Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Tafuta Quran usome mwenyewe.

Sura Al Baqarah 2:6 - 2:7

"Indeed, those who disbelieve - it is all the same for them whether you warn them or do not warn them - they will not believe.

Allah has set a seal upon their hearts and upon their hearing, and over their vision is a veil. And for them is a great punishment."

Mwisho wa nukuu.

Sasa huyu Mungu anafunga mioyo watu wasimjue, halafu wakikosa kumjua anawahukumu.

Ujinga mtupu.

Nikisema sitaki kukubali Mungu wa ujinga huu utanishangaa vipi?
Haya mavitabu ya dini yana too much ambuiguity ,hapo utaambiwa hujaitafsiri vizuri,
Nonsense this religions
 
Haya mavitabu ya dini yana too much ambuiguity ,hapo utaambiwa hujaitafsiri vizuri,
Nonsense this religions
Hata kama sijatafsiri vizuri, mimi kushindwa kutafsiri vizuri neno linalosemwa la Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kunaonesha Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo sio tu ningeweza kutafsiri vizuri, ningekuwa hata sina haja ya kutafsiri, kwa maana ningemjua moja kwa moja bila kusoma kitabu na bila ya kuwa na swali lolote juu ya uwepo wake.

Huu mjadala wa kuwepo Mungu huyo tayari ni ushahidi hayupo.

Angekuwepo, kungekuwa hakuna hata mjadala.
 
Hata kama sijatafsiri vizuri, mimi kushindwa kutafsiri vizuri neno linalosemwa la Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kunaonesha Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo sio tu ningeweza kutafsiri vizuri, ningekuwa hata sina haja ya kutafsiri, kwa maana ningemjua moja kwa moja bila kusomakitabu na bila ya kuwa na swali lolote juu ya uwepo wake.

Huu mjadala wa kuwepo Mungu huyo tayari ni ushahidi hayupo.

Angekuwepo, kungekuwa hakuna hata mjadala.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kwa mfano mnaanza kujadili eti TZ kuna raisi au hakuna rais wakati tayari yupo na mnamwona sasa ichukulie vice versa kwa upande Wa dini
Ni ujinga mtupu kwakweli
 
Sasa mbona wewe unaniuliza maswali mimi tu mfululizo nakujibu, maswali yangu hunijibu?

Taja sifa za Mungu wako kwanza.

Kiranga , hizo sifa haujaanza kuzisema leo na kila mjadala unaohusu uwepo wa Mungu, ukichangia huwa unazitaja.

Nimeomba jambo moja tu. Chanzo cha hizo sifa ulizozitaja za Mungu unaesema hayupo.

Kama haujataja chanzo ulichokinukuu ili tujue ndio sifa pekee au baadhi ya sifa, maswali yako mengine yanahitaji jibu la hili swali, vinginevyo tutavuruga lengo la kuuliza swali.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kwa mfano mnaanza kujadili eti TZ kuna raisi au hakuna rais wakati tayari yupo na mnamwona sasa ichukulie vice versa kwa upande Wa dini
Ni ujinga mtupu kwakweli
Dini/ Mungu nikama hela.

Nikitu ambacho kimetengenezwa na watu.

Ukisema Mungu yupo, ni sawana kusemanoti ya sh elfu kumi ina thamani ya vitu inavyonunua kwa sh elfu kumi.

Watu wameipa thamani ile, na kesho Magufuli akisemahiinotitunaibadilisha, inakuwa haina thamani.

Mungu naye kawekwa juu pale na watu tu, wamemtungatunga kwa kumuunga unga tu.

Ndiyo maana ukisoma habari za kuwepo kwake zina ujinga mkubwa sana.
 
Kiranga , hizo sifa haujaanza kuzisema leo na kila mjadala unaohusu uwepo wa Mungu, ukichangia huwa unazitaja.

Nimeomba jambo moja tu. Chanzo cha hizo sifa ulizozitaja za Mungu unaesema hayupo.

Kama haujataja chanzo ulichokinukuu ili tujue ndio sifa pekee au baadhi ya sifa, maswali yako mengine yanahitaji jibu la hili swali, vinginevyo tutavuruga lengo la kuuliza swali.
Wewe unataka nikujibu maswaliyako tu? Yangu hutaki kujibu?

Basi na mimi sitaki kujibu yako, tuone kama utaweza kuendeleza mjadala nami kwa kutaka kuniuliza mimi tu, bila kunijibu.

Unaelewa maana ya neno "reciprocity" ?
 
Vitabu vinavyosemwa kuwa ni vya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuhitaji ufafanuzi ni ushahidi mwingine Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo, siyo tu vitabu vyake visingehitaji ufafanuzi, tusingehitaji hata vitabu kumuelewa.
Huo ni utoto Kiranga hasa kwa heshima yako uliyonayo humu,kuna atheists kibao wanafuatilia hoja zako.
 
Wewe unataka nikujibu maswaliyako tu? Yangu hutaki kujibu?

Basi na mimi sitaki kujibu yako, tuone kama utaweza kuendeleza mjadala nami kwa kutaka kuniuliza mimi tu, bila kunijibu.

Unaelewa maana ya neno "reciprocity" ?

Kiranga kama unashindwa kuleta chanzo chako cha sifa za Mungu unaedai hayupo lakini umezitaja hapo juu tena zaidi ya mara moja. Tunajadili nini?
 
