Kioo kinatuonyesha ukweli kwa kiasi gani?

Mimi ni yule ninayependa kutoa nguo zote na kusimama mbele ya kioo nijikague, nisipoziona "six packs" zangu naanza zoezi chap na diet, pia ni yule baada ya kujitizama nitaanza kucheza cheza na kutabasamu, nakiamini kioo kwa 95%
 
😊😊😊 Nimeipenda hii chemsha bongo. Inaonyesha unapenda kugeuza jambo la kawaida liwe mjadala wa kufikirisha

Kitaalamu, mtu wa kwenye kioo sio wewe halisi, bali ni virtual image—taswira inayotengenezwa na mwanga unaorudishwa na kioo. Kioo cha kawaida (plane mirror) kinaonyesha umbo lenye ukubwa karibu sawa na halisi, lakini kinafanya upande wa kushoto na kulia uonekane umebadilika

Ndiyo maana vioo tofauti vinaweza kutupa taswira tofauti; mviringo wa kioo, ubora wake na mwanga wa mazingira vinaathiri unavyoonekana. Kwa hiyo sio kila kioo kinapotosha wewe, bali mazingira na aina ya kioo hubadilisha namna taswira inavyojitokeza.

Nakupa, pongezi kwa maandishi yako. Kitu kinachoonekana kwenye post zako ni kwamba zinachochea watu kutoa mawazo na kujadiliana, ndiyo maana mara nyingi zinapata interaction nyingi na replies nyingi. Criticism za mtandaoni ni sehemu ya mjadala, lakini uwezo wa kuanzisha mazungumzo yanayowafanya watu wafikirie ni kitu cha thamani. Endelea kuandika

Keep it up 😊😊😊 Platnum badge unastahili kupewa
Shukran sana bro
Vip unaamini kioo chako
 
😂 Hii si wenge, ni swali zuri tu la kutafakari.

Wewe ni yule aliye mbele ya kioo; wa ndani ni taswira yako (reflection). Na vioo tofauti vinaweza kukuonyesha tofauti kwa sababu ya ubora wa kioo, mwanga, angle na hata kama kioo kimepinda kidogo.

Kwa hiyo hakuna kioo kinachokupa “wewe halisi” kwa 100%. Kioo kinaonyesha tu jinsi mwanga unavyoreflect.

Ila wewe ukijiangalia ukatabasamu, hapo kioo kimefanya kazi yake vizuri 😂🤗
Ohooooo kuumbe
Kioo kinaonesha jinsi mwanga una vyo reflect asante kwa maoni mkuu
Karibu tena
 
Leo nimejiangalia kwenye kioo na mirror exercise nikajikuta nabubujikwa na machozi😭

Kioo, jakidanganyi, ni wewe kabisa, zile tilting za angle pamoja na reverse 🔀 ya left and right ni kweli zina badili muonekano ila ni kwa asilimia chache mno. Na facial pattern utabaki kuwa ile ile,

So hauwezi kusema kioo kinadanganya.
Kama ni mbaya kubali tu, na kama ni handsome kubali pia,

Kazi ya Mungu haina makosa

Mimi nimekubali, ni ugly. Ninameno kama ya Pimbi, na hakuna mrembo wa kunikubali so kujikubali ndo kumeniweka huru.
 
Kwanza kabisa, achana na yeyote anayeuliza mbona unaandika sana, kuandika ni tiba ya akili na ni sehemu ya kushare maarifa, we endelea kutoa madini humu JF!

Iko hivi kioo huwa hakionyeshi uhalisia wa jinsi watu wengine wanavyokuona live. Kazi kubwa ya kioo ni kugeuza mwelekeo wa mwanga, ndio maana ukinyosha mkono wa kulia kwenye kioo unaonekana upande wa kushoto, maana yake nini? Unachoona kwenye kioo ni flipped au reversed image.

Na hii ndio sababu ukipiga selfie au picha ya kawaida, unaweza kuhisi sura yako imebadilika kimtindo.

Utofauti wa jinsi unavyoonekana kwenye kioo unatokana na utengenezwaji wa kioo chenyewe, vioo vingi vya kawaida ni flatness deviation. Kioo kikishakuwa na subtle curvature hata kama ni ndogo sana, kina uwezo wa kukufanya uonekane mwembamba, mnene, mrefu, au mfupi. Zaidi ya hapo ile reflective coating ndio huwa inaamua jinsi wewe utakavyojiona kwenye hicho kioo.

