Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,444
Joice analazimisha watu wote wasifanye sherehe za harusi eti ni anasa eti oooh watu wanacheza kwaito wanakunywa kama yeye hapendi asilazimishe na wengine wawe kama yeye!, alafu anakuwa mkali na kuwaona wanaofanya sherehe hizo ni wajinga yeye ndio mjanja zaidi! Pia anawafundisha wanawake wawe na kiburi kwa waume zao. Kweli inabidi abadirike
Hapana, halazimishi tatizo linarudi pale pale kuwa anashindwa kucheza na lugha na mazingira!! Watanzania wengi tuna lugha fulani ya kubembeleza zaidi (nimeshindwa kupata neno moja hapa) ila mfano mzuri ni kwamba Mtanzania akienda dukani kununua kitu badala ya kusema 'nipe' atasema 'naomba' as if anapewa bure!!! Nahisi utakuwa umenielewa mpaka hapo.
Back to the point, Joyce Kiria amegundua tatizo kubwa sana kwenye jamii yetu na tunapaswa kumuunga mkono kwa kila hali, watu wangapi wanaomba misaada kwenda kutibiwa kwa gharama za shilingi milioni moja tu lakini katika mtaa/jumuiya au ukoo huo huo wakati huo huo kuna mtu unakuta anafunga harusi yenye kugharimu milioni 30 tena kwa kuchangisha!! Kwa nini nafasi kubwa ya kuchangiwa asipewe huyu mgonjwa anayepigania uhai wake?? Ni hoja ya msingi sana isipokuwa lugha anayotumia Joyce Kiria kushawishi watu kuacha kutumia fedha nyingi kwenye sherehe na kutumia fedha nyingi kwenye matatizo ya kijamii ndiyo inayomfanya aeleweke vibaya kama wewe Yusuphsabury ulivyomuelewa.
Kama nilivyosema, Watanzania tuna lugha yetu ingawa kuna baadhi ya makabila wako tofauti kidogo kama Wachaga na Wakurya na ndiyo maana makabila haya watu wengi hudhani kuwa wanapenda sana ubabe ubabe lakini kumbe sivyo, wao hiyo ndiyo ongea yao ya kawaida kabisa!
Hivyo basi, kazi ya Joyce Kiria ingekuwa nyepesi sana kama angefuata matumizi ya lugha yetu ambayo ni ya kama kubembeleza hivi!!! Joyce ameathiriwa na lugha mama ambapo kwa watu wa pembeni ya mlima Kilimanjaro huwa hawana sana lugha ya kushawishi kwa kubembeleza (nahisi ni sababu ya kuwa karibu na Kenya).
Na hii ndiyo inayosababisha alaumiwe na wengi humu kwa kuongea na yule baba lugha fulani hivi ya ukali kuwa ambebe mkewe. Ile kwake anaona ni sawa kabisa, lakini hadhira yake inasemaje juu ya swala lile?? Hasa ukizingatia alikuwa anaongea na mtu mzima, si heshima kuongea nae maneno kama yale.
Kikubwa anachotakiwa kufanya ni kusoma mazingira ya anaowafikishia ujumbe yakoje? Atumie lugha gani kuwafanya watu wamuelewe hasa ukizingatia kuwa kipindi chake kinahusu sana maswala ya mahusiano.
Wengi watabisha lakini ukweli utabaki pale pale, presenter unaposhindwa kueleweka kwenye jamii husika ujue umefeli!! Kama unamwambia mwanaume ambebe mkewe ikiwa ni njia ya kurudisha upendo lakini ukawa umetumia lugha ambayo jamii imeelewa kuwa umemnyanyasa mwanaume ni wazi kuwa umefeli!!!
Ukifeli kutumia media kushawishi jamii, ni dhahiri kipindi chako kitafeli pia!! Marekebisho ni muhimu sana
cc:Ntakasi