Ni kweli, aliwahi kutoa historia ya maisha yake, yeye ni Standard Seven leaver, alikuja mjini Dar kama "tx" namwanzo aliolewa na DJ!.
Nawaombeni sana nikiri wazi kuwa huyu dada anastahili pongezi, incouragement na kusaidiwa ili awe bora zaidi!. Kwa mtu wa darasa la saba kufika pale alipo, ni hatua na inahitaji hard work kujituma na kupambana!.
Katika kile kipindi chake cha ushuhuda ameeleza amejiendeleza kwa masomo ya jioni, na kwa sasa amepumzika kidogo ili kwanza kujenga familia, atataendelea mpaka kufika chuo kikuu na wale wahadhiri wanawake wa UDSM wamekubali kumsaidia kutimiza ndoto yake!.
Mimi niliwahi kuendesha talk show enzi zangu, na kiukweli kati ya wanawake wote wanaoendesha talk show, huyu ni mmoja ambao namkubali sana ila ukweli unabaki ni ukweli ni lazima ajielimishe zaidi.
Mpaka sasa tuna wanawake zaidi ya 20 bongo wanaoendesha vipindi vya talk show lakini vingi havina impact kama wanawake live!. Hawa ni baadhi yao.
- Joyce Kiria-Wanawake Live
- Salama Jabir-Mikasi
- Zamaradi Mketema-Bongo Movies
- Hoyce Temu-Tanzania yetu
- Sphora Mushi-Sphora Show
- Mboni Mhita-The Mboni Show
- Judith Wambura-Diary ya Lady JD
- Kanky Mwaigomole-Daladala Show
- Wema Sepetu- My shoes
- Christina Manongi-Sintah-Wedding Lounge
- Mayrose Kavura-The Mayrose Show
- Amabulis Batamula -Fema TV Talk Show
- Elizabeth Shirima-Mapishi
- Irene Uwoya-Paradise
- Shamim -Sherehe yetu
- Rose Ndauka-The Family Talk Show
- Kuna mmama mtu mzima anaendesha talk show fulani mpya TBC
- Kuna yule dada anaendesha kipindi cha wanawake ITV
- Kuna yule dada anaendesha kipindi cha EATV
- Kuna yule dada wa Star TV anaendsha talk show ya bongo beat
Happy New Year
Paskali