Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Shekizongoro

JF-Expert Member
Dec 9, 2013
388
195
Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Wewe unakuja na hoja hii kwa kutaka kuwaaminisha watu na uliyoyaandika, Mimi ni mmojawapo niliyeweza kuangalia siku ambayo Joyce Kirya ilibidi awe mkali kiasi kile kwani tukio lile lilikuwa ni la kuhudhunisha na kukasilisha sana kumbuka Yule Mwanaume alikuwa akimnyanyasa Mkewe na huyu Mke alikuwa ni Mstaafu na huku akiwa kisha chukua mafao yake na wameyatumia katika kujijenga kimaisha huku wakiwa na gari pia, Huyu mama alikuwa ni mgonjwa sana hajiwezi kabisa lakini mume wake hakuchukua hatua zozote za matibabu huku huyu mama mgonjwa akiwa na Bima ya Afya ambayo kama angepelekwa Hospitali matibabu yangekuwa Bure, Kilichotafsiriwa hapa ni kuwa huyu mume alikuwa amemtelekeza huyu Mke ili afe yeye aendelee na maisha kupitia kwa mali za huyu mama na ndipo JOYCE KIRYA ilipobidi awe mkali kwani huyu jamaa hakutaka kutoa ushirikiano wowote pale ilipotakiwa huyu mama apelekwe Hospitali.

Kwa hiyo usitake kupotosha watu tukio lile lilikuwa ni baya na la kusikitisha na kuudhi sana tufanye aliyekuwa akifanyiwa yale ni mama yako na aliyekuwa akifanya yale ni baba yako ungefanyeje?.
 
Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,572
2,000
Anyway kama kuna kizuri out of this post Joyce Kiwia yupo hapahapa jamvini atayachukua mazuri na kuyafanyia kazi
 
Last edited by a moderator:

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,280
2,000
Pia hiki kipindi huwa hakifuati sheria na maadili ya habari!! Kuonesha sura ya mwanamke au mtoto aliyenyanyasika kijinsia si sawa, kuna mama mmoja alibakwa alikuwa anahojiwa na Joyce bila hata kuficha sura, kuna yule aliyekatwa mkono na mumewe pia vivyo hivyo!! Lakini kubwa zaidi kuna siku alikuwa anakahoji katoto ka kike kamenyanyaswa kijinsia wazi wazi bila kumficha sura wala nini.

Sijajua kama yupo juu ya sheria au?? Na TCRA unawatumia taarifa wala hakuna action yoyote inayochukuliwa!! Ngoja tuone mwisho wake kama kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii kama anvyofikiria!!
 
kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,740
2,000
binti mwenyekuendesha kipindi elimu hana...wafikiri uwezo wake wa kupambanua mambo utakuwa mkubwa...? naamini hata malezi mazuri hajapata toka kwa wazazi wake....
 
Teacher1

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
331
250
Hongera Joyce Kilia kwa ubunifu wako na namna unavyoendesha kipindi endesha wewe maana ni wewe hao wanaojifanya ni wasomi watoe ushauri tu na upime ukifaa katika kipindi chako au au uache wakae nao. Katika nchi hii watu wengi wanataka mtu afanye kwa mtazamo wao hiyo haiwezekani maana tunatofautiana kimtizamo. Tanzania inao wasomi wengi wasio wabunifu kazi yao kufanya marekebisho na kungoja kutwa studio kuhojiwa, hebu tujiulize ni wasomi wangapi wenye PHD wanao endesha vipindi radioni au katika TV station nchini? Wengi ni kuhojiwa tuu na utaona wanavyochemka wakibanwa. Joyce asikubabaishe mtu songa mbele Wanawake wanahitaji ukombozi kupitia kwako.
 
chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,915
2,000
Haina haja ya kumshutumu Joyce kwa kipindi kama hiki,.

Kuna watu wengi wamefaidika kupitia kipindi hiki na hata kupata misaada ya kisheria na haki kupatikana hasa kwa wanawake,.

Ungejaribu kuainisha pia na yale mazuri yanayopatikana katika kipindi chake ungekuwa umefanya la maana,.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.

Wewe unakuja na hizi shutuma ebu naomba tuangalie kati ya vipindi hivi ni kipi ambacho kimeweza kutoa msaada kwa jamii
- Wema Sepetu in my shoes
- The Mboni Show
- Diary ya Lady Jay Dee
- Wanawake Live
- Nivana
- Wanawake Live

Ukiangalia katika vipindi hivi ambavyo vinaongozwa na wanawake ukipima utaona kabisa hiki kipindi cha Wanawake Live kimejikita zaidi ndani ya yamii na hasa kumkomboa mwanamke kama kinavyojieleza kwani tumeweza kuona maeneo mbalimbali kama vile ndoa za utotoni, manyanyaso ya wanawake na hata manyanyaso ya watoto katika familia kwa hiyo kinatoa elimu tofauti na hivi vingene vya kuonyesha umaarufu tu na matumizi ya fedha ambazo hata hazijulikani wanazitoa wapi mwisho wa siku tutasikia na wao wamekamatwa na sembe huko China wanakoenda kila mara.
 
McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
No hard feelings...!uyu dada hajui nn hasa anatetea anafanya vitu vyake ki-mtaani zaidi ni sawa na kuangalia uswazi ya Zembwela anatakiwa aongee na wanaojua kuhusu gender issues ki-undani ili arguments zake ziendane na mada husika kwa sasa kipindi ni km kijiwe cha wadada wa saloon naona km anaanzisha upinzani vile na wanaume baada ya kuelimisha.
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Believe me, huyo dada ni akili ndogo,ni nafasi tu katika maisha kama ilivyo kwa kina josephine mushumbuzi!!

Kwa hiyo wewe kwa hivi vipindi vinavyoonyesha Nyumba watu wakijirusha, wakila bata na kuonyesha vitanda wanavyo lala na huku chupi zikiwa zimeanikwa ndio vinaongozwa na akili Kubwa.
 
Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,797
2,000
binti mwenyekuendesha kipindi elimu hana...wafikiri uwezo wake wa kupambanua mambo utakuwa mkubwa...? naamini hata malezi mazuri hajapata toka kwa wazazi wake....

Hzi ni chuki binafsi..huna habari kwamba watu wanaweza jijendeleza ukubwani kama wewe ulivosoma QT? acha dharau na majigambo dogo
 
umla

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
1,166
1,250
Katika kubadili chanel za TV yangu kuna siku huwa najikuta nimeweka hiki kipindi kiukweli huyu dada anawafundisha vibaya sana wanawake hasa kutowatii waume zao yaan mumeo akikutuma amekunyanyasa huyu Dada ni janga sidhani kama kichwani kuna kitu.
 
Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,888
2,000
Elimu ya JOYCE KIRIA ni darasa la saba (7).
Historia inaonyesha kwamba aliwahi kuolewa kwanza na mume mwingine tena kwa ndoa kabla hajaolewa tena na kufunga tena ndoa na huyu HENRY KILEO.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom