Kipi cha ziada kwenye line ya tigo ya 4G

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
14,537
31,686
Wakuu leo nimepigiwa simu na Tigo wakidai wanatoa offer ya line za 4g kwa watumiaji wa internet, yani napewa hiyo line kwa namba yangu ile ile!

Sasa kabla sijaamua kuifata na kubadilisha line nataka nijue faida gani ambazo zipo katika hiyo line kulinganisha na hiz za kawaida??
 
kabla hujafanya huo uamuzi jiulize mambo haya
1. simu yako inakubali 4g? kama inakubali ina frequency ya 4g ya tigo?
2. eneo lako unalokaa kuna signal za 4g?

kama ina 4g na unapokaa kuna mnara wa 4g ni vyema uka upgrade kwenda 4g kuna faida nyingi kama vile speed kubwa ya internet na pia watumiaji wa 4g ni wachache hivyo service inakuwa ya uhakika hakuna kubanana watu kibao mnara 1
 
Asante mkuu natumia Samsung galaxy note 4, nadhani inasupport 4g
 
3G imewashinda wanakimbilia 4G, wangeboresha kwanza ngazi za chini ndipo wasogee mbele. Siongei kiunafiki wala nini Maeneo ya Himo Kilimanjaro kuipata 3G ya Tigo ni shida sana.
Sijui huwa wanawaza nini!? Jamaa yangu kahamia Kigambino imembidi mpaka anunua sim card ya Voda. Mimi mwenyewe nikitoka mjini nikifika maskani kimara stop over internet sipati yaani imenibidi kuwa na laini nyingine yaani kwa ajili ya internet jumapili nikiwa home. Yaani hovyo kabisa halafu wanakimbilia 4g . maajabu kweli.
 
kabla hujafanya huo uamuzi jiulize mambo haya
1. simu yako inakubali 4g? kama inakubali ina frequency ya 4g ya tigo?
2. eneo lako unalokaa kuna signal za 4g?

kama ina 4g na unapokaa kuna mnara wa 4g ni vyema uka upgrade kwenda 4g kuna faida nyingi kama vile speed kubwa ya internet na pia watumiaji wa 4g ni wachache hivyo service inakuwa ya uhakika hakuna kubanana watu kibao mnara 1
Hii 4g ya tigo ni magumashi sana. Sehemu nilipo kuna 4g na ninatumia line yao na simu yangu ina support 4g. Ila cha kushangaza kitu hata cha 5Mb inaweza kuchukua dk 15 kudownload.
 
Ni hivi hizo technology hapa bongo ni magumashi tu. 3g kama ingefungwa na kusambazwa ipasavyo inatosha kabisa kwa matumizi ya kawaida ya Internet lakini kilichopo ni kwamba minara mingi haina hata hiyo 3g. Kwa Dar tu ukienda pembeni kidogo ya jiji minara kibao ni 2g na ukienda mikoani 3g ndio michache zaidi. Hivyo usipoteze muda wako kuingia hiyo 4g
 
1. kunaweza kuwa na 4g lakini wewe ukawa hutumii 4g kwa wakati huo, umehakiki kama unatumia 4g? kuna baadhi ya simu h+ zinasoma kama 4g hizi kitaalamu hazina 4g

2. signal unapataje? tigo huathiriwa sana na signal zikiwa kidogo na speed hushuka

3. cheki na TTCL na smart vifaa vingi vinavyokubali 4g ya tigo hukubali na smart.

pia ukieka eneo na aina ya simu sio mbaya pengine kuna mtu karibu yako anaweza toa maelezo zaidi
 
1. si kweli kama 3g inatosha nakupa hizi sababu
-3g speed inapanda na kushuka mara kwa mara
-3g haitoi quality nzuri wakati wa kupiga simu
-movie za full hd (zina zaidi ya 1gb) bado zinachukua muda mrefu kudownload kwa 3g tuna flat tv siku hizi zina resolution hadi 4k ya nini tubaki na internet slow?
-video call maofisini
nk nk nk

sababu unatuma tu msg za whatsapp haimaanishi watu wote ni kama wewe even 4g haitoshi internet za mobile data ni nadra kukuta latency single digit bado tunahitaji internet bora zaidi.

na sababu eti hujajenga nyumba nyumba ya vigae ndio ukatazwe kujenga ghorofa? tupo ulimwengu wa kibepari tigo hana jukumu lolote la kusambaza internet mahala maalumu sio serikali hawa kwamba maeneo yote waeke minara wanaangalia faida. kama eneo lako hawashiki hama nenda mtandao unaoshika hio ndio sheria ya ubepari. tunaotakiwa tuwalalamikie ni mashirika yetu ya uma kama TTCL wao ndio wana jukumu la kutufikia watz wote
 
1. kunaweza kuwa na 4g lakini wewe ukawa hutumii 4g kwa wakati huo, umehakiki kama unatumia 4g? kuna baadhi ya simu h+ zinasoma kama 4g hizi kitaalamu hazina 4g

2. signal unapataje? tigo huathiriwa sana na signal zikiwa kidogo na speed hushuka

3. cheki na TTCL na smart vifaa vingi vinavyokubali 4g ya tigo hukubali na smart.

pia ukieka eneo na aina ya simu sio mbaya pengine kuna mtu karibu yako anaweza toa maelezo zaidi
Natumia Note 5, Nipo Morogoro town. Kama mida hii nipo karibu kabisa na ofisi zao. Na hii mara nyingi inakuwa hivyo hata nikiwa Dom sehemu yenye coverage ya 4g.

Hadi huwa naamua ku set kwenye 3g only ndio net inakuwa faster.

93437750a243318b62cb4bd68d8078da.jpg
 
3G imewashinda wanakimbilia 4G, wangeboresha kwanza ngazi za chini ndipo wasogee mbele. Siongei kiunafiki wala nini Maeneo ya Himo Kilimanjaro kuipata 3G ya Tigo ni shida sana.

Sio lazima mtandao u cover maeneo yoyote wanasema Tigo 4G ipo Dar nzima ila ukienda hapo Nyuma ya Ubalozi wa Ufaransa Kinondoni biafra haukuti 4G.
You have plenty of options halotel,airtel and vodacom ukiamua kutumia mtandao fulani lazima uwe unajua coverage yake iko vizuri
 
Back
Top Bottom