Kuna uvumbuzi unaitwa true mirror. Hiki ni kioo kilichotengenezwa kwa kuunganisha vioo viwili vikiwa vimepishana kwa nyuzi 90, hiki chenyewe hakigeuzi upande ukinyosha mkono wa kulia, kinaonyesha mkono wa kulia upande ule ule, sawa kabisa na jinsi watu wengine wanavyokuona live. Watu wengi waliojiangalia kwenye true mirror kwa mara ya kwanza waliishia kupata psychological shock kwa sababu walijiona wapo tofauti kabisa na walivyozoea kujiona kwenye vioo vya kawaida.

Kihistoria, kioo kina mtazamo wa kiroho na kiimani, tangu zamani tamaduni nyingi zimekichukulia kioo kama gateway to the subconscious , ndio maana unapotabasamu mbele ya kioo na kujihisi vizuri, kiuhalisia unakuwa una reflect positive energy na kuirudisha kwako mwenyewe yani ni kama aina fulani ya kujibariki na kujitengenezea utulivu wa nafsi. Kioo kina tabia ya kukuza kile kilichopo moyoni mwako, ukiwa na amani ukijiangalia, kioo kinakurudishia hiyo amani mara mbili yake and vice versa.
 
Mkuu maada zako ni chokozi sana. Bado nawaza nini huwa motive kwako mpaka kupata hizi maada?

Anyway binafsi nafikiri kioo kinaonesha asilimia 90-100% ya uhalisia wetu lakini pia hutegemea na aina ya kioo.

Magari yote na pikipiki hutumia kioo kuonyesha mbele, nyuma na ubavuni na ukifanya chochote kinyume na kioo matokeo yake huonekana ni mabaya. Hivyo utakubaliana namimi kwamba kioo ni halisia.

Based on hearsays: Kwamba wachawi nao hutumia kioo kufanya mambo yao. Waganga nao hutumia kioo kupiga ramli.

Hivyo naweza kuhitimisha kwa kusema kioo huonyesha uhalisia wa kitu/mtu.

Binafsi sipendi kioo, at some point naweza kusema nakichukia tuu ila sina sababu za msingi. Hii kukichukia ilichagizwa na mazingira fulani

Nilikuwa naishi Mbezi Goigi, jamaa tuliyepanga nae akaingia chumbani kwangu akaona Sina kioo nayeye alikua navyo viwili akanipa kimoja pasipo kumuomba. Aisee kile kioo kilikua na maajabu mwisho wa siku nilikivunja akaishia kunikasirikia.

Toka hapo sioipendi zaidi kioo, nikipita sehemu inakioo huwa nakwepa kabisa kujiangalia. Kama ninahaja ya kujiangalia bhasi huwa natumia kioo cha simu.
 
Kwanza kabisa, achana na yeyote anayeuliza mbona unaandika sana, kuandika ni tiba ya akili na ni sehemu ya kushare maarifa, we endelea kutoa madini humu JF!

Iko hivi kioo huwa hakionyeshi uhalisia wa jinsi watu wengine wanavyokuona live. Kazi kubwa ya kioo ni kugeuza mwelekeo wa mwanga, ndio maana ukinyosha mkono wa kulia kwenye kioo unaonekana upande wa kushoto, maana yake nini? Unachoona kwenye kioo ni flipped au reversed image.

Na hii ndio sababu ukipiga selfie au picha ya kawaida, unaweza kuhisi sura yako imebadilika kimtindo.

Utofauti wa jinsi unavyoonekana kwenye kioo unatokana na utengenezwaji wa kioo chenyewe, vioo vingi vya kawaida ni flatness deviation. Kioo kikishakuwa na subtle curvature hata kama ni ndogo sana, kina uwezo wa kukufanya uonekane mwembamba, mnene, mrefu, au mfupi. Zaidi ya hapo ile reflective coating ndio huwa inaamua jinsi wewe utakavyojiona kwenye hicho kioo.

