ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 17,569
- 41,676
Maisha ni kama hadithi
Pindi tu unapozaliwa, ukurasa mpya wa hadithi hufunguliwa
Unajikuta kwenye dunia ukiwa mgeni kabisa, na jambo la ajabu zaidi ni kwamba hujui ulipotoka
Ukiachana na simulizi za Biblia na Qur’an, bado huna uhakika mkubwa kuhusu safari yako ya kuja hapa
duniani wewe ni mgeni tu
Unakutana na watu, unaambiwa
Huyu ni baba yako.
Huyu ni mama yako.
Huyu ni kaka yako.
Huyu ni dada yako.
Na hapo ndipo safari inaanza
Katika hii safari, hadithi hutofautiana sana
Hadithi ya Juma jirani yenu haiwezi kuwa sawa na hadithi yako
Mfano, Juma huenda amezaliwa kwenye familia ya wasomi, wafanyabiashara, wafugaji au wakulima wenye uwezo
Juma ana uhakika wa kula milo mitatu kwa siku, tena lishe bora Utapiamlo kwake ni jambo la nadra sana
Anapoenda shule, anavaa nguo safi, viatu vizuri na mkanda mzuri
Njiani anasifiwa shuleni anapendwa, na kila mtu anatamani kuwa rafiki yake
Juma analelewa kwa upendo Anapakwa mafuta, anaongezeshwa vizuri anakua akiwa na amani kwa sababu hana trauma wala hajapitia bullying
Ana wazazi wote wawili, na karibu kila anachokitaka anakipata
Kwa kifupi, Juma anakuta ukurasa wa maisha yake tayari umeboreshwa Kinachobaki ni kuendelea pale alipoanzia
Lakini tukimwangalia mwingine, tumwite Ali (Kuna rafiki yangu anaitwa Ali akijua nimetumia jina lake kwenye hii story 😅😅 Ali kama unatumie JF basi mi ni S🤪)
Hadithi yake inaanza tofauti kabisa Changamoto zake zinaanza hata kabla hajazaliwa yaani kasheshe
Mama yake Ali alikuwa akiishi kwa huzuni na vilio wakati akiwa na ujauzito, kwa sababu baba yake Ali alikuwa mlevi kupindukia
Kila aliporudi nyumbani akiwa amelewa, alimshushia kipigo mama yake Ali😢
Mama yake Ali akaishi kwenye msongo mkubwa wa mawazo mpaka anajifungua
Na ukweli ni kwamba, mtu mwenye msongo wa mawazo mara nyingi huwa vigumu hata kulea au kuwatreat vizuri wengine
Ali akajikuta anakulia kwenye mazingira ya baba mlevi asiye na future yoyote kwa mtoto wake, na mama mwenye uchovu wa maisha na majeraha ya moyo💔
Ali akidondosha kikombe tu, mama anaona amerithi ukorofi wa baba yake
Anaanza kupigwa na kutukanwa bila kosa lolote kubwa (kuna wazazi wanachapa yoo🙌)
Mama yake Ali hana muda wala nguvu za kumlea vizuri
Anafanya kazi nzito, anarudi amechoka, hata sabuni ya kufulia ni shida ile ya kuoshea vyombo ndiyo hiyo hiyo ya kufulia nguo
Nakumbuka mpaka ule msemo wa msanii sijui ni Lapcha ule wimbo sijui ni Champion hata sikumbuki vizuri
Nitasahihishwa;[ ili sabuni lisiishe si tulinyoa madongo]
I
Ali anaenda shule na nguo chafu Anaanza kuona tofauti kubwa kati yake na akina Juma
Anaanza kuingia kwenye msongo wa mawazo akiwa bado mdogo
Anakua huku akili na mwili vikiwa vimechoka
Ukurasa wa maisha yake tangu akiwa tumboni tayari ulikuwa umejaa wino kila sehemu
Maskini Ali… 😢
Wewe unadhani Ali akiwa mkubwa atakua nani?
Wewe unadhani Juma akiwa mkubwa atakua nani?
Maisha kweli ni hadithi
Sasa wewe hadithi yako ya maisha ipo upande gani? Ya Juma au ya Ali?
Sikukuu njema for all Muslims
Simu hazijaita🤪
ShesRise_1 👋