. Inawezekana Mungu akawa hayupo,halafu hicho kitu bado kikakufanya ufikiri kwamba yupo?
3. Kama umemkataa Mungu wa vitabu,kwa sababu anaonekana anajikanganya sana, huyo Mungu unayemkubali anaepukaje kuingia katika mtego wa kuweza kukanganyika? Unaweza kumuelezea kwa namna ambayo haiwezi kukanganyika?
 
Hujanifafanulia swali.

Akili ni nini?
Kiranga una wafuasi wanakusifu sana kuwa wewe ni akili kubwa lakini ni mwepesi mno.. Sijawahi kukuona ukiwahoji kuwa akili ninini[emoji3] [emoji3] [emoji3] what a setback!
 
Kiranga una wafuasi wanakusifu sana kuwa wewe ni akili kubwa lakini ni mwepesi mno.. Sijawahi kukuona ukiwahoji kuwa akili ninini[emoji3] [emoji3] [emoji3] what a setback!
Hujajibu swali.

Akili ni nini?

Mpaka utakapojibu swali, naendeleza mjadalana wengine.

Maana wewe umekwama.
 
Akili ni uwezo wa kupambanua mambo kwa ufasaha kwa maana ya negativities na postivities ya jambo husika.
Kwa sasa nitakuwa naendeleza mahojiano na wengine, hususan wanaojibu swali hili.

Kuonesha kwamba naweza kuendelea na mjadala swali hili likijibiwa.

Kama hizo ndizo akili, basi ninazo, maana nimewezakupinga uwepo wa Mungu kwa ufasaha kwa kutumia"proof by contradiction", proof by contradiction inaanza kwa ku assumekitu kuwa kweli (positives kutokakatikadefinition yako)halafu ina contradict positives hizo na kuonesha assumptions fulani si sahihi na hizopositives si kweli (negatives kwa mfano wako) kwa namna ambayo watu hawajaweza kuipinga hapa.

Sasa kwa nini inakuwa vigumu sana Mshana kunijibukamaulivyonijibu wewe?

Anaogopa nini?
 
Una akili ama huna AKILI?
Unalazimisha swali wakati huwezi kulinyambulisha.

Wenzakowanaonijibu akili ni nini nawaambia kama ninazo au sina.

Kuna wawili nishawajibu swali hili.

Wewe tu nikikuuliza akili ni nini huwezi kujibu.

Hujui unachouliza, nitakujibuje?
 
Kwa sasa nitakuwa naendeleza mahojiano na wengine, hususan wanaojibu swali hili.

Kuonesha kwamba naweza kuendelea na mjadala swali hili likijibiwa.

Kama hizo ndizo akili, basi ninazo, maana nimewezakupinga uwepo wa Mungu kwa ufasaha kwa kutumia"proof by contradiction", proof by contradiction inaanza kwa ku assumekitu kuwa kweli (positives kutokakatikadefinition yako)halafu ina contradict positives hizo na kuonesha assumptions fulani si sahihi na hizopositives si kweli (negatives kwa mfano wako) kwa namna ambayo watu hawajaweza kuipinga hapa.

Sasa kwa nini inakuwa vigumu sana Mshana kunijibukamaulivyonijibu wewe?

Anaogopa nini?
Kiranga nakuuliza tena na tena... Una akili ama huna? Mengine yote ni non n void.. Acha kukwepa swali kwa maelezo yasiyo akisi uhalisia.. Maelezo mepesi mno yaliyojaa utetezi wa kitoto
 
Back
Top Bottom