Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Kipindi cha 'Wanawake Live' na madhara yake

Mleta mada ana wivu wa kike!

Unashangaa pamoja na kwamba mwendesha kipindi Ana elimu ndogo ya darasa la saba na pamoja na history yake iiyovutia ya kupitia magumu,lakini ameweza kuwazidi nyie mlomaliza vyuo na masters na p.h.d zenu!

Acha wivu,UTAKUUA!
Kweli mkuu
 
Wengine wanamponda joyce kwasababu mume wake henry kilewo ni kada wa chadema wanachofanya ni spring doctor, mfano kipindi cha wema sepetu kina mafunzo gani kwetu zaidi ya kutuharibia vijana haswa wanafunzi wetu kukata viuno.acha kutumika na kuzomoka na kuandika mihemko yako huku mbulula,na wasiwasi na elimu yako pia kama sio darasa la saba wewe
 
Mi sibishani na wewe tena,nimekwambia maudhui ya kipindi ni mazuri ila muendeshaji kipindi akitendei haki kwa sababu ya akili ndogo,and bear on your mind akili ndogo sio elimu ndo maana nimeweza kulinganisha udogo wake wa akili na bi mshumbuzi ambaye ana shule!!
Kwa heri ya kuonana!!!

Vipi unaenda kujinyonga? acha hasira Joyce Kiria atabaki kuwa Joyce Kiria na wewe utabaki kuwa hivyohivyo na elimu yako kubwa
 
Katika television zetu pamekuwa na utitiri wa uanzishwaji wa vipindi vyenye kuongozwa na watu binafsi Mfano Jenerali on Monday, This week in perspective, je tutafika, mimi na tanzania-Hoyce Temu, Diary ya Lady Jay Dee, Wema Sepetu in My Shoes, WANAWAKE LIVE-CHA JOYCE KIWIA Kileo na vingine.

Uanzishwaji wa vipindi hivi sijui unazingatia nini lakini kipindi cha wanawake live ni kipindi Muhimu hasa ambapo wanawake tunahitaji usawa na wanaume lakini SI kuwa sawa., ni kipindi sensitive kinachohitaji mwongozaji makini pengine mwenye uelewa wa hali ya juu ya Gender, Sociology, Sheria, Pschology n.k mi sijui Joyce Kiwia ana elimu gani maana hiki kipindi kitageuka janga siku sio nyingi. Anatumia maneno makali kwa wanaume mf Aliwahi kumwambia mzee mmoja "mbebe mkeo kama ulivyokuwa unamtongoza"! ha-balance story (kusikiliza pande mbili) yeye anahukumu tu.

Lakini anaongea na mambo ambayo yanaweza kusababisha chuki kwenye familia hasa ambazo hazina uwezo wa kuchambua mambo vizuri na ndoa zitavunjika na kusambaratika nyingi. Lakini baadae itaathiri hata siasa za Henry Kilewo negatively kama mambo hayatabadilika.

Wanawawake tunahitaji utetezi bila kuathiri ndoa zetu au kudhalilisha waume zetu.

naona wewe mwanamke uliandika haya unamuonea wivu mbona wanawake wenyewe hampendani kwa nini siku nyingine utaje mazur yake sio kuwa bias mbona mama makinda anaboronga kila siku hamsemi kama anadharirisha wanawake umekimbilia kwa joyce dada wa watu anajitahid kulingana na uozo wa nchi yetu
 
naona wewe mwanamke uliandika haya unamuonea wivu mbona wanawake wenyewe hampendani kwa nini siku nyingine utaje mazur yake sio kuwa bias mbona mama makinda anaboronga kila siku hamsemi kama anadharirisha wanawake umekimbilia kwa joyce dada wa watu anajitahid kulingana na uozo wa nchi yetu

Yaani acha tu...Wanawake Vs Wanawake........
Jamani,baada ya kumrekenisha kwa kumjenga,watu wanataka kumbomoa....oooh Elimu Yake,oooh Mume Wake....Inahuuuuuu.....?.
Wamuache Dada Joyce....Wamuacheeeeeee....
 