Kuna uvumbuzi unaitwa true mirror. Hiki ni kioo kilichotengenezwa kwa kuunganisha vioo viwili vikiwa vimepishana kwa nyuzi 90, hiki chenyewe hakigeuzi upande ukinyosha mkono wa kulia, kinaonyesha mkono wa kulia upande ule ule, sawa kabisa na jinsi watu wengine wanavyokuona live. Watu wengi waaliojiangalia kwenye true mirror kwa mara ya kwanza waliishia kupata psychological shock kwa sababu walijiona wapo tofauti kabisa na walivyozoea kujiona kwenye vioo vya kawaida.

Kihistoria, kioo kina mtazamo wa kiroho na kiimani, tangu zamani tamaduni nyingi zimekichukulia kioo kama gateway to the subconscious , ndio maana unapotabasamu mbele ya kioo na kujihisi vizuri, kiuhalisia unakuwa una reflect positive energy na kuirudisha kwako mwenyewe yani ni kama aina fulani ya kujibariki na kujitengenezea utulivu wa nafsi. Kioo kina tabia ya kukuza kile kilichopo moyoni mwako, ukiwa na amani ukijiangalia, kioo kinakurudishia hiyo amani mara mbili yake and vice versa.
MIRROR FACT related to BRAIN

Kadiri unavyojiangalia kwenye mirror mara nyingi, ndivyo unavyoweza kuwa sensitive zaidi .

hii ni kwasababu ya tiny imperfections ambazo watu wengine hawazioni kabisa.

Ubongo wako huanza kujifunza uso wako kwa detail pimple ndogo, asymmetry ya lips, eyebrow moja kuwa juu kidogo.

Halafu attention yako inazipa importance kubwa kuliko zilivyo objectively.

Then you start seeing yourself as nothing but flaw and bad looks.
 
Kwanza kabisa, achana na yeyote anayeuliza mbona unaandika sana, kuandika ni tiba ya akili na ni sehemu ya kushare maarifa, we endelea kutoa madini humu JF!

Iko hivi kioo huwa hakionyeshi uhalisia wa jinsi watu wengine wanavyokuona live. Kazi kubwa ya kioo ni kugeuza mwelekeo wa mwanga, ndio maana ukinyosha mkono wa kulia kwenye kioo unaonekana upande wa kushoto, maana yake nini? Unachoona kwenye kioo ni flipped au reversed image.

Na hii ndio sababu ukipiga selfie au picha ya kawaida, unaweza kuhisi sura yako imebadilika kimtindo.

Utofauti wa jinsi unavyoonekana kwenye kioo unatokana na utengenezwaji wa kioo chenyewe, vioo vingi vya kawaida ni flatness deviation. Kioo kikishakuwa na subtle curvature hata kama ni ndogo sana, kina uwezo wa kukufanya uonekane mwembamba, mnene, mrefu, au mfupi. Zaidi ya hapo ile reflective coating ndio huwa inaamua jinsi wewe utakavyojiona kwenye hicho kioo.

Kuna uvumbuzi unaitwa true mirror. Hiki ni kioo kilichotengenezwa kwa kuunganisha vioo viwili vikiwa vimepishana kwa nyuzi 90, hiki chenyewe hakigeuzi upande ukinyosha mkono wa kulia, kinaonyesha mkono wa kulia upande ule ule, sawa kabisa na jinsi watu wengine wanavyokuona live. Watu wengi waliojiangalia kwenye true mirror kwa mara ya kwanza waliishia kupata psychological shock kwa sababu walijiona wapo tofauti kabisa na walivyozoea kujiona kwenye vioo vya kawaida.

Kihistoria, kioo kina mtazamo wa kiroho na kiimani, tangu zamani tamaduni nyingi zimekichukulia kioo kama gateway to the subconscious , ndio maana unapotabasamu mbele ya kioo na kujihisi vizuri, kiuhalisia unakuwa una reflect positive energy na kuirudisha kwako mwenyewe yani ni kama aina fulani ya kujibariki na kujitengenezea utulivu wa nafsi. Kioo kina tabia ya kukuza kile kilichopo moyoni mwako, ukiwa na amani ukijiangalia, kioo kinakurudishia hiyo amani mara mbili yake and vice versa.
Mkuu umeiweka vyema sana hii. Hasa hapo kwenye reflection.
Nafikiri ile picha ya kwenye kioo ndio reflection of our energy that given out.
 
