Uingereza yapunguza bajeti Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingereza yapunguza bajeti Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 30, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Andrew Mitchell
  • YATOA ASILIMIA 30 KWENYE FUNGU LA BAJETI
  SERIKALI ya Tanzania imepata pigo kiuchumi baada ya Uingereza kupunguza msaada wake katika fungu la bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/12 kwa asilimia 30, Mwananchi Jumapili limebaini. Hatua hiyo ya Uingereza kupitia Idara ya yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), imekuja wakati nchi wahisani zinazochangia bajeti ya serikali (GBS), zikisema zitapitia misaada ya fedha wanazotoa ili kujua kama serikali imefikia malengo yaliyokusudiwa. Jumla ya Washirika wa Maendeleo (DPs) 12 wanasaidia bajeti ya Tanzania, ambapo kwa mwaka huu wa fedha, nchi hizo zilitoa kiasi cha Dola 453 milioni.

  Hata hivyo, katika mchango wao wa bajeti ya mwaka huu wahisani wamezuia kiasi cha Dola 100 milioni( karibu Sh170bilioni) ambazo zitatolewa iwapo nchi hizo zitaridhishwa na utendaji wa Serikali katika maeneo mbalimbali. Katika mwaka wa fedha 2010/11 nchi hizo zilitoa Dola 534 milioni ( karibu Sh907.8 bilioni) kuchangia bajeti ya serikali.

  Hatua ya kuzuiwa kwa kiwango hicho cha msaada wa Uingereza kwenye bajeti inatokana na serikali kushindwa kusimamia vizuri masuala mbalimbali, kubwa ikiwa ni mazingira ya uwekezaji na kupambana na umasikini, kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Andrew Mitchell. Mitchell katika barua yake ya Agosti 3, 2011 kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Uchumi ya Bunge la Mabwanyenye la Uingereza (House of Lords), amesema mawaziri wa Uingereza na serikali yake kwa ujumla wamekuwa wakisisitiza Tanzania kuimarisha mazingira ya kufanya biashara kama njia muafaka ya kupunguza umasikini............

  zaidi soma gazeti Mwananchi
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ule mzimu wa Serikali ya Kikwete kutegea wahisani kama njia ya kuendesha shughuli za utawala, maendeleo na huduma za umma umeingia dosara kwa mara nyingine tena wakati baadhi ya nchi washiriki wa kutoa bajeti ya serikali kusitisha kwa kupunguza kiwango ikiwepo nchi ya Uingereza.

  Hoja ya sera za Chama cha Chadema ya kuondokana na bajeti tegemezi na kujenga msingi wa kujitegemea kwa kutumia rasilimali na kodi inazidi kuiweka Serikali ya CCM kwenye rehani kwa chama cha Chadema, na ipo siku serikali ya CCM itakuja kuridhia ilani ya Chadema inayotekelezeka kuliko kuendelea kupitisha bakuli kama mzee Matonya wakati uwezo tunao.
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Mwenye macho aone,mwenye sikio naye asikie!mwenye akili timamu aachane na upuuzi wa CCM!Hivi nchi iliyobarikiwa na rasilimali nyingi inashindwa kutumia rasilimali kukuza uchumi wake?kila kukicha wanatembeza bakuli kuomba msaada!Mi naona waingereza wako sawa kabisa!!ngoja tupate shida labda akili zetu zitafunguka!SHAME ON CCM
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  what did you expect with uchumi wao kuyumba, na sisi wenyewe kutokua accountable enough?
   
 5. k

  king11 JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  waingereza wapumbavu yani wanatoa msaada na wenyewe wanaenda kuomba msaada kwa china
   
 6. mkolosai

  mkolosai JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Nani kakwambia wameenda china kuomba? Leta evidence.Umesoma hivo vigezo? Sio kukurupuka tu.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wao wenyewe wamefulia huko kwao ndo maana ya kwenda Libya na kupoteza ushahidi wa madeni ya mafuta wanayodaiwa na Gadafi. Ndio magamba watie akili sasa.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaka fuatilia habari. Mkurupukaji ni wewe.
   
 9. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Msaada wao kwanza hauna maana hata kidogo!, ni wa kutufanya tuendelee kujiona kama bila wao hatuwezi (mental slavery). waende zao na msaada wao na sisi tuanze kuuza madini yetu (sio sasa ambapo tumewapa bure) na tutoze kodi (badala ya mrahaba) uone kama tutapata shida yoyote. Msaada siku zote huwa wanatoa kwa faida yao (ikiwa ni pamoja na kufuta historia mbaya ya ukoloni) wala sio kwa faida yetu. Ningefurahi kama wangefuta kabisa tukajifunza kwa vitendo kujitegemea
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  We did not understand umuhimu wa siasa ya ujamaa ba kujitegemea. Hata kama ujamaa ulikuwa haufai,na kujitegemea kulikuwa na dosari gani? Anyway tumeasisi siasa za kuomba omba na kujikomba kwa wale tunaowaita wahisani. Tunavuna tulichopanda
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,514
  Likes Received: 19,932
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen, width: 870"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Uingereza yaipiga nyundo serikali
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 29 October 2011 20:17
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  YATOA ASILIMIA 30 KWENYE FUNGU LA BAJETI Claud Mshana
  [​IMG]Andrew Mitchell


  SERIKALI ya Tanzania imepata pigo kiuchumi baada ya Uingereza kupunguza msaada wake katika fungu la bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/12 kwa asilimia 30, Mwananchi Jumapili limebaini.

