Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

sababu moja ni.kua hakuna kitu chochote kinachoeza kutokea au kujiumba bila kuundwa kwa hio dunia na vilivyomo vyote vimeumbwa na alieviumba ndio mungu...nami nakuuliza niambie kitu kinachoeza tokea chenyewe tuh

Hehehe, unaona sasa uwezo wa kufikiri ulivyo mdogo?
Unasema hakuna chochote kinachoweza kujiumba bila kuundwa, haya niambie mungu imekuaje yeye akajiumba? au na yeye aliumbwa na mungu mwingine? na huyo mwingine alijiumbaje? Unaongea sentensi ambayo inajifunga yenyewe.
 
Twende mdogo mdogo
1. Umeuliza swali nami nimekujibu
2. Jibu langu pengine halijakufurahisha sana.. Mpaka umetumia neno KUCHAMBA WENZAKO! hapa umepotoka vibaya sijamchamba mtu bali tumeendelea kubishana kwa hoja
3. Umesema kila mtu ana imani yake hii inaweza kukugharimu maelezo ya kina kama nikiamua kukuuliza kama Atheism ni imani ama sio imani..
4. Kitu kinachoitwa imani hakina ithibati za kidunia kwakuwa ni cha kiroho....
5. Umezungumzia kuhusu smart phone... Hapa nimepapenda mno na labda unijibu kama unaweza kujua kwa hakika kwanini tunaweza kuwasiliana mimi na wewe kupitia hizi simu janja....
Je ni hizi vitu tulivyoshika na kubofya ndio vinafanya tuwasiliane?
Vipi kuhusu chaji
Vipi kuhusu network
Vipi kuhusu bundle
Vipi kuhusu software
Vipi kuhusu number ya simu
Vipi kuhusu IP address
Vipi kuhusu User ID
Mpaka tunaweza kuwasiliana hivi ni mchakato mrefu usioonekana... Zaidi ya
Siku tulizoshika mikononi
Maandishi tunayoandika
Minara ya simu nknk
Kwenye kila kitu kuna software na hardware...
Software haina ithibati ama proof ya kuonekana kwa macho so the God, hardware inaweza kuonekana kwa macho, na ukaipima kwa vipimo, ukaipa uzito na ujazo, ukaipa rangi nk
Na hapa ndio tunapopishana uelewano

Atheism sio imani, ni ukosefu wa imani kwa mungu, ukosefu wa imani sio kuamini kua kitu hakipo.
Naweza kukujibu kila kitu kuhusu simu inakuaje hadi tunawasiliana, nimesoma computer engineering na nilikua mzuri kwenye physics na hesabu, naelewa very deep jinsi hivi vitu vinavyofanya kazi infact nishafanya kazi kampuni kubwa ya kutengeneza electronics duniani nikadeal na chips ndogo kabisa so nimeona na kushiriki directly kutengeneza from scratch, hakuna muujiza hapa ni mambo yanaelezeka vizuri, pure science hakuna ujinga ujinga, sio maduduwasha mnayoamini kua binadamu tunawekwa chumba kingine huku aliens wanakaa kututengenezea betri sisi tunaenda kuchukua tu, hahaha, betri hazisushwi toka mbinguni, tunatengeneza wenyewe.

Uliza hata mtu aliyesoma electrical anayeweza tengeneza pcb boards atakwambia, sio muujiza, inahitaji akili tu.

Kama ushauri tu kwa watanzania, ukiingia google, usianze kwa kusearch "alien, area51" em jaribu kuanza na "physics, chemistry, mathematics, software, artificial intelligence e.t.c" vitu ambavyo vimekua proved over and over again na unavitumia, sio unakomaa kutafuta vitu ambavyo hakuna aliyewahi kuprove, hakuna aliyewahi kuona, wewe hujawahi ona, mnakaa kuzidi kudanganyana tu, unatumia simu tumetengeneza, leta kitu ambacho umewahi tumia kilichotengenezwa na mchawi.
 
Unajuaje kuna aliyeanzisha - aliyeanzisha maana yake kuna mtu/Mungu/ some being mwenye consciousness- na ulimwengu haujaanza kwa kitu kingine tofauti usichokijua bado kama ambavyo sisimizi anaweza kuwa hajui hesabu za string theory?
Nimeupa tu consciousness kama heshima kulingana na uwezo wangu wa kifkra.

