Kipi ni Bora kwako: Kununua nguo/kiatu kimoja brand/OG kwa bei kubwa au kununua copy nyingi kwa bei ndogo?

Kipi ni Bora kwako: Kununua nguo/kiatu kimoja brand/OG kwa bei kubwa au kununua copy nyingi kwa bei ndogo?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,800
Wakuu.
Upi mtazamo wako kwenye bei inapokuja swala la kununua mavazi, nguo au mikoba nk?

Kuna viatu vinauzwa zaidi ya $200 (zaidi ya Tsh 500,000) wakati kiatu iko iko kwa muonekano unakipata Kariakoo kwa Tsh 50,000!
IMG_5879.jpeg


Pia kwa mikoba ya brand maarufu kama LV, Gucci, Hermes nk unakuta unauzwa hadi million kadhaa, ila unaweza kupata “mchina” kwa 0.1% ya iyo bei.
IMG_5880.jpeg


Mifano itaenelea ivyo ivyo kwa tshirts, suruali, makoti etc.

Nauliza tu, ni bora kipi, kununua mfano kiatu pair moja kwa laki 5 “OG” au kununua pair 5 rangi tofauti tofauti labda kwa elfu 50 kila moja na chenji ikabaki?

Au wenzangu uwa mnazingatia brand na authentic?

Mada haihusiani na appliances kama TV, radio, pasi, simu na electronics nyingine wala vyakula na urembo wa perfumes na mafuta.
 
Naunga mkono hoja. Kama hela ipo hutakumbuka hata kuandika uzi. Mleta mada ni maskini anayetaka kufuata mkumbo.
hapo naona tuhuma za umaskini hazina ukweli wowote, ungezitoa tu labda tu iwe maamuzi ya mtu mwenyewe kununua copy au og ni kama biashara ya malori mtu kununua Howo au Scania inatokana na maamuzi ya mmiliki.
 
Back
Top Bottom