Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Joyce Kilia yupo wazi sana aliwahi kusema kabla hajawa na mpenzi wake wa sasa alishakuwa na wanaume(boyfreinds)12,nilishangaa sana kwani wanawake wengi huwa hawasemi background zao

Wengi wanasema " wewe ni wa pili ukiacha yule wa kwanza aliyeniumiza sana"
 
Ukishindwa kuangalia wanawake live angalia in my shoes kwa kipindi kikiisha unavunja Tv yako

kama cha tarehe mosi Januari, binti matiti nje. Wanaume wanamshikashika tu! Terrible
 
Alimaliza darasa la saba na yeye alishasema kuwa elimu si muhimu katika maisha (Bofya). Tulipinga sana wakati ule ingawa na sie ni FFF (Form Four Failure) lakini tunahusudu shule ni bahati mbaya. Tusitetee udhaifu wetu

Duh kumbe kuna chama kinaitwa FFF? Hebu kisajilini aisee, kina wanachama wengi sana.
 
huyu dada ni mbunifu bsana na ni lazima aungwe mkono hamuwezi kumlaumu wakati kazi anayoifanya ni kuwainua wanawake wawe live haijalishi anajua mambo ya gender issue au la anachojua yeye ni kwamba kuna mfume dume na unyanyasaji wa kijinsia ndani ya jamii yetu jambo ambalo ni kweli na ndio maana ameamua kulivalia njuga akaachana na mambo ya kuonyesha wasaanii wa bongo movie, huwez kumfananisha na kina lady j dee au wema ambao wanatuonyesha miili yao na vyombo vya nyumbani kwao.
keep it up sister joyce na kama utahitaji kujua mambo ya gender zaid c lazima uwe na degree ili uweze kuchambua mambo.
 
Elimu ya JOYCE KIRIA ni darasa la saba (7).
Historia inaonyesha kwamba aliwahi kuolewa kwanza na mume mwingine tena kwa ndoa kabla hajaolewa tena na kufunga tena ndoa na huyu HENRY KILEO.

Juzi nimemsikia eti ndio aliingia kanisani, kwani mume wa kwanza alikuwa Mujahidina?
 
Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.

Darasa la 7 Kiria, aliwahi kuwa Housegirl
 
Kiukwel mm c muumin wa hicho kipindi ila nmepata elim bt kwa michango nliyoisikia kipindi hiki kinatazamwa na watu wengi. Joyce anaweza kulekebisha mambo machache na kipindi kikawa bora afanyie kazi ushauri aliopewa. Tatzo langu lipo kwa mhuska je utafuata ushauri? Naomba mniambie ni lin kipindi kipo hewan na station ip ili nifuatilie plz.
 
Tatizo ni kwamba huyu mwanamke analeta ushabiki na matatizo yake binafsi katika kuendesha hiki kipindi hapo tu ndo anapoharibu mambo nadhani angeweza kutenganisha ushabiki na ushambenga wake na kufanya kipindi kwa kufuata misingi mizuri ni kipindi kizuri cha kuelimisha jamii sio anatumia hiki kipindi kama kicheni party ya kufunda wanawake jinsi ya kutowaheshimu na kuwasikiliza waume zao hapo ndo anaharibu mambo
 
Mnalalamika kwa kuwa wanaume ndio wanyanyasaji wakubwa na hamtaki mambo mnayowafanyia wake zenu yajulikane??
 
Elimu ya JOYCE KIRIA ni darasa la saba (7).
Historia inaonyesha kwamba aliwahi kuolewa kwanza na mume mwingine tena kwa ndoa kabla hajaolewa tena na kufunga tena ndoa na huyu HENRY KILEO.

Ni kweli kabisa Elimu yangu ni std7 na wala sioni aibu kamwe. Hata hivyo namshukuru sana Mungu kwa sababu amenitoa mbali sana na amenipa Kibali Kikubwa sana kwenye jamii yangu.

Ni kweli kabisa kwamba nimeolewa mara mbili sasa. Na sintaionea aibu Historia yangu bali namshukuru Mungu kwa yote.

Nitafunga Ndoa hata 1000 kwa sababu Sintaruhusu UKATILI WA KIJINSIA kwenye maisha yangu...

Naishi kwa ajili yangu, siishi kwa ajili ya walimwengu...

Mungu wangu ndiye atakaenihukumu....
 
usemacho ni kweli,joyce anakuwa hakimu tena na mamlaka ya kuarest,yule mzee hakumfanyia sawa na mara nyingi kwenye familia kuna mambo yako nje ya uwezo wa mtu mwingine kudadafua,kwa ufupi joyce iko siku utapigwa mawe kwenye benzi yako ya jana

Heri kupigwa mawe ukitetea Haki za Wanyonge kuliko kupigwa mawe kwa sababu ya kupora wananchi ardhi na kuwapiga risasi za moto..
 
Tatizo ni kwamba huyu
mwanamke analeta ushabiki na matatizo yake binafsi katika kuendesha hiki
kipindi hapo tu ndo anapoharibu mambo nadhani angeweza kutenganisha
ushabiki na ushambenga wake na kufanya kipindi kwa kufuata misingi
mizuri ni kipindi kizuri cha kuelimisha jamii sio anatumia hiki kipindi
kama kicheni party ya kufunda wanawake jinsi ya kutowaheshimu na
kuwasikiliza waume zao hapo ndo anaharibu mambo

mwanamke hafundishwi kutomheshimu mume wake ni jukumu lako mwanaume kumpenda na kumheshimu mkeo na yeye atakuheshimu, lakini kama unamkera humheshimu, kumpiga, nyumbani huonekani basi tegemea hiki kipindi cha dada joy na kitchen party lazima zitamfanya ayabebe hayo maushaur na kuyapeleka kwa ndoa yake na kuanza kutokukuheshimu wewe wala nduguzo! jiheshimu nawe utaheshimika!
 
Asikuumize kichwa kaka huyo ni kibaraka miongoni mwa vibaraka wa mataifa ya magharibi yaliyokusudia kumvuruga mwanamke kwa kumdanganya kuwa wanamtetea.
Kama wanamtetea mwanamke apate hadhi na heshima wanazungumzaje juu ya utitiri wa wanawake wanaojiuza,wanazungumzaje kuhusu wanenguaji wa miziki etc mbona hata siku moja hawaonekani kwa nguvu zote wakikemea wanaume wanaowafanya wanawake ni kitu dharili kwa kuwafanya wakae uchi mbele ya watu.

Katika Wanawake ninaowahurumia ni hao wanaojiuza. Kwa sasa bado natafakari jinsi ya kuwasaidia. Bahati mbaya sana Kuna WANAUME ambao wanawafanya hawa WANAWAKE waendelee na hiyo kazi huku vidole vikiwaelekea Wanawake kwa majina ya CHANGUDOA, KAHABA n.k

Naomba Mungu anipe maono jinsi ya kuwafikia...
 
Hakuna mlingano.. mwanaume ni mwanaume tu, kuheshimiana ndo jambo la msingi
 
Back
Top Bottom