Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Ni Mwandishi wa habari

Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.
 
yes! Kunakasoro zilizopo ktk kipindi hiki kama kuonyesha moja kwa moja picha za waathrka wa manyanyaso, lugha ambayo saa zngne inaonyesha kuibua ama kuendeleza chuki dhidi ya wanaume LAKINI tusisahau uzuri na maudhui hasa ya kpind hiki ambacho kwa kiwango kikubwa mama zetu, dada zetu, wadogo zetu, rafiki zetu wa kike wamepata nafasi ya walau kuelezea manyanyaso, mikandamizo, ubaguzi, dharau wanazozipata kutoka kwetu wanaume. Si lazima mwendesha kipindi ajue mambo yote ya sheria, saikoloji n.k ndio maana linapokuwepo swala linalohtaj uchambuzi wenye ujuzi ktk fani hyo wanakarbishwa.
 
Feminism is not necessarily being anti-men.

I can understand anti-chauvinism as part of feminism, but there are some men who are feminists and some women who are anti-feminism.

Wanawake na wanaume hawawezi kuwa sawa, ndiyo maana wakaitwa wanawake na wanaume, lakini tunaweza kuhakikisha mazingira ya usawa.

A true feminist will question even the idea of mwanamke kubebwa au kutongozwa as a natural/ default position, because it implies that the woman is passive.

Kwa hiyo hizo habari nzima za "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza" zinaondoa usawa kati ya wanawake na wanaume na kuashiria kwamba mwanamke mara zote ni mtu wa kubebwa na kutongozwa tu.

Unaweza kukuta mpigania haki za wanawake kajaa mfumodume na hata hajui.
 
Hata ukiwa na PHD kama huna msaada kwa jamii yako ni ujinga, kuwa na elimu ni jambo moja na namna una vyoitumia ni jambo lingine,kuna watu wanaelimu kubwa lakini mambo wanayoyafanya kwenye jamii hata mtoto wa miezi miwili ANASHANGAA, kwa hiyo wewe angalia nini unafanya kwa jamii yako, watu wangapi wamepata msaada kupitia wewe, angalia dada yangu watu wasikufanye uwe laana badala ya baraka. usivunjike moyo, kazana tena sana kukataa ukatili wa kijinsia
 
Tangu mume wake amwagie ndugu yangu Tindikali kule igunga hata kipindi hicho huwa siangalii.
Kwanza Joyce Kiria alifeli form four na akajaribu kusoma pale ustawi akaangukia pua.
Kwa ufupi ni kilaza.

Joyce kiriia kileo,nashukuru nawe ni member wa hapa jf.kipindi chako ni kizuri mno,mim ni mwanaume lakini nakifuatilia sana.hizi commenys mbaya zisikukatishe tamaa kabisa.go on...go... on go..on joyce.
Hivi tanzania kwa miaka mingi inawasomi wakubwa na nyadhifa kubwa.ni nin mchango wao kwa jamii yao?ebu rejea historia za gavana balali,liyumba,na masomi wengine waolingia mikataba ya rushwa wote ni wasomi na huo ni mchango wao kwa jamii yetu.
Hivi kuna member yeyote hapa jf aliyekupa idea ya kuanzisha hiyo program?
Namshukuru mtoa mada,amekusaidia kulekebisha kasoro za hapa na pale
 
Hata ukiwa na PHD kama huna msaada kwa jamii yako ni ujinga, kuwa na elimu ni jambo moja na namna una vyoitumia ni jambo lingine,kuna watu wanaelimu kubwa lakini mambo wanayoyafanya kwenye jamii hata mtoto wa miezi miwili ANASHANGAA, kwa hiyo wewe angalia nini unafanya kwa jamii yako, watu wangapi wamepata msaada kupitia wewe, angalia dada yangu watu wasikufanye uwe laana badala ya baraka. usivunjike moyo, kazana tena sana kukataa ukatili wa kijinsia

Very true 100%
 
Kiukwel mm c muumin wa hicho kipindi ila nmepata elim bt kwa michango nliyoisikia kipindi hiki kinatazamwa na watu wengi. Joyce anaweza kulekebisha mambo machache na kipindi kikawa bora afanyie kazi ushauri aliopewa. Tatzo langu lipo kwa mhuska je utafuata ushauri? Naomba mniambie ni lin kipindi kipo hewan na station ip ili nifuatilie plz.