Elimu ya darasani peke yake wakati mwingine inaweza isimsaidie mtu, vipindi kama hivi vinaweza kuongozwa na watu wa elimu ya kawaida.
Ninampinga anayetaka kuhusisha elimu na ubora wa Joyce Kiria katika kuendesha kipindi, mkitaka kujua fuatilieni elimu ya GWIJI WA KIPINDI CHA AINA HIYO LARRY KING ALIYEKUWA NA KIPINDI CHA LARRY KING LIVE. FUATILIENI ELIMU YAKE MUONE, Jamaa hakuwa na elimu ila wasomi na magwiji walikuwa wanamgwaya na bila kuhojiwa naye haupewi nafasi ya kuukwa urais US.

Wasomi tuache dharau, kuna wengi tumewazidi elimu but wapo mbali sana ki mafanikio na hata status kuliko sisi!

Hilo nalo neno .....watakuelewa tuu
 
Wewe unakuja na hoja hii kwa kutaka kuwaaminisha watu nai uliyoyaandika, Mimi ni mmojawapo niliyeweza kuangalia siku ambayo Joyce Kirya ilibidi awe mkali kiasi kile kwani tukio lile lilikuwa ni la kuhudhunisha na kukasilisha sana kumbuka Yule Mwanaume alikuwa akimnyanyasa Mkewe na huyu Mke alikuwa ni Mstaafu na huku akiwa kisha chukua mafao yake na wameyatumia katika kujijenga kimaisha huku wakiwa na gari pia, Huyu mama alikuwa ni mgonjwa sana hajiwezi kabisa lakini mume wake hakuchukua hatua zozote za matibabu huku huyu mama mgonjwa akiwa na Bima ya Afya ambayo kama angepelekwa Hospitali matibabu yangekuwa Bure, Kilichotafsiriwa hapa ni kuwa huyu mume alikuwa amemtelekeza huyu Mke ili afe yeye aendelee na maisha kupitia kwa mali za huyu mama na ndipo JOYCE KIRYA ilipobidi awe mkali kwani huyu jamaa hakutaka kutoa ushirikiano wowote pale ilipotakiwa huyu mama apelekwe Hospitali.

Kwa hiyo usitake kupotosha watu tukio lile lilikuwa ni baya na la kusikitisha na kuudhi sana tufanye aliyekuwa akifanyiwa yale ni mama yako na aliyekuwa akifanya yale ni baba yako ungefanyeje?.

Sasa hivi hilo tukio limetoka kurushwa hewani nimeona hakika yule baba ni mnyama tena afai kwenye jamii
 
...,Kiukweli nyie mnaomkingia kifua huyo Joyce Kiria ndo mnaozidi kumvimbisha kichwa na hatimae kumpotosha kabisaa.., Maudhui ya kipind ni mazuri ila huyo Joyce ndo amekosa Maadili ya kuendesha hcho kpndi na itakua imechangiwa na malezi ktk makuzi aliyopitia.., na kibaya zaidi ni kupenda kuhukumu mambo kutokana na past experience yake ktk ndoa au maisha alopitia ambacho si kitu kizuri! Ushauri; ajfanyie tathmin kutokana na maoni ya wadau then anachukue hatua!!
 
Mkuu wewe unatafsiri elimu ni kitu gani? kuoanisha nadharia na vitendo au uhalisia ndio elimu yenyewe na si accumulation of certificates. Kugundua tu kwamba huyu dada anaharibu sociopsychological state ya jamii nayo ni elimu tosha kwa kuanzia kwani usipojua tatizo huwezi kulitatua.
Elimu ya darasani peke yake wakati mwingine inaweza isimsaidie mtu, vipindi kama hivi vinaweza kuongozwa na watu wa elimu ya kawaida.
Ninampinga anayetaka kuhusisha elimu na ubora wa Joyce Kiria katika kuendesha kipindi, mkitaka kujua fuatilieni elimu ya GWIJI WA KIPINDI CHA AINA HIYO LARRY KING ALIYEKUWA NA KIPINDI CHA LARRY KING LIVE. FUATILIENI ELIMU YAKE MUONE, Jamaa hakuwa na elimu ila wasomi na magwiji walikuwa wanamgwaya na bila kuhojiwa naye haupewi nafasi ya kuukwa urais US.

