Kinyume cha asante (thanks)!

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
Wataalamu wa lugha naomba mnijulishe kinyume cha neno "Asante" au "Thanks" kwa kingereza.

Natanguliza shukrani.
 
Nionavyo mimi asante ni neno la kushukuru mtu akifanyiwa hisani fulani. Kama mtu hataki kushukuru, kwa kawaida hasemi kitu, hubaki kimya - hivyo hakuna kinyume cha moja kwa moja ya neno "asante" au "thanks".
 
kinyume cha asante ni ile asante ya jicho fulani hivi la kama jamaa akirudia tena utamfanya kitu mbaya.
 
kinyume cha asante ni ile asante ya jicho fulani hivi la kama jamaa akirudia tena utamfanya kitu mbaya.

sasa mkuu kama mlengwa ni kipofu, atajuaje kuwa umempiga hilo jicho?
ninachojaribu hapa ni kupata neno unaloweza kulitamka litakalomaanisha kinyume cha neno asante
 
Hapa umekusudia nini? Tafadhali jibu kabla sijazidi kukasirika.

Excuse me! unamaanisha nini??

Wakuu msikasirike, Binafsi nilivyomuelewa Jamaa anamaanisha kuwa kama mtu amekukera unatumia hayo maneno kumfikishia ujumbe, nadhani kwa mujibu wake hicho ndiyo kinyume cha neno asante.. At least hivyo ndivyo nilivyomwelewa. Hope hakukusudia kumkera mtu yeyote!

Peace.
 
asante kwa kutuelewesha binafsi kwa mbaaali nilikereka
 
Kwa mujibu wa mahusiano ya kileksikoni katika lugha, si lazima kila neno liwe na kinyume chake.. Nadhani neno 'ahsante' huangukia katika maneno yasiyo na kinyume.
 
sasa mkuu kama mlengwa ni kipofu, atajuaje kuwa umempiga hilo jicho?
ninachojaribu hapa ni kupata neno unaloweza kulitamka litakalomaanisha kinyume cha neno asante

hilo jicho hata kipofu atahisi unamuangalia....maana litakuwa jicho fulani hivi......we hujawahi kukaa sehemu ukahisi kama vile mtu anakuangalia ingawa humuoni?
 
hilo jicho hata kipofu atahisi unamuangalia....maana litakuwa jicho fulani hivi......we hujawahi kukaa sehemu ukahