Kipindi cha uchaguzi wa kisiasa, tasnia ya habari pamoja na waandishi wa habari mara zote nao wanajumuishwa kama vyama vya upinzani

sopinta

Member
May 28, 2020
46
93
Historia ya ndani ya nchi ya Tanzania katika kipindi cha uchaguzi wa kisiasa, tasnia ya Habari pamoja na waandishi wa habari mara zote nao wanajumuhishwa kama vyama vya upinzani hususani vyombo binafsi vya habari, waaandishi wanaojitegemea pia huwa katika wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yao.

Mikasa ya kupigwa na polisi, vyombo kufungiwa, vitisho kwa vyombo hivyo kutoka mamlaka za kiserikali kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, mpaka kitaifa.

Na ndio kipindi hiki ambapo sheria, kanuni, na taratibu za kuwabana waandishi na kuibana sekta ya habari zinaibuliwa sana, niseme tu Tanzania hakuna Uhuru wa Habari ila kuna waandishi na vyombo vya habari ambavyo vinafanya kazi bora siku iende lakini sio makosa yao.
 
Hata wakibana tv, radio na magazeti, kwa teknolojia hii mkuu watatuweza? binafsi siagalii tv, radio sisikilizi wala kusoma magazeti yalishapitwa na wakati. Na deal na mitandao ya kijamii over.
 
Hongera umenena vilivyo. Tatizo kubwa lililopo ni kuwa tuliingia kwenye democrasia bila kutengeneza katiba mpya.

Hili la watu kunyanyaswa limeonekana sana awamu hii kwasababu tunaongozwa na mtu mbaguzi, mkabila na mwenye visasi. Yeye baada ya kupewa uongozi (hakushinda) aliamua kufanya bila kufuata sheria.
 
Hata wakibana tv, radio na magazeti, kwa teknolojia hii mkuu watatuweza? binafsi siagalii tv, radio sisikilizi wala kusoma magazeti yalishapitwa na wakati. Na deal na mitandao ya kijamii over.
Redio na tv ndiyo tegemeo kubwa na watu wa vijijini kupata habari. Hofu yangu ccm watapata kura nyingi vijijini
 
Back
Top Bottom