Akili ya kuambiwa nitachanganya na yangu ya std7. Kipindi ni jnne saa tatu usiku Eatv, jtano saa nane mchana, jpili saa nane na nusu mchana. Karibu
 
Alimaliza darasa la saba na yeye alishasema kuwa elimu si muhimu katika maisha (Bofya). Tulipinga sana wakati ule ingawa na sie ni FFF (Form Four Failure) lakini tunahusudu shule ni bahati mbaya. Tusitetee udhaifu wetu
Kumbeee!!! Siku aliyoandaa maandamano akishirikiana na dada wa kazi akidai aonyeshwe alipo mmewe ndo nilianza kijiuliza maswali kidogo
 
Huyu dada n opportunist balaa....mabinti msimsikilize .... mkimfuata ndoa zitawashinda kama zinavyomshinda...ukiona mtu anajisifia kwa kuachika na kuolewa Jiulize malambili...am sory jaman nilisahau kua elim yake imeelemewa na atakacho kufanya...tumvumilie tu
 
Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.

Mleta uzi nakushukuru sana. Nitachanganya na za kwangu, nitafanya maboresho kwa ushauri nilioupata hapa. Huu ni mwaka wa Kibali Kikubwa sana kwangu na Taifa langu... kupata ushauri mwingi kutoka hapa Jf ndo Kibali namba 1.
 
all, asanteni sana. Mawazo yenu ni changamoto kwangu 2014. Mbarikiwe
 
Last edited by a moderator:
Huyu dada n opportunist balaa....mabinti msimsikilize .... mkimfuata ndoa zitawashinda kama zinavyomshinda...ukiona mtu anajisifia kwa kuachika na kuolewa Jiulize malambili...am sory jaman nilisahau kua elim yake imeelemewa na atakacho kufanya...tumvumilie tu

Mabinti wakusikilize wewe ili waendelee kuwa vilema na kufa kwenye Ndoa kwa sababu ya Unyama wa Wanaume!

Imekula kwako. Ukitili wa Kijinsia Hapana hata Ndoa 1000000000 haina kwere...

Mpaka utakapojua kumpenda mkeo na kuacha vitendo vya Unyanyasaji... fyuuuuuuu
 
Anajitahidi kwa kweli na anavutia wanawake wengi. Ila kama mtoa mada alivyoongea, anatakiwa kujirekebisha. Mfano kuna siku alishauri wanawake wawashtaki polisi waume zao wanaowaomba kinyume na maumbile. Mi nadhani angesema wawashirikishe viongozi wa dini na wazee kuliko alivyoshauri kwani baba akitoka polisi ndo hakuna ndoa hapo. Ataelewa tu kwani naye ni mwana JF mwenzetu.

Hakika wewe ni mmoja wao! Mangi Aloyce Temba huu mchezo umejifunza wapi? Umeshawahi kukaa Mombasa babangu? Sasa unaomba ya nini wakati unaogopa kufungwa? Yaani uhalifu uripotiwe kwa wazee ni si polisi! Kiiru!
 
Anayefahamu elimu yake aniambie.

Ninaweza kumlaumu bure wakati elimu yake ni ndogo.

Elimu yangu ni std7, nilikuwa Housegirl zamani.

Ni Historia ambayo siionei Haya hata kidogo.

Wasomi wengi wanalalamika pamoja na PHD zao. Tumia historia yangu Joyce Kiria kutafakari umeifanyia nini nchi yako.

Kama we ni msafi chukua Mawe unirushie...
 
Hakika wewe ni mmoja wao! Mangi Aloyce Temba huu mchezo umejifunza wapi? Umeshawahi kukaa Mombasa babangu? Sasa unaomba ya nini wakati unaogopa kufungwa? Yaani uhalifu uripotiwe kwa wazee ni si polisi! Kiiru!

Bwahahahahahahahahaha firahuni anajianika hapa kweupeee... arooo afande huyu tutam'buruza hapo sero aisee..
 
Mimi sikipendi na simshauri mke wangu aangalie kipindi hicho kwa sababu hakijengi ndoa wala kuimarisha bali hubomoa ndoa
 
Elimu ya JOYCE KIRIA ni darasa la saba (7).
Historia inaonyesha kwamba aliwahi kuolewa kwanza na mume mwingine tena kwa ndoa kabla hajaolewa tena na kufunga tena ndoa na huyu HENRY KILEO.
kumbe tatizo lake ni kuolewa na Henry Kilewo? nilikuwa sijui
 
Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.

Kakosa kitu kinaitwa "Kidaka Tonge" maneno huchujwa pale yeye cha kwake kinapitisha kila kitu.
 
Back
Top Bottom