Na pia nimeeleza kwamba kile kianzilishi/ mwanzilishi wa huu ulimwengu, kwangu hicho/ huyo ndio mungu!!

Na nikakazia kwamba, habari zenye uhakika kama vile kuwa hicho kianzilishi, mwanzilishi ni being mwenye consciousness mimi sizifahamu na in fact sina.
 
Kwa hiyo unakubali kwamba kuupa mwanzo huu consciousness ni makosa?

Unajua kwamba dhana nzima ya cause and effect, ambayo inaleta habari nzima ya kianzilishi/ muanzilishi inaweza kuwepo kama tunaangalia ulimwengu katika upeo (level) wetu tu.

Unaelewa kwamba ukizama katika upeo wa chini kabisa kwenye kwanta huko, dhana ya kwamba hiki kitasababisha kile kwa sababu hiki kimeanza kabla ya kile inavunjika?

Kwa sababu dhana nzima ya muda inavunjika na kuwa tegemezi wa mengine?

Unaelewa hayo?

Unaelewa kwamba ukishikilia xhana ya kianzilishi kuwa ni kitu cha kazima, hata Mungu naye atahitaji kinzilishi, na hivyo atakuwa si Mungu?

Unaelewa kwamba dhana hiyo inaonesha kwamba hakuna Mungu?
 
Hitimisho ni nini?Tuache kufanya ibada tusubiri kuwa mbolea ?
Japo sijakuelewa lakini ibada si chakula cha mwili bali cha roho... Huo mwili ni kasha tu lenye lifespan fupi sana
 
Atheism sio imani, ni ukosefu wa imani kwa mungu, ukosefu wa imani sio kuamini kua kitu hakipo.
Naweza kukujibu kila kitu kuhusu simu inakuaje hadi tunawasiliana, nimesoma computer engineering na nilikua mzuri kwenye physics na hesabu, naelewa very deep jinsi hivi vitu vinavyofanya kazi infact nishafanya kazi kampuni kubwa ya kutengeneza electronics duniani nikadeal na chips ndogo kabisa so nimeona na kushiriki directly kutengeneza from scratch, hakuna muujiza hapa ni mambo yanaelezeka vizuri, pure science hakuna ujinga ujinga, sio maduduwasha mnayoamini kua binadamu tunawekwa chumba kingine huku aliens wanakaa kututengenezea betri sisi tunaenda kuchukua tu, hahaha, betri hazisushwi toka mbinguni, tunatengeneza wenyewe.

Uliza hata mtu aliyesoma electrical anayeweza tengeneza pcb boards atakwambia, sio muujiza, inahitaji akili tu.

Kama ushauri tu kwa watanzania, ukiingia google, usianze kwa kusearch "alien, area51" em jaribu kuanza na "physics, chemistry, mathematics, software, artificial intelligence e.t.c" vitu ambavyo vimekua proved over and over again na unavitumia, sio unakomaa kutafuta vitu ambavyo hakuna aliyewahi kuprove, hakuna aliyewahi kuona, wewe hujawahi ona, mnakaa kuzidi kudanganyana tu, unatumia simu tumetengeneza, leta kitu ambacho umewahi tumia kilichotengenezwa na mchawi.
Nimekuuliza maswali rahisi sana Graph.. Ila naona umeishia kujisifia na kutoa ushauri kwa watanzania
Kwa kiwango chako hicho cha elimu ulichonacho sidhani kama ungeshindwa kabisa kujibu swali walau moja moja...
Kujibu kwa usahihi hayo maswali ndio kutathibitisha kiwango chako cha elimu, umahiri katika tech na kufanya kazi kwenye kampuni kubwa.....
Kumbuka hata mtunza bustani wa ikulu akiulizwa unafanya wapi kazi atasema ikulu
. hatujivunii tumesoma kiasi gani na kupata madaraja mangapi kielimu
. hatujivunii umahiri wa kufaulu mitihani na kupata alama za juu
. hatujivunii tumeisafiri dunia na kupata maarifa kiasi gani
. hatujivunii kusoma doctrines mahiri za wasomi wafu waliosifika enzi zao. Wanafizikia, watheolojia, wakemia, wanafilosofia, wanasaikolojia nknk

Huwa daima tunajivunia UELEWA na UWEZO wa kutafsiri na kupambanua mambo katika mazingira tuliyokuwa nayo kwa muktadha na mtazamo binafsi kuliko kuishia kukariri mabandiko ya wengine kama ndio uhalisia
 
Hujaelewa vizuri.

