Kipi chakula chako pendwa?


Sawa.
 
Kipenzi Changu unaitwa huku. 🤪
Napenda wali dagaa sana. Bahati mbaya kinaonekana kama chakula duni,wakati mwingine naonekana naagiza kwa sababu nimeishiwa.
Siku moja mgahawani nikaagiza wali dagaa, dada akaniambia dagaa anauza na ugali tu. Nikamwambia naomba nisaidie tu wali dagaa, dada akaniambia kwa sauti kama huna hela anipe wali mchuzi. Daah nikaumia sana

Ukibidi nilinde heshima
Nikamwambia lete ugali dagaa na wali, alipoleta nikamwambia huu ugali kamwage halafu naomba bill ya watu wanaokula muda huu.
 
Dagaa la aina gani
Dagaa bukoba
Dagaa mwanza
Dagaa mchele
 
Hahahaaa. Kweli uliilinda heshima. Hongera.

Mie kuna muda natamani kula Ubwabwa na dagaa wale wa Mwanza japo sasa hao dagaa napenda nikipika mwenyewe ndo nawaelewa sio wa kupikiwa wala kununua mgahawani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…