Akili ni uwezo wa kufikiri, kuhoji na kung'amua mambo.
Nidhamu ya akili ni kuelewa ukweli. Kivipi? Kwa uyakinifu kwa ushahidi, na akili ya namna hii inapewa taswira ya akili yenye afya njema. Na muktadha wa namna huu ndiyo unaobeba dhana nzima ya Ubinadamu. Binadamu mwenye tija, binadamu aliye hai.
Watu wa imani nao wanautumia huu muktadha kwa maana: Kama akili ya mtu imeshindwa kufikiri, kuhoji na kung'amua kanuni na nidhamu ya Ulimwengu jinsi ulivyo kwa kuanza na wewe binafsi.
Kwa akili yenye kuhoji na kufikiri inajipa moja kwa moja yupo aliyevifanya hivi, ambaye ni Muumbaji. Uking'amua hayo akili yako ni akili yenye afya kwa sababu mazingira yenyewe yanajidhihirisha. Kinyume na hapo akili ya mtu inakuwa si yenye afya bali ni yenye uwalakini. Kwa muktadha huo itatafsirika akili yenye dosari, yaani hauna akili. Bi maana Akili haijatimia, haijawa na ukamilfu.
Lakini maana ya neno akili ni pana. Inategemea itatumiwa kwenye muktadha upi.
Ni mawazo yangu tu. Kusahihishwa ruhusa.