Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
Habari zenu wana JF wenzangu,
Kuna pindi niliangalia kimenipa inspiration,kuna jamii ya watu fulani ambao kipigo kwao ni PRIDE,yaani mwanamke anafurahia kupigwa/kuchapwa mpaka atoke damu na halii anafurahia.
Kulia kwao ni mwiko,mtu analia akifiwa tu..ni ushujaa na ushupavu mkubwa kwa watu hao.Hata kwenye vitabu vya dini vinasema mwanamke anatakiwa amtii mumewe.
Kwa kufikiria harakaharaka kipigo kinatumika kama njia ya kufundisha au kukosoa na kikumbusho kwamba mtu hakuwa muadilifu na amevunja au kukiuka sheria fulani.Tangia enzi za ukoloni ilikuwa ni kawaida sana haswa kwa watumwa kupigwa na kuadhibiwa iwapo kama hawatekelezi amri walizopewa na ndio maana ukaitwa UTUMWA.Kipigo kilikuwepo hata nchi za magharibi miaka ya 60-70 mpaka haki za binaadamu zilipopatikana ndipo zikawekwa sheria kali kupinga KIPIGO

- Tuje kwenye mada kuu sasa,Kuna kupigwa kwa aina nyingi,kuna kile kipigo cha watoto/wanafunzi kama njia ya kuwafundisha maadili mema,na kipigo hiki kinaweza kuwa na faida na hasara zake.Kuna walio wengi walishakiri wenyewe kwamba walikuwa watukutu mno na kama wasingewekwa sawa na wazazi wao wasingefika walipofika leo. Je hii ni dhana tu waliojiwekea watu kichwani kwamba kipigo kimewanyoosha?Na tukumbuke pia kuna waliopigwa mno mpaka wamekuwa sugu kwasababu wanajua nikifanya hivi nitapigwa halafu basi.Kwa mtazamo wangu mm kipigo hakifundishi bali kina jenga uoga.Nimegundua kitu kimoja muhimu sana kwenye jamii yetu kwamba watoto na wazazi hawana mawasiliano mazuri.Mfano baadala ya kumuonya mtoto na kumueleza madhara ya aliyoyafanya na kwanini asifanye alivofanya,tunapiga hapo tunakuwa hatujengi bali tunabomoa.Wazazi wengi pia wanasahau kuna umri fulani ukifika lazima mtoto atapitia vikwazo tofauti kwahio yeye kama mzazi anatakiwa amuongoze kwa hekima na sio kwa kumjengea uoga,anatakiwa awe mfano mwema.
- Kuna wale ambao hata akigombana na mwenza wake hasira anamaliziwa mtoto,Kila aliye wa juu anamuadhibu wa chini yake yule alomzidi.
- Kuna kupigwa kwa mke na mumewe!Hapa ndipo nisipopaelewa,hiki kweli utamkunguta mtu mzima mwenzio mwenye meno 32 kisa amekukera,kwani ukiongea nae ujumbe hautofika.Kwa mtazamo wangu mimi maneno yanauma kuliko kitu kingine,Kuna maneno mtu ukiambiwa unaumia unaweza hata ulie na ujutie matendo yako.
- Hivi kipigo kweli kinajenga kama wanavyofikiria wengi?Kuna wezi wanaoiba wakapigwa mpaka karibia kifo,lakini wanaenda kuiba tena!Unadhani kipigo kimemfundisha kitu?Mwanafunzi mtukutu,ambaye anapigwa na hatii anayoamrishwa,je kipigo kimemsaidia?