  Hatua hiyo ya Uingereza kupitia Idara ya yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), imekuja wakati nchi wahisani zinazochangia bajeti ya serikali (GBS), zikisema zitapitia misaada ya fedha wanazotoa ili kujua kama serikali imefikia malengo yaliyokusudiwa. Jumla ya Washirika wa Maendeleo (DPs) 12 wanasaidia bajeti ya Tanzania, ambapo kwa mwaka huu wa fedha, nchi hizo zilitoa kiasi cha Dola 453 milioni.

  Hata hivyo, katika mchango wao wa bajeti ya mwaka huu wahisani wamezuia kiasi cha Dola 100 milioni( karibu Sh170bilioni) ambazo zitatolewa iwapo nchi hizo zitaridhishwa na utendaji wa Serikali katika maeneo mbalimbali. Katika mwaka wa fedha 2010/11 nchi hizo zilitoa Dola 534 milioni ( karibu Sh907.8 bilioni) kuchangia bajeti ya serikali.

  Hatua ya kuzuiwa kwa kiwango hicho cha msaada wa Uingereza kwenye bajeti inatokana na serikali kushindwa kusimamia vizuri masuala mbalimbali, kubwa ikiwa ni mazingira ya uwekezaji na kupambana na umasikini, kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Andrew Mitchell. Mitchell katika barua yake ya Agosti 3, 2011 kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Uchumi ya Bunge la Mabwanyenye la Uingereza (House of Lords), amesema mawaziri wa Uingereza na serikali yake kwa ujumla wamekuwa wakisisitiza Tanzania kuimarisha mazingira ya kufanya biashara kama njia muafaka ya kupunguza umasikini.

  “Hatua za kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji zimehusishwa katika kitengo cha ufuatiliaji wa misaada kwenye bajeti unaotolewa na Uingereza,” “Mwaka huu nimepunguza msaada wa Uingereza kwenye bajeti ya Tanzania kwa asilimia 30, kuonyesha kuwa tuko makini katika hili,” alisema Mitchell katika barua hiyo.

  Mei 2010, Mitchell, aliiagiza Tume ya Mapitio ya Misaada (Bilateral Aid Review) kuchunguza kwa makini nchi ambazo DFID inafanya kazi kupitia programu za Uingereza za moja kwa moja za nchi na kanda. Mapitio hayo kwa mujibu wa mpango kazi wa DIFD nchini wa mwaka 2011 – 2015, yalitazama njia bora ambazo Uingereza inaweza kutumia kupambana na umaskini na kuhakikisha unakuwepo ufanisi wa kila fedha ya nchi hiyo inayotumika. Machi 2011, matokeo ya mapitio hayo yalitangazwa ambapo pamoja na mambo mengine, walifanya mapitio ya misaada inayotolewa kwa nchi mbalimbali. “Mapitio hayo yalifanya tubadili kidogo mtazamo wa programu zetu na yametufanya tulenga nchi chache zaidi ili misaada yetu iende pale ambapo italeta tofauti na pale palipo na mahitaji makubwa,” inasema sehemu ya mpango kazi huo wa DIFD wa miaka mine kuanzia 2011.

  Mapitio hayo pia yamependekeza DFID Tanzania kupunguza kutumia mfumo wa kupitisha msaada kwenye Bajeti ya Serikali (General Budget Support), kama tathmini ya programu ya nchi ya mwaka 2010 ilivyoshauri. “Tathmini hii ilionyesha kuwa katika hali ya sasa, kupitisha msaada kwenye bajeti ya serikali si njia yenye ufanisi zaidi ya kuwasilisha matokeo ya misaada yetu na ilipendekeza tupunguze matumizi ya mfumo huo.” Naibu Waziri wa Fedha Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima, alisema uamuzi huo wa Uingereza hautaiathiri serikali kwani ilishapanga bajeti kulingana na kiasi cha fedha walichokwisha fahamu kuwa watakipata.

