Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Joyce Kilia yupo wazi sana aliwahi kusema kabla hajawa na mpenzi wake wa sasa alishakuwa na wanaume(boyfreinds)12,nilishangaa sana kwani wanawake wengi huwa hawasemi background zao
 
Anayefahamu elimu yake aniambie.

Ninaweza kumlaumu bure wakati elimu yake ni ndogo.
Alimaliza darasa la saba na yeye alishasema kuwa elimu si muhimu katika maisha (Bofya). Tulipinga sana wakati ule ingawa na sie ni FFF (Form Four Failure) lakini tunahusudu shule ni bahati mbaya. Tusitetee udhaifu wetu
 
Elimu ya JOYCE KIRIA ni darasa la saba (7).
Historia inaonyesha kwamba aliwahi kuolewa kwanza na mume mwingine tena kwa ndoa kabla hajaolewa tena na kufunga tena ndoa na huyu HENRY KILEO.

Sawa kabisa! Haya ni zamu yako kuolewa na Henry Kilewo ili uwe mke wa pili umsaidie Joyce kuendesha kipindi kwani una elimu ya kukidhi vigezo.
 
Tangu mume wake amwagie ndugu yangu Tindikali kule igunga hata kipindi hicho huwa siangalii.
Kwanza Joyce Kiria alifeli form four na akajaribu kusoma pale ustawi akaangukia pua.
Kwa ufupi ni kilaza.
 
Huwezi kumlinganisha ze supa woman Joyce Kiria na hao wauza sura wengine kama wema na mboni.

Kazi anayoifanya Joyce ni ya kupigiwa mfano na anastahili pongezi na kuungwa mkono.
 
Last edited by a moderator:
mimi kwakweli sijawahi kuangalia hicho kipindi kwa hiyo ngoja ni kae kimya ila kama ana tabia ya kuwafundisha kiburi wake zetu aache mara moja.
 
Kama no mshauri mzuri mtafute joyce mwenyewe kuanika elimu yake haitakusaidia,lakini ukweli tuseme amethubutu na mara nyingi amekuwa akiibua mambo mengi yaliyofichika,sifa zake lazima apewe jamani ,ni wanawake wangapi wanaojaribu,mwqnamke mwenzetu amejaribu naanapaswa kutiwa moyo,hayo mengine ni ya kumshauri tu,hakuna mtu anayepatia moja kwa moja
 
Mleta mada ana wivu wa kike!

Unashangaa pamoja na kwamba mwendesha kipindi Ana elimu ndogo ya darasa la saba na pamoja na history yake isiyovutia ya kupitia magumu,lakini ameweza kuwazidi nyie mlomaliza vyuo na masters na p.h.d zenu!

Acha wivu,UTAKUUA!

Inawezekana ikawa Sahihi usemavo lkn tuangalie pande zote mbili.nmemuelewa mtoa mada vzuri,ukitaka kujua asemalo ni kweli,linganusha Kipindi hicho na vipindi vyA dizaini hyo mfano njiapanda ya Dr Isack. Yule mtu hua anajtahidi sana kubalance story.hatoi story ama kumuhoji mtu km hajasikiza upande wa pili.km hua unamfatiliA utakubaliana name.mfn kuna Kipindi alihijiwa mm mmoja alikua anamshutumu mumewe kua anamlawiti na alikua anamnyanyasa hvo akawa anataka msaada wa jinsi ya mumewe kuleta matumizi ya watoto.bt alipohojiwa mume kibao kiligeuka kwake kwani ilionekana ye Ndo alikua anapga shoo za nje na kurudi home late na vitu km hvo case ilipofka kwa wazazi mm akijikimbza na watoto hvo mume akasema hatoi pesa ya matumizi arudishe watoto aone km hatawalea So mm akakimbilia Kwenye media na story za uongo..So kuna vitu Kwenye ndoa inakua ngumu kujudge upande mmoja
 
Mimi niliwahi kuendesha talk show enzi zangu, na kiukweli kati ya wanawake wote wanaoendesha talk show, huyu ni mmoja ambao namkubali sana ila ukweli unabaki ni ukweli ni lazima ajielimishe zaidi.
kaka Pasco wewe ndo yule mwandishi paschal mayalla? Yule anayependa kutembelea Boda boda yake? Yule alikuwa mwandishi baadae akasoma sheria pale Mlimani? Yule Swahiba wa Zitto? Yule wa Bonafide genuine?
 
Last edited by a moderator:
Awafundishe wanawake wenzie katika maadili ya mwanamama wa kiafrika ili maana yake iendelee kuwepo,yawezekana yeye kwake hapiki,hafui,hateki maji,hatandiki n.k ni sawa lakini ajue kama ni kwa Tz na Afrika yetu hii,asitumie mwanya huu eti kisa ana kipindi kuwalaghai akina mama/dada zetu yeye anavyofeel moyoni mwake na ajifunze kutokuonyesha upande wake katika taharifa anazozipata,awe partial,neutral na emotionless,aache watazamaji waamue na si yeye ndo maana anakuwa emotional mpaka anainsult wanaume,BAD!
 
