Kuna Mambo Katika Historia ya Mapinduzi Wazanzibari Wangependa Kusahau

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,263
MAPINDUZI YA ZANZIBAR: KUNA MAMBO WAZANZIBARI WANGEPENDA KUYASAHAU

Jana nimeandika hapa kuwa katika mahojiano ndani ya kipindi cha mapinduzi na Azam TV nilijizuia kueleza historia ya yale yaliyotokea Zanzibar baada ya kutokea mapinduzi.

Nisingeweza kueleza historia ya jela za mateso zilizoanzishwa Zanzibar mara baada ya mapinduzi.

Wala simlaumu aliyeniuliza maswali kutaka kujua nini kilikuja na mapinduzi yale.

Allah ana njia zake za ajabu za kutufunza.

Sikutegemea hata siku moja wala hili halikupita katika fikra zangu hata kwa mbali sana kama iko siku nitakutana na mmoja katika watesaji aliyetesa watu wengi Zanzibar uso kwa macho na kufanya mazungumzo na yeye kuhusu maisha yake haya.

Soma kisa changu hiki nilichoandika miaka minne iliyopita:

"FOOL' S PARADISE" ... PEPO YA WATU WAJINGA

"Fool's paradise," starehe bila kufikiri hatari iliyoko mbele.

Si watu wengi wanaweza kujifunza katika historia.

Nimekaa barazani kwenye mkeka uliokuwa hoi kwa kuchakaa.

Mwenyeji wangu ni mzee wa Kizanzibari na muonekano wake ulikuwa wa mtu anaeteswa na maradhi na ufukara.

Kufika hapo kwake ilikuwa kazi kubwa lakini alinipa majina ya sehemu za kuuliza ambazo ndizo zilinifikisha nyumbani kwake.

Sijui kwa nini lakini sikumpenda jicho langu lilipotua kwake.

Sikusikia raha hata kidogo jinsi alivyokuwa akiniangalia na macho yake madogo yaliyobonyea kwa ndani.

Alikuwa akiniangalia kuanzia chini kuja juu kama vile ananipima kimo changu.

Mtu aliyenikutanishanae ni ndugu yake na nashukuru kuwa alinipa taarifa za huyu bwana kabla.

Huyu bwana alikuwa baada ya mapinduzi mmoja wa askari usalama na mtesaji wafungwa.

Sheikh Mohamed, "Nimesikia sifa zako nimeambiwa wewe ni mwandishi hodari sasa mimi nataka nikueleze maisha yangu baada ya mapinduzi hadi kufikia kuuawa Mzee Karume mwaka wa 1972."

Mwanafunzi wa Gestapo na SS mkimbizi huyu kakimbia Zanzibar kwa ule ubaya wake kaja kujificha huku Bara "sweken," huku shamba porini kabisa mbali na macho ya watu wanaoweza kumtambua.

"Mimi mgonjwa naumwa sana lakini nataka kueleza niliyoshuhudia kwa macho yangu mwenyewe Zanzibar.

Yule sahib yako nilipomweleza hii azma yangu ndiyo akaniambia ataniletea mtu wa kufanya kazi hii."

Pale tulipokaa tuko nje pana upepo lakini vest yake imelowa jasho lakini joto lile nilishangaa lilikuwa linamuadhibu yeye peke yake.

Nikawa najisemea kimoyomoyo, "Huenda moto wa jahanamu umemfuata huyu bwana hapa hapa duniani huku porini juu ya kujificha kwake."

Namwangalia msuli haukai kiunoni kila saa unamshuka kutaka kumweka uchi na yeye hachoki kuupandisha juu ya kitovu chake kwa mikono yake miembamba iliyobakia mfupa na ngozi.

Najihisi kama "charachter" katika "scene," moja ya senema ya Steven Spielberg bingwa wa kutengeneza filamu zinazohusu mateso waliyopata Wayahudi katika mikono ya Manazi wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia.

Akaanza kuzungumza...

Aliyonieleza ya mauaji ya kundi moja la watu walioshutumia kutaka kupindua serikali ya Karume nilikuwa nimeyasikia kabla kutoka chanzo cha kuaminika.