Mungu wako angekuwepo, kungekuwa hakuna haja ya kuomba.

Angeumba ulimwengu ulio perfect kiasi kwamba kuomba - kitu kinachotokana na kukosa- kusingewezekana.

Kwa sababu kungekuwa hakuna kukosa.
Nafikiri na mie hujanielewa,wewe unazungumza katika hali ya kufikirika na ndiyo maana unatumia sana neno "ange.." ila mie nazungumza katika uhalisia,wewe unaongea katika hali ya ya kuondoa uwepo wake na mie nazungumza katika hali ya uwepo wake.

Kwako wewe sifa za mungu zinaanza na kuishia kwenye uumbaji wa ulimwengu tu,na ndiyo maana muda wote umekuwa ukisema mara angeumba hivi nasi vile kana kwamba huu ulimwengu ndiyo mungu mwenyewe.

Ila mie namzungumzia Mungu zaidi ya sifa hizo unazozitaja humu,namzungumzia mungu zaidi ya kuumba huu ulimwengu.

Unaona hapo tatizo lilipo? na ndiyo maana nakwambia mie sio Mungu hivyo kuomba sio ajabu maana sina uwezo wote wala ujuzi wote.
 
Unaelewa kwamba unaweza kuelewa pi mpaka decimal places 4 lakini tukiipeleka kwenye decimal places 10 ukawa huelewi?

Na hapo kati kunawezekana kuwepo point unayoshindwa kuielewa ambayo mwalimu anaweza kutaka kuitafuta kukutoa kwenye kutokuelewa na kukupeleka kwenye kuelewa?

Na kwa wakati mmoja huo huo ukawa huelewi (kwa kiwango cha decimal places 10) na unaelewa (kwa kiwango cha decimal places 4) ?

Unajibizana na mimi?

Jibu pist yangu namba 1994.
Hiyo pi ikiwa kwenye decimal places 4 au decimal places 10 kunaifanya isiwe pi?

Unajuaje upeo wangu wa uelewa ambao umeuita mdogo kwamba naweza kuelewa hata huu mfano achilia mbali hizo decimal places 4 za pi?

Haukuamua kujibu swali la mfano nilioutoa mimi kitambo, na ukasema tusihusishe kiwango cha uelewa wa msomaji, wewe huyo huyo umerudi huko, haiendi hivyo.

Nauliza tena, uelewa wangu umekua kiasi cha kujibizana na wewe? Au na hili utasema haukusema?
 
Japo sijakuelewa lakini ibada si chakula cha mwili bali cha roho... Huo mwili ni kasha tu lenye lifespan fupi sana
Kwa vile umeelezea kwa marefu kuwa Mungu hayupo na tukifa tutakuwa mbolea tu.Swali langu ni "Je tuache kufanya ibada inayotuimarisha kiroho na tusubiri tu kuwa mbolea baada ya kifo?
 
Kwa vile umeelezea kwa marefu kuwa Mungu hayupo na tukifa tutakuwa mbolea tu.Swali langu ni "Je tuache kufanya ibada inayotuimarisha kiroho na tusubiri tu kuwa mbolea baada ya kifo?
Mzee kanisome tena... Nimeeleza kwa mitazano mitatu
1. Nimeeleza kwa wanaoamini katika Mungu mmoja
2. Wanaoamini katika miungu
3. Wasioamini katika Mungu wala miungu...
 
Hahaha duh! aisee watu sijui mna akili zinafikiria vipi, hivi mungu ambaye hajaonwa na mtu hata moja kati ya mabilioni waliowahi kuishi unakuja kulinganisha na kukosekana ushahidi mahakamani? Aisee umenichekesha, so hiyo ndo evidence yako kua mungu yupo? Basi kwa sababu hiyo tuseme thor, zeus, na greek gods wengine wote wapo maana hakuna mwenye ushahidi ila kuna watu walisema kua waliwaona.

Wabongo mmefungwa kwenye jela la dini ambalo ni la kijinga sana, mnakaa kuishi kwa kuoga wa kijinga kuogopa vitu ambavyo havipo, hahaha, toka zunguka duniani ujionee maisha, nchi ambazo population kubwa hawana dini cha kushangaza ndizo zinaongoza kwa utulivu, amani, furaha, sio bongo mnajidanganya tu. Waafrika dini zimewavuruga sana vichwa. Hamtokuja kuendelea kamwe 95% ya population mnaamini upuuzi.