Wasomi tuache dharau, kuna wengi tumewazidi elimu but wapo mbali sana ki mafanikio na hata status kuliko sisi!
 
Kunaweza kukawa na uhusiano katika maisha aliyopitia Joyce mwenyewe na kipindi hiki,namaanisha social background na mtizamo wake ama jinsi ya anavowafundisha wanawake wenzake wawe

Mfano aliwahi achwa ila hatujuhi sababu ni ipi?, amelelewa katika mfumo wa baba ndo kichwa ama mama ndo kichwa? i.e(patrilineal ama matrilineal family) ...ila tumshauri pia, kuna haki za wanawake kama mwanadamu alafu kuna wanawake kutaka kuwapindua wanaume,sijuhi objectives zake ni nini hasa ila the latter seems her trend.
 
Ndugu zangu taasisi muhimu kuliko zoote ni ndoa, ndoa ndiyo chanzo cha familia. Familia bora huzaa taifa bora, ndoyo maana nimezungumzia kipindi cha Wanawake Live, na hivyo vingine vina matatizo yake. Na nimeaknowledge kwamba kipindi ni kizuri; lakini uendeshaji wake unafanya kilete madhara katika taasisi hii muhimu. Sina wivu na Joyce hata kidogo na elimu yangu sio kubwa kama mnavyosema wengine. Ni muhimu kuanticipate the side effect of the programme. Ahsanteni wakuu.
 
Kweli kabisa, huyo Joyce Kiria, not Kiwia or Kirya? Ni janga, nadhani hajui hata matumizi ya maneno, nadhani Elimu yake pia ni tatizo ndio maana anashindwa kuchambua mambo kwa uweledi na lugha ya staha. Na si yeye tu Kuna jamaa anaendesha Kipindi Radio EATV anaitwa Zembwea, duuuh, janga hajui hata mfumo wa serikali ukoje, hajui hata wapi watu wanapata haki zao..... Joyce Kiria alikuwa mchambuzi wa Bongo Movie kule Clouds FM kabla ya kuja wanawake LIVE, nadhani hayo mazingira ya Clouds na Kipindi alichokuwa anaongoza kule ndio kimemfanya ashindwe kufikir vyema na kujua lugha (muktadha) sahihi kwa wakati.

Elimu: Nina uhakika ni drs la saba, labda kama amejiendeleza sasa hivi, na alikuwa anauza duka la nguo KARIAKOO kwa Anaitwa Moria, analifukuzwa baada ya kutuhuma za kuwa mwingi wa habari kwenye eneo la kazi.

ALIWAHI KUOLEWA NA DJ maarafu ndani ya Clouds FM anaitrwa Muli Bling cjui nn, wanajua majina yao wenyewe! Unaweza kukonect dots..uwezo wake katika Wanawake Live na maisha yake ya nyuma...
Aliolewa na Dj Nelly then wakaachana
 
Elimu ya JOYCE KIRIA ni darasa la saba (7).
Historia inaonyesha kwamba aliwahi kuolewa kwanza na mume mwingine tena kwa ndoa kabla hajaolewa tena na kufunga tena ndoa na huyu HENRY KILEO.
Ni kweli, aliwahi kutoa historia ya maisha yake, yeye ni Standard Seven leaver, alikuja mjini Dar kama "tx" namwanzo aliolewa na DJ!.

Nawaombeni sana nikiri wazi kuwa huyu dada anastahili pongezi, incouragement na kusaidiwa ili awe bora zaidi!. Kwa mtu wa darasa la saba kufika pale alipo, ni hatua na inahitaji hard work kujituma na kupambana!.