Maelezo ya huyu mtesaji muuaji hayakupisha hata kwa tone na yale aliyonieleza mpashaji wangu.

Nimetulia tuli namsikiliza.
Kisa ni cha kutisha na kusikitisha.

Nikamwambia kwa siku ile yanatosha apumzike kwani kwa hakika alikuwa amechoka.

Sijui kipi kilikuwa kinamwelemea, ni kule kukumbuka unyama waliowafanyia ndugu zao au maradhi aliyokuwanayo.

Si yeye peke yake aliyekuwa amechoka.
Nami pia nilikuwa nimechoka.

Nilitamani kumwambia tupige Fatha tuombe dua kabla ya kuagana lakini kuna kitu kilikuwa kinanizuia.

Narudi kwangu katika mengi aliyonieleza kuna maneno yalikuwa yakijirudia kichwani kwangu.

Aliniambia, "Wakati ule mimi nafanya haya sikujua kama iko siku itafika nitakuwa kama hivi, mgonjwa, peke yangu na yote yale yatarejea kunihangaisha."

Nilimsikitikia sana kwani katika yote tuliyozungumza jina la Allah halikutokeza hata mara moja.

Tuliagana na kuweka miadi ya kukutana siku nyingine.

Miaka 56 ilikuwa imepita toka mapinduzi yatokee na baada ya miaka hii yote kaamua aseme labda huku kusema kutamwondolea kifuani kwake joto kali la mzigo wa damu na roho za wale waliopita mikononi mwake.

Tulikuwa tumeshaanza kuandika sura ya kwanza ya kitabu cha maisha yake.

Historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa hakika imejaa dhulma na damu nyingi.

Ukiyajua haya yanakufanya uwe mwangalifu pale unapoizungumza historia ya mapinduzi.
 
Chamsingi sultan na genge lake walifurumushwa visiwahi,hakuna mapinduzi yasiyoacha vilio na huzuni,lengo kuu la uhuru na kujitawala lilipatikana.
 
Mkuu kwa nin usitusimulie kwa undani kama yeye alivopata kukusimulia!!??

Tunahitaji kufahamu kiundani zaidi kuhusu haya mapinduzi ya zanzibar.

Mana kuhusu uhuru wa tanganyika na harakati zake umezieleza kiundani sana humu jf, fanya hivo pia katika upande wa the so called "mapinduzi ya zanzibar".
 
Chamsingi sultan na genge lake walifurumushwa visiwahi,hakuna mapinduzi yasiyoacha vilio na huzuni,lengo kuu la uhuru na kujitawala lilipatikana.
Bado sultan ana magenge huko Zanzibar kuna Mashina yake bado
 
Wakati tunazungumzia mapinduzi ya 1964 wangapi wanamjua mtesaji mkuu pale gerezani akijulikana kama BAMKWE?
Wangapi wanaelewa jinsi viongozi wa ASP kama Abdulla Kassim Hanga na Mdungi Usi na Othman Shariff walivyouliwa na serikali ya mapinduzi?
Hii ndio historia ya mapinduzi ambayo imefichwa
 
Mapinduzi yeyote lazima yawe na gharama zake, hamna Cha ajabu sana ili pawe na mafanikio lazima damu na jasho vihusike
 
Mpaji...
Inataka ujue nini khasa kilitokea Zanzibar baada ya mapinduzi kuelewa kwa nini inasemwa yale mauaji siku ya mapinduzi na baada ya mapinduzi hayakuwa na sababu yoyote.

Watu wengi hapa hupenda kujadili somo ambalo hawalijui na hawa huseme chochote na lolote liwajialo akilini.

Historia ya Zanzibar inatisha.

Ukipenda kujua yale yaliyotokea unaweza kuanza na kumsikiliza Aman Thani katika series zake ambazo zipo katika YouTube zilizorekodiwa na Prof. Ibrahim Noor Shariff: ''za Aman Thani Akielezea Aichokiona na Yaliyomfika.''

Tuanze hapa.

1705379577009.png
 
Back
Top Bottom