Hakuna niliposema huo ndiyo uthibitisho wa kuwepo mungu na wala sipo hapa kufanya hivyo,nimeeleza hivyo ili uone hali ya ushahidi ilivyo katika uhalisia,ushahidi haufanyi jambo liwepo au lisiwepo.

Kuja hapa kusema hakuna uthibitisho wa kuwepo mungu na mungu hajawahi kuonekana,inaonesha ni jinsi gani ulivyo mjinga na hujui unachokipinga.
 
Mzee kanisome tena... Nimeeleza kwa mitazano mitatu
1. Nimeeleza kwa wanaoamini katika Mungu mmoja
2. Wanaoamini katika miungu
3. Wasioamini katika Mungu wala miungu...
Wewe binafsi uko katika fungu lipi?
 
Hehehe, unaona sasa uwezo wa kufikiri ulivyo mdogo?
Unasema hakuna chochote kinachoweza kujiumba bila kuundwa, haya niambie mungu imekuaje yeye akajiumba? au na yeye aliumbwa na mungu mwingine? na huyo mwingine alijiumbaje? Unaongea sentensi ambayo inajifunga yenyewe.

Una tatizo la kujihisi una upeo mkubwa wa kufikiri,na ndiyo maana mnadhani kusema kwenu hakuna mungu ni dalili ya mtu msomi.

Yani unakuja kuuliza imekuaje mungu kajiumba?? duh? mna uhuru wa kuuliza upuuzi kwa kweli.
 
Nimekuuliza maswali rahisi sana Graph.. Ila naona umeishia kujisifia na kutoa ushauri kwa watanzania
Kwa kiwango chako hicho cha elimu ulichonacho sidhani kama ungeshindwa kabisa kujibu swali walau moja moja...
Kujibu kwa usahihi hayo maswali ndio kutathibitisha kiwango chako cha elimu, umahiri katika tech na kufanya kazi kwenye kampuni kubwa.....
Kumbuka hata mtunza bustani wa ikulu akiulizwa unafanya wapi kazi atasema ikulu
. hatujivunii tumesoma kiasi gani na kupata madaraja mangapi kielimu
. hatujivunii umahiri wa kufaulu mitihani na kupata alama za juu
. hatujivunii tumeisafiri dunia na kupata maarifa kiasi gani
. hatujivunii kusoma doctrines mahiri za wasomi wafu waliosifika enzi zao. Wanafizikia, watheolojia, wakemia, wanafilosofia, wanasaikolojia nknk

Huwa daima tunajivunia UELEWA na UWEZO wa kutafsiri na kupambanua mambo katika mazingira tuliyokuwa nayo kwa muktadha na mtazamo binafsi kuliko kuishia kukariri mabandiko ya wengine kama ndio uhalisia
Mkuu umemaliza kila kitu. Tatizo hawa jamaa wanahusisha elimu na hiyo imani yao ya hakuna,utafikiri shule walienda wao tu na hii dunia inaongozwa na wao tu.

Kuna vitu vyengine ni upuuzi uliyopitiliza.
 
Hivi kuna neno lenye tafsiri moja?
Kila neno lina tafsiri nyingi.

Wewe unaijua ipi?

Twambie hizo tafsiri nyingi za akili ili tujue tunayo maanisha.
Mana Mshana yeye anajua tafsiri moja, ukitaja tafsiri tofauti na anayoielewa yeye atakueleza hapa na sisi pia tupo hapa.
Tafsiri ipi anayoijua?
 
This guy explicated it very well, the issue about we who don't follow the normal way of the world prominent religions. Not only scientists

read

Scientists believe that every occurrence, including the affairs of human beings, is due to the laws of nature. Therefore a scientist cannot be inclined to believe that the course of events can be influenced by prayer, that is, by a supernaturally manifested wish.

However, we must concede that our actual knowledge of these forces is imperfect, so that in the end the belief in the existence of a final, ultimate spirit rests on a kind of faith. Such belief remains widespread even with the current achievements in science.

But also, everyone who is seriously involved in the pursuit of science becomes convinced that some spirit is manifest in the laws of the universe, one that is vastly superior to that of man. In this way the pursuit of science leads to a religious feeling of a special sort, which is surely quite different from the religiosity of someone more naive.

With cordial greetings,

your A. Einstein
 
Back
Top Bottom