Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Kuna msemaji mmoja aliwahi kuivunja hiyo mada kwa maneno machache sana akasema hivi:- UKIPITA PORINI UKAKUTA SAA YA MKONONI IMEDONDOKA PALE, JAMBO LA KWANZA KUKUJIA KICHWANI NI KWAMBA LAZIMA KUNA MTU AMEPITAPO MAENEO HAYO NA KUIDONDOSHA.

Wazo hilo hilo pia hebu lihamishie katika kumtafuta huyu Mungu na uwepo wa vilivyopo.
Ni scenario mbili tofauti.. hapo kwasababu najua all about saa.... ndio maana conclusion yangu itakuwa sahihi....

Je, Mungu ni saa????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Allah na Mungu... kwako wew unasema ni tafsiri tu lakini ni huyo huyo mmoja.... ndio nimekuja na hilo swali.

Je, unajua kwamba Allah na Yehova wana some attributes ambazo hazifanani????

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba twende kwa mtiririko... Ni andiko gani limesema hivyo? Nijibu hili halafu hayo mengine yatafuatia hakuna haja ya kuwa na haraka

Jr[emoji769]
 
Una akili au huna akili? Jibu NDIO au HAPANA...

Jr[emoji769]
Akili ni uwezo wa kufikiri, kuhoji na kung'amua mambo.

Nidhamu ya akili ni kuelewa ukweli. Kivipi? Kwa uyakinifu kwa ushahidi, na akili ya namna hii inapewa taswira ya akili yenye afya njema. Na muktadha wa namna huu ndiyo unaobeba dhana nzima ya Ubinadamu. Binadamu mwenye tija, binadamu aliye hai.

Watu wa imani nao wanautumia huu muktadha kwa maana: Kama akili ya mtu imeshindwa kufikiri, kuhoji na kung'amua kanuni na nidhamu ya Ulimwengu jinsi ulivyo kwa kuanza na wewe binafsi.

Kwa akili yenye kuhoji na kufikiri inajipa moja kwa moja yupo aliyevifanya hivi, ambaye ni Muumbaji. Uking'amua hayo akili yako ni akili yenye afya kwa sababu mazingira yenyewe yanajidhihirisha. Kinyume na hapo akili ya mtu inakuwa si yenye afya bali ni yenye uwalakini. Kwa muktadha huo itatafsirika akili yenye dosari, yaani hauna akili. Bi maana Akili haijatimia, haijawa na ukamilfu.

Lakini maana ya neno akili ni pana. Inategemea itatumiwa kwenye muktadha upi.
Ni mawazo yangu tu. Kusahihishwa ruhusa.
 
''kwa tafsiri rahisi atheist ni mtu asiyejua lolote kuhusu Mungu ama miungu (Hana ABC zozote kuhusu hizo imani za Mungu na miungu)"
Tafsiri uliyotoa hapa ni ya agnostic na wala sio atheist.
Kinara mbishi asiyekubali kuwa kuna Mungu. Mbishi kwa viwango vyote unavyojua ila mwepesi wa hoja.

Kiranga sio atheist, kwa tafsiri rahisi atheist ni mtu asiyejua lolote kuhusu Mungu ama miungu (Hana ABC zozote kuhusu hizo imani za Mungu na miungu)

Kiranga sio mmojawapo. Kiranga ni mmojawapo wa wale waliokengeuka imani, walizaliwa katika ukristo wakabatizwa na kuishi maisha ya ukristo... Lakini along the way wakabahatika kusoma doctrines za kikristo, Mungu nk.

Ni katika hizo doctrines wakashindwa kukubaliana na vifungu kadhaa hivyo wakakengeuka na kuwa wapinga Uwepo wa Mungu mkuu.

Ni watu wenye elimu kubwa kuhusu dini hasa ukristo halafu wakasoma na doctrines nyingine zinazopinga uwepo wa Mungu na kuchagua kuyaamini hayo.

Kipengele muhimu hawa watu wasio waaamini ni kule kutaka wanachokikwepa ni kile cha kutotaka kutambua kuwa ishu za kiroho, Kimungu hazina ithibati za kisayansi.

Wote tuna akili. Je, kuna ithibati? Na kama hatuna akili tuna ithibati? Lakini uhalisia unasemaje?

Kwahiyo Kiranga anataka umuoneshe Mungu as if ni kitu solid. Kiufupi hawa sio atheists bali non believers!!!

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
''kwa tafsiri rahisi atheist ni mtu asiyejua lolote kuhusu Mungu ama miungu (Hana ABC zozote kuhusu hizo imani za Mungu na miungu)"
Tafsiri uliyotoa hapa ni ya agnostic na wala sio atheist.

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
Ok atheist ni nani basi au atheism ninini

Jr[emoji769]
 
Nilichopinga ni wewe kusema Kiranga sio Atheist wakati maelezo yote uliyotoa yanaoonyesha yeye ni Atheist.
Sasa umepinga nini?

Jr[emoji769]

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Back
Top Bottom