  “Unajua tunapopanga bajeti, tunajua wafadhili wanatoa nini, kwa hiyo taarifa tunapoipata kuwa fulani atapunguza, inakuwa iko nje ya bajeti yetu,” alisema Silima. Alifafanua kuwa kiasi kilichoingizwa kwenye bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/12 ni kile ambacho kiliahidiwa kutolewa na kuongeza kuwa bajeti haitadhurika kwani kama ni kutafuta njia mbadala, serikali ilishafanya hivyo tayari. Alikiri kuwa taarifa ya kupunguzwa kwa kiasi hicho cha fedha kwenye mchango wa bajeti walishaipata kwenye vikao vya awali vya kupanga bajeti na kuongeza: “Kuna wakati tunakuwa na vikao vya kuulizana ambapo kila nchi husema kile ambacho itachangia katika bajeti ya mwaka husika.”

  Alipoulizwa kuwa kama Uingereza ilitoa sababu ya kupunguza fedha hizo, Silima alisema nchi hiyo ilibadilisha utaratibu kulipoingia serikali mpya. “Unajua serikali ni nyingine kwa hiyo zile taratibu zilibadilishwa na walipunguza nchi nyingi katika orodha ya nchi walizokuwa wakizisaidia,” alisema Silima. John Mnyika Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika aliitaka Uingereza kuweka wazi sababu za kupunguza misaada kwani kuna mambo mengi ambayo nchi wahisani wa maendeleo hawaridhiki nayo lakini hawaweki wazi. Aliongeza kuwa wadau wa maendeleo hawaridhiki na jinsi Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia ufisadi, hususan suala la EPA.

  “Baada ya EPA kujadiliwa bungeni, Serikali ya Tanzania ilikubaliana na wahisani kutengeneza mpango kazi wa kushughulikia ufisadi wa EPA, sasa hawaridhishwi na jinsi hatua zinavyokwenda,” alisema Mnyika. Aliongeza kuwa wahisani hao bado hawaridhishwi na jinsi serikali inavyoshughulikia mianya ya ubadhilifu wa fedha za bajeti ndani ya serikali. “Sehemu kubwa ya pesa za bajeti zinaishia mikononi mwa mafisadi badala ya kuwafikia wananchi na kuendeleza miradi yao,” aliongeza.

  Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, aliongeza kuwa sababu nyingine ya Uingereza kupunguza misaada yake kwa nchi nyingi, ni mgogoro wa kiuchumi kwa nchi za ukanda wa Ulaya hususan tatizo la madeni linalozikabili nchi hizo hivi sasa. Alishauri kupunguzwa kwa matumizi yasiyo ya lazima ya serikali ili kufidia upugufu huo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 12. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana, kwani mwisho wa siku hizo pesa za bajeti asilimia kubwa zinaishia mikononi mwa mafisadi na familia zao..bora walivyopunguza hiyo bajeti tukose wote.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,514
  Likes Received: 19,932
  Trophy Points: 280
  bora mboga na ugali vimwagike sio?
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,514
  Likes Received: 19,932
  Trophy Points: 280
  misaada imepunguzwa kwa vile rais ni mwislamu
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mods unganisha hii thread zinajazana tu bila mpango
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Watanzania tunapenda kupewa,tunapenda misaada,hatupendi kujitegemea tumefikia hatua hatufanyi kazi kujiletea maendeleo hata katika ngazi za chini tunailalamikia serikali,tunawalilia wafadhili...huu ni umaskini wa mawazo..hivi ni nani atakuwa mzalendo ampelekee jirani yake maendeleo wakati yeye ana matatizo?
   
 17. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  safi kabisa Uingereza na Nchi zote wahisani,ikiwezekana msitupe hata sumni ili inayojiita serikali ibadilike kwa kuacha kuombaomba. Nalog off
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,028
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Mpumbavu ni muhongwa suti,hakuna cha maana alichofanya zaidi ya kusafiri na kutoa takwimu fake za uchumi wa nchi,watu wanaiba mali yeye anachekelea tu,hajawahi kuchukua hatua hata siku moja,misaada yenyewe wanayopewa inaishia kwenye mifuko ya watu wachache,jamani eeh ccm haitufai kabisa inazidi kutuangamiza tuitose.
   
 19. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  bora walivyopunguza kwani mafisadi ndo wananufaika nayo.
   
 20. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sera ya maendeleo ya serikali yenu ni kuombaomba kwa matajiri. Jamaa huwa anajisifia eti yeye anatafuta wawekezaji na misaada huko nje ndo maana anasafiri sana! Wako bize na vikoao vya kutengeneza sera mbalimbali lakini kuzitekeleza kwa vitendo hamna. Sasa hivi wamekuja na Kilimo mwisho lakini hamna kiongozi hata mmoja anaye spearhead hii kitu wote wako mjini wanasubiri wakulima waitekeleze wenyewe! Mchonga alikuwa bize kufatilia huko kijijini kama anachokisema kinatekkelezwa. Leo hii viongozi waoni watu wa kukwea pipa tu kila siku wakienda kwenye mikutAno ambayo angeweza kuhudhuriwa hata na mbunge tu sisi anaenda Raisi au waziri mkuu.
  Tumejaribu,tumeshindwa na tunarudi nyuma -miaka 50 ya Tanganyika.
   
Loading...