Kiranga kama unashindwa kuleta chanzo chako cha sifa za Mungu unaedai hayupo lakini umezitaja hapo juu tena zaidi ya mara moja. Tunajadili nini?
Wapi nimekwambia nashindwa?Unawezaje kufikia hitimisho hilo kwamba nashindwa?

Nimekwambia hunifanyii haki wewe kuniuliza maswali mimi nakujibu wewe tu wakati wewe hujibu maswali yangu.

Jibu swali langu uone kama nitashindwa kukupa references.

Sifa za Mungu wako ni zipi?

Jibu, na mimi nitakujibu.

Kama hunijibu, naona unanivunjia heshima.

Sikujibu.

Sasa hapo utasemaje nimeshindwa kujibu?
 
Kama kweli dini ni useless onyesha kwa vitendo... Anza kubadili jina ulilonalo sasa... Naamini una jina lako la kibantu... Likane hili la Emmanuel (Mungu pamoja nasi) kuthibitisha maneno yako... Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa
Sehemu karibia zote ambako dini zilianzia ndiko pametawaliwa na vita,mfano Israel na Palestina.

Lakini pia Damascuss (Syria), Iraq (Babeli ya zamani) na hata miaka ya hivi karibuni huko Misri.

Magaidi wa dunia wa leo hii wanaua huku wakiwa wamejificha nyuma ya dini,mfano Bokoharam, Alishabab,Ant-Baraka na Seleka kule Afrika ya kati,bila kusahau kundi la Al-qaeda.

Kusema nibadili jina langu kisa hicho ukisemacho ni sawa na kumwambia Mwanachadema aache kuishabikia Yanga kisa inatumia rangi za jezi zenye mfanano na wa rangi za Chama cha Mapinduzi,

Unasahau kuwa rangi za kijani na njano zimekuwepo hata kabla ya kuwepo kwa Yanga,Chadema na Ccm.

Kama wenye majina ya Emmanuel ndiyo wanatakiwa kuwa wafuasi wa biblia maana yake wewe hukupaswa kuwa miongoni mwa washabikia
dini.

Kwa kumbukumbu zangu hakuna kitabu cha dini chenye jina Mshana Jr ndani yake.

Na kwa kuwa vitabu hivyohivyo vinavyosema maana ya Emmanuel ni hiyo uliyosema,ndiyo vimeleta contradictions za uwepo wa Mungu,basi ni ngumu kuiamini hiyo maana.

Labda utumie kitabu kingine kisicho na mkanganyiko,nami ntapima.
 
Wapi nimekwambia nashindwa?Unawezaje kufikia hitimisho hilo kwamba nashindwa?

Nimekwambia hunifanyii haki wewe kuniuliza maswali mimi nakujibu wewe tu wakati wewe hujibu maswali yangu.

Jibu swali langu uone kama nitashindwa kukupa references.

Sifa za Mungu wako ni zipi?

Jibu, na mimi nitakujibu.

Kama hunijibu, naona unanivunjia heshima.

Sikujibu.

Sasa hapo utasemaje nimeshindwa kujibu?

Siwezi kukuvunjia heshima.
Kama unaweza si ulete chanzo chako cha hizo sifa ulizozitaja? Uone kama ntasema umeshindwa.

Hilo ndio swali la mwanzo, kutokuleta chanzo na hapohapo kutaka nikujibu maswali yako sio sawa.

Au kama ni maoni yako napo unawezasema ili tusiendelee kusubiria ulipotoa hizo sifa za Mungu asiyekuwepo.
 
Unataka nikujibu wewe tu, mimi hunijibu.

Sikujibu.
 
Vitabu vinavyosemwa kuwa ni vya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuhitaji ufafanuzi ni ushahidi mwingine Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo, siyo tu vitabu vyake visingehitaji ufafanuzi, tusingehitaji hata vitabu kumuelewa.
Ni Makuzi Tu.. hatua kwa hatua kila mmoja anapata anachostahili kwenye sahani moja na anashiba ipasavyo.!

Ni akili kubwa tu inayoweza hayo.

"Gharamia mwenye weka mkono upapase..ukikutacho Ndo saizi Yako"

Ulichoshindwa wewe si chakula ni uwezo wako uliishia Hapo.

Wewe ni kama kijana aliyepevuka, hawezi rudia kunyonya,Ila pia bado hawezi kufanana na Baba.

Hulka ya kujitegemea kabla ya Mda inakutesa.Huna jipya.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Unalazimisha hoja tu.
 
Quran inatyambia kwamba kuna watu fulani wabishi. Wanaoamini Mu gu hata wasijishuvhulishe nao hawa watu.

Kwa sababu Mungu mwenyewe kaifanya mioyo yao kuwa mizito kumjua Mungu. Allah kawaziba macho na masikio hawa watu wasimjue.

Halafu siku ya kiama atawahukumu na kuwachoma moto.

Kwa sababu hawajamjua Mungu.

Eboo?

Huyu Mungu ana kichaa?

Yani yeye Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote, kawaziba watu hawa masimio na macho, kawafanya mioyo yao iwe mizito kumjua Mungu.

Halafu hawakumjua Mungu.

Kwa sababu Mungu kapanga hivyo kwa makusudi. Na anachopanga hakipingiki.

Halafu wakikosa kumjua Mungu tena wanaadhibiwa kwa kutomjua Mungu?

Yani watu wanasoma hiki kitabu na kumkubali huyu Mungu yupo kweli?
Mkuu quran ni mashairi hakuna kitabu mule uzuri wake ni kwa kiarabu ukitafsiri majanga matupu hawasomi wanaimba kama nyimbo
 
Back
Top Bottom