Tutu kalundji
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 531
- 1,285
Nakumbushia tu siyo kwa ubaya.Niliwahi kutoa maandiko zaidi ya manne nikionyesha jinsi biashara ya uuzaji dhahabu feki ilivyoathiri maendeleo ya wanafunzi mashuleni na kujikuta wamelowea kwenye biashara hiyo na kuacha masomo.Matokeo yake wengi wamepata vilema kwa vipigo,na baadhi kupoteza MAISHA.
Kulwa Gidion Nyachiliga almaarufu Kulwa kadisi (18)alitakiwa kuwa mhitimu wa kidato cha nne mwaka Jana,2025 ila mpaka naandika andiko hili yupo kaburini takribani wiki tatu zilizopita baada ya kipigo cha wananchi katika mnada wa kiabakari,butiama alipokuwa akijaribu kutapeli wafanyabiashara kwa kuwauzia dhahabu feki.Mwenzake Maganya Machanchu(17)alifanikiwa kutoroka na mpaka dakika hii yupo mkoani Tabora wakiendelea kutapeli watu mbali kwenye minada na magulio ya huko.
Wakati jamii ikiendelea kuhudhunika kumpoteza kijana mdogo kiasi hicho,Jana mtoto mdogo aliyekatisha masomo mwaka Jana katika shule ya Sekondari Rubana,Sikonde Msafiri(15) kafariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali moja iliyopo Musoma.Sikonge,alifikishwa hospitalini hapo akiwa mahtuti baada ya kupigwa akiwa na wenzake walipokuwa wakijaribu kurubuni wafanyabiashara ili wawauzie dhahabu feki katika mnada wa Mtana uliopo Tarime,mkoani Mara.
Mlolongo ni mrefu na idadi ya watoto wanaokatisha masomo na kujiunga na biashara hii haramu inaongezeka kila kukicha.Maeneo ya mtaa wa Nyerere na hasa uswahilini zaidi ya 95%ya vijana wanafanya biashara hii haramu ambapo mbali ya kuchukua pesa kwa anayetapeliwa Kuna nyakati huchukua vifaa vingine mfano simu ambapo hizi huwa wanapeleka kwa Jamaa mmoja ambaye anakula na baadhi ya walinzi wa usalama ndio maana pamoja na kujulikana hii ndio kazi yake kuu Bado hagusiki(Polisi Toka makao makuu fuatilieni hili,mjiridhishe)Simu zote na kompyuta mpakato zinazoibiwa hupelekewa huyu jamaa ambaye naye huzifanyia utaratibu wa biashara Kisha anagawana na baadhi ya wanausalama(Waziri wa mambo ya ndani fuatilia hili kinagaubaga tumia tu intelijensia yako utalibaini).Huyu Jamaa hagusiki.Yaani hata wanawake wakiporwa tu simu zao,kituo cha kwanza ni kwa huyu Mr.Untouchable!Kibaka akipora tu simu Jamaa anapelekewa!
Nani wa kulaumiwa hapa kuhusu mvuto wa biashara ya dhahabu feki kwa watoto?
Binafsi lawama zote nazitupa kwa walezi na wazazi wa hawa vijana maana kwa macho ya kawaida tu wamebariki kabisa hii michezo kwa kufurahia pesa za short cut!
Ushauri wangu kwa kifupi;
Serikali kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama itumie maaskari waaminifu kukamata vinara wote wa biashara hii,Nitawataja hapa chini
1.Kolo
2.Maganya Machanchu(mkazi wa uswahilini,alikamatwa hivi karibuni akachomoka kwa namba anavyojua mwenyewe)
3.Gega .(Mkazi wa eneo la jarufu)
4.Baraka wasiler( Huyu kaanza hii kazi zaidi ya miaka 15 iliyopita,mkazi wa nyamakokoto siku hizi ana bodaboda ya kupotezea maboya)
4.Mundu huyu ni kama familia yao Ina DNA ya uhalifu maana baba yake mzazi maarufu kwa jina la kaliagogo aliuawa na wananchi wenye hasira Kali akiwa kwenye shughuli zake za wizi maeneo ya Nyasura.
B:Nitaendelea kutoa orodha ya wahusika kadri muda utakavyoruhusu
Ukiwapata hawa unaikamata chain nzima.Tukipuuzia hili tunaenda kuongeza idadi ya wahalifu under-age karibu Kila kona ya bunda.Wahalifu hawa wanapoona mtu anawafuatilia nyiendo zao na kuwadhibiti wamebuni mbinu ya kusingizia kwamba washamuuzia vitu vyao vingi na kwa kuwa akili za baadhi ya Polisi ndio hivyo tena mtu mwema hujikuta anasumbuliwa na wahalifu kutamba kwamba yeyote atakayewaingilia 'watakufa nae sambamba'Mbinu hii imesababisha watu wema kuwaogopa sana hawa wahalifu.
Polisi fanyeni kazi yenu sasa nishawapa pa kuanzia!Bila kudhibiti hawa watu watoto wengi wataendelea kurubuniwa na kuacha shule kwa kigezo cha utajiri
Rip kwa marehemu wote
Ila kwa wahusika niliowataja hapo naweza kutoa namba zao inbox kwa Afisa yoyote wa Polisi Toka makao makuu,siyo hawa ninaowajua ambao mara kwa mara hupishana kufuata posho za ten ten kwa wahalifu
Pongezi kwa diwani wa kata ya Bunda mjini Mr.Obwete kupambana na matukio ya uhalifu,tatizo tu wengi wa
unaowashirikisha hawana Nia ya dhati pamoja na tamaa za kuomba omba viposho