Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Kiongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai nchini Tanzania, Laigwanan Isack Olekisongo, ametoa wito kwa jamii hiyo kote nchini kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, huku akisisitiza umuhimu wa kuwachagua madiwani na wabunge watakaowaletea maendeleo.
Akihutubia maelfu ya Wamaasai katika eneo la kimila la Elerai mnamo Agosti 1, 2025, Olekisongo aliwataka vijana wa jamii hiyo kuwa mstari wa mbele katika kushiriki uchaguzi, huku akieleza kuwa kwa upande wa urais, jamii hiyo inapaswa kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassan, akimtaja kama kiongozi wa mfano ukilinganisha na marais waliopita.
"Uchaguzi wa vyama unaendelea, chagueni mnavyotaka, lakini Tanzania nzima inajua Wamaasai ni CCM, kile chama cha Nyerere. Mtu asije akahoji kwa nini, maana huo ni umoja wetu," alisema Olekisongo.
Hata hivyo, kauli hiyo imeibua upinzani kutoka kwa baadhi ya vijana wa jamii hiyo, waliopinga vikali madai ya kiongozi huyo wa kimila.
Wameeleza kuwa wana uhuru wa kuchagua chama wanachokitaka, huku baadhi yao wakijitambulisha kama wafuasi wa vyama vingine, wakisisitiza kuwa si sahihi kuunganisha jamii nzima na chama kimoja cha siasa.