Katika kile kipindi chake cha ushuhuda ameeleza amejiendeleza kwa masomo ya jioni, na kwa sasa amepumzika kidogo ili kwanza kujenga familia, atataendelea mpaka kufika chuo kikuu na wale wahadhiri wanawake wa UDSM wamekubali kumsaidia kutimiza ndoto yake!.

Mimi niliwahi kuendesha talk show enzi zangu, na kiukweli kati ya wanawake wote wanaoendesha talk show, huyu ni mmoja ambao namkubali sana ila ukweli unabaki ni ukweli ni lazima ajielimishe zaidi.

Mpaka sasa tuna wanawake zaidi ya 20 bongo wanaoendesha vipindi vya talk show lakini vingi havina impact kama wanawake live!. Hawa ni baadhi yao.
  1. Joyce Kiria-Wanawake Live
  2. Salama Jabir-Mikasi
  3. Zamaradi Mketema-Bongo Movies
  4. Hoyce Temu-Tanzania yetu
  5. Sphora Mushi-Sphora Show
  6. Mboni Mhita-The Mboni Show
  7. Judith Wambura-Diary ya Lady JD
  8. Kanky Mwaigomole-Daladala Show
  9. Wema Sepetu- My shoes
  10. Christina Manongi-Sintah-Wedding Lounge
  11. Mayrose Kavura-The Mayrose Show
  12. Amabulis Batamula -Fema TV Talk Show
  13. Elizabeth Shirima-Mapishi
  14. Irene Uwoya-Paradise
  15. Shamim -Sherehe yetu
  16. Rose Ndauka-The Family Talk Show
  17. Kuna mmama mtu mzima anaendesha talk show fulani mpya TBC
  18. Kuna yule dada anaendesha kipindi cha wanawake ITV
  19. Kuna yule dada anaendesha kipindi cha EATV
  20. Kuna yule dada wa Star TV anaendsha talk show ya bongo beat
Happy New Year
Paskali
 
Joice analazimisha watu wote wasifanye sherehe za harusi eti ni anasa eti oooh watu wacheza kwaito wanakunywa kama yeye hapendi asilazimishe na wengine wawe kama yeye!, alafu anakuwa mkali na kuwaona wanaofanya sherehe hizo ni wajinga yeye ndio mjanja zaidi! Pia anawafundisha wanawake wawe na kiburi kwa waume zao. Kweli inabidi abadirike
 
Yote uliyosema yanaweza kuwa sahihi,je kama hana elimu na hajapata malezi mazuri haya ni makosa yake?Unamsaidiaje wewe uliyepata elimu ili awe na uwezo wa kupambanua mambo na kipindi kiwe bora?au unashauri kisiwepo na yeye aishi kinyonge tu kwa vile hana elimu?au asijaribu kufanya kitu kizuri kwa vile hakupata malezi mazuri toka kwa wazazi?je ukimshauri akualike wewe uliyepata elimu ili umsaidie kuweka mambo vizuri unadhani atakataa?Heri ya mwaka mpya 2014!


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Huwezi kuachwa unaharibu jamii eti kwa sababu unasubiri ushauriwe ili uyafanyie kazi uwe bora. JK aliongea hili la makanjanja mwaka ule alipokuwa anazindua TBC nashangaa TCRA hawajamdaka mpaka sasa!
 
Nilijua tu kuwa iko siku litatokea hili. Mimi ni mwalimu wa Elimu maalumu(ya wanafunzi wenye mahitaji maalum) kuna kanuni inasema hivi "chukua lililozuri/jema toka kwa mwanafunzi wako ili umwendeleze/kuchochea kipaji alichonacho. Pia ni rahisi hata kumrekebisha kasoro zilizopo.
 
Joice analazimisha watu wote wasifanye sherehe za harusi eti ni anasa eti oooh watu wanacheza kwaito wanakunywa kama yeye hapendi asilazimishe na wengine wawe kama yeye!, alafu anakuwa mkali na kuwaona wanaofanya sherehe hizo ni wajinga yeye ndio mjanja zaidi! Pia anawafundisha wanawake wawe na kiburi kwa waume zao. Kweli inabidi abadirike
 
Back
Top Bottom