Wewe unakuja na hizi shutuma ebu naomba tuangalie kati ya vipindi hivi ni kipi ambacho kimeweza kutoa msaada kwa jamii .......
........ Ukiangalia katika vipindi hivi ambavyo vinaongozwa na wanawake ukipima utaona kabisa hiki kipindi cha Wanawake Live kimejikita zaidi ndani ya yamii na hasa kumkomboa mwanamke kama kinavyojieleza kwani tumeweza kuona maeneo mbalimbali kama vile ndoa za utotoni, manyanyaso ya wanawake na hata manyanyaso ya watoto katika familia kwa hiyo kinatoa elimu tofauti na hivi vingene vya kuonyesha umaarufu tu na matumizi ya fedha ambazo hata hazijulikani wanazitoa wapi mwisho wa siku tutasikia na wao wamekamatwa na sembe huko China wanakoenda kila mara.

Wewe ni mdau nini mbona umekuwa mkali hivyo?

Jamani sidhani kama huyu dada aliyetoa maoni yake amekusudia vibaya, ila huyo Joyce achukuwe hizi kama ni changamoto na azifanyie kazi kuboresha kipindi.

Tuchukulie hizi criticisms zinazotolewa kwa mtazamo wa kuongeza maarifa (positive) na siyo dharau.
 
Pia hiki kipindi huwa hakifuati sheria na maadili ya habari!! Kuonesha sura ya mwanamke au
mtoto aliyenyanyasika kijinsia si sawa, kuna mama mmoja alibakwa alikuwa anahojiwa na Joyce bila hata kuficha sura, kuna yule aliyekatwa mkono na mumewe pia vivyo hivyo!! Lakini kubwa zaidi kuna siku alikuwa anakahoji katoto ka kike kamenyanyaswa kijinsia wazi wazi bila kumficha sura wala nini.

Sijajua kama yupo juu ya sheria au?? Na TCRA unawatumia taarifa wala hakuna action yoyote inayochukuliwa!! Ngoja tuone mwisho wake kama kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii kama anvyofikiria!!

Kijana Juzi
Sasa hapa wa kumlaumu ni Joyce Kiriya au TCRA?? Jamani tujifunze sana kuyapeleka malalamiko pale ipasapo. Wengine mnaanza kuuliza kiwango chake cha elimu nk hivi tujiulize je inahitaji digirii ya Masters ili kuwa Presenter kwenye TV?? Vitu vingine jamani tusiwe Biased hivyo.
Let us hope that anachokifanya kitawafanya wengine wabadilike haraka.
 
kaka Pasco wewe ndo yule mwandishi paschal mayalla? Yule anayependa kutembelea Boda boda yake? Yule alikuwa mwandishi baadae akasoma sheria pale Mlimani? Yule Swahiba wa Zitto? Yule wa Bonafide genuine?
Hapana, mimi ni Pasco wa jf!, ila yule yeye pia yumo humu jf kwa majina yake kamili na ni verified user!.
Happy New Year
Pasco
 
No wonder hii mada imeletwa na mwanamke, maana nimeskia adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake. Kwahiyo katika talk show zote ya Joyce ndio ina lugha kali??? Badala ya kumtia moyo mwanamke mwenzio, based on her past history na elimu yake anajitahidi sana. Wanawake acheni hizo!!!

Kipindi kile nilikiona na kwa ujumla yule mzee mhusika si dhani kama alikuwa sahihi. Isue ni jinsi Joyce alivyo mhandle yule baba kama ni sahihi. Ukweli alikuwa anamfokea yule baba nilikuwa na wasiwasi lolote lingeweza kutokea pale. Nilijiuliza nia kuu ya kipindi kile ilikuwa ipi? Kumsaidia yule mama au kuwafanya wakina baba wasiwe na muelekeo wa yule baba au yote mawili? Hapa sikupata jibu. Joyce naamini alishikwa na hasira jambo ambalo lilimpelekea kupoteza ushawishi wake.

Mleta maada ninahakika nia yake ni jinsi ya kuboresha uwasilishaji wa mada na kukifanya kipindi kiwe ni shule kwa pande zote. Naamini Joyce akiangalia kile kipindi na kama ni msikivu ataleta mabadiliko na kuwa mvumilivu zaidi hasa pale anapokutana na issue kama ya yule baba.
 
Uelewa wake mdogo,hafikirii kabla hajasema,kuna siku alikua anamlazmisha mzee mmoja ambebe mke wake,anatoa amri huyo mke apelekwe hospitali,anasema anasimamia haki za wanawake,nikajiuliza anasimamia km nan,hakim,polisi,mahakama au waziri wa haki za wanawake,kweli hajatambua malengo ya kpnd chake,analazmisha mambo badala ya kuelimisha,kichaa akipewa rungu n matatizo.
mimi kwakweli sijawahi kuangalia hicho kipindi kwa hiyo ngoja ni kae kimya ila kama ana tabia ya kuwafundisha kiburi wake zetu aache mara moja.
 
Back
Top Bottom