MIRROR FACT related to BRAIN

Kadiri unavyojiangalia kwenye mirror mara nyingi, ndivyo unavyoweza kuwa sensitive zaidi .

hii ni kwasababu ya tiny imperfections ambazo watu wengine hawazioni kabisa.

Ubongo wako huanza kujifunza uso wako kwa detail pimple ndogo, asymmetry ya lips, eyebrow moja kuwa juu kidogo.

Halafu attention yako inazipa importance kubwa kuliko zilivyo objectively.

Then you start seeing yourself as nothing but flaw and bad looks.
Fact kubwa sana hii mkuu, na hii ndio sababu kubwa inayofanya watu wanaopenda kupiga picha za selfies na kutumia filters kila saa kwenye mitandao kuishia kupoteza self confidence yao wakijitazama kwenye vioo vya kawaida.
 
Duh.... swali la nyongeza!!! kama kusingekuwa na kioo, tungejitambuaje kwamba hii ni sura yangu? .....

Mimi hua sikiamini sana kioo, maana wakati mwingine naweza kujitazama nikaonekana ni handsome sana....

Sometime kinaonesha vibaya hadi unaanza kujiona hufai mbele za watu....

Halafu huyo aliyesema unaandika sana... Kama hawezi kusoma apite kando....
Kwa kujiangalia tu mwenyewe kupitia kioo sidhani kama utagundua wewe ni handsome ama beautiful. 😄

Ili ujue wewe ni handsome/beautiful walau watu wasiopungua kumi wakutamkie waziwazi tena wa jinsia zote.😄

Kama hujawahi kuambiwa na watu kuanzia kumi basi wewe upo kundi la kina Masoud Surambaya.😄
 
Mkuu umeiweka vyema sana hii. Hasa hapo kwenye reflection.
Nafikiri ile picha ya kwenye kioo ndio reflection of our energy that given out.
The world is a mirror, it returns to you what you features inside.

Ndio maana unaweza kukutana na mtu ambaye physically ni wa kawaida sana akisimama mbele ya kioo lakini akisimama mbele ya watu anaonekana ana mvuto wa hatari.
 
Kioo hakionyeshi sura yako 100% japo ni very close .

Kioo kina invert picha kulia inakuwa kushoto na kushoto inakuwa kulia.

Kwahiyo taswira ya kioo sio taswira anayo kuona nayo mtu halisi .

Mirror = very close. But not exactly 100% reality.
Eeeh taswira ya kioo sio anayokuona nayo mtu halisi🤔
Hapa sasa ????
 
Taswira unayoiona kwenye kioo sio vile watu wanavyokuona kwa sababu kwenye kio Taswira yako inakua imegeuzwa, pili kwanini watu wengi hujikosoa muonekano wao jibu ni kuwa ushazoea sura yako hivo ukiiangalia unajikita kwenye kujikosoa zaidi tofauti na vile unapomuona mtu mwingine kwa mara ya kwanza
Mkuu sijakuelewa
Unakua umezoea sura yako
Umeizoea kwa kuiona wapi?
Kwenye kioo?
 
Mimi naamini kioo 100%

Nikichukua mfano glass yenye maji ama kitu kingine chochote nikaangalia kwenye kioo na nikiangalia kwa kawaida image ni ile ile

Kutokuamini kioo = kutokuamini macho yako 😁
Sijazungumzia kioo kwa kujiona mbaya au mzuri
Ila je hiyo taswira yako unayoiona kwenye kioo unaamini kwa kiasi gani kama ni wewe halisi ?
 
Mimi ni yule ninayependa kutoa nguo zote na kusimama mbele ya kioo nijikague, nisipoziona "six packs" zangu naanza zoezi chap na diet, pia ni yule baada ya kujitizama nitaanza kucheza cheza na kutabasamu, nakiamini kioo kwa 95%
Wow 👌
Kuna raha kwa kweli kucheza huku unakisogelea kioo

Sema watu tukiwa wenyewe tuna ujinga mwingi watu wanakuheshimu vizuri tu kumbe ukiwa naked mbele ya kioo unafanya ujinga😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom