Wasalaam
Najaribu kupata uzoefu toka kwa wadau!
Binafsi hufanya safari za Mara kwa Mara kwa barabara! Katika safari zangu za mkoa wa Rukwa safari yangu huwa inaingiwa na ukakasi nikishafika Mbeya Mjini nikianza kuitafuta Tunduma.
Sijui wewe mdau kipande gani kinakutesa kutokana na Barabara kutokuwa rafiki na hali ya safari kwa ujumla
1.Ifakara,Lupilo to Mahenge
2.Kasulu-Nyarugusu- Kibondo-Nyakanazi
3.Nzega-Kahama unapita katikati unatokea Kagongwa..nimesahau jina ila ni by bass ya kutozungukia Tinde,kama 40kms hivi..
4.Karagwe to Rulenge- Kabanga- Kyerwa..dah aisee
5.Mkta - Handeni-Kilindi
6.Singida -Nzega barabara ina vipara na mashimo tena hatari hii ya mvua..kama haina lami hivi
7.Makambako- Mbeya-Tunduma..barabara ishakuwa finyu sana (narrow),ina altitude changes za ghafla,lama haiko grip..kuteleza (skidding) kwa matairi ni obvious situation hasa muda wa usiku..maeneo yale usiku hupoa sana then kuna umande..
7.Chunya -Lupa- Makongolosi mpaka Sikonge..na vitongoji jirani...iyo heshima..
Kuna sehemu unapita unajiuliza bado uko inji hii au???ajabu kuna utajiri na rasilimali nyingi ajabu..
Nashukuru kwa kujitembeza kwangu,yale mawazo mgando ya kitoto ya kuamini mitikasi iko Dar na miji mikubwa yaliisha siku hizohizo..
Truth be told with honesty,nchi yetu inahitaji uwekezaji mkubwa wa kujenga miundo mbinu msingi kwa sana..
Nina binamu yangu huwa ana Asthma,siku ilimbana tukiwa huko..,kama sio ujuzi,busara na hek'ma za mdau mwenyeji..
Walahi shangazi yangu ningemrejeshea cadava, kuna mzee alitupatia mizizi imetokoswa na udadambwi mwingine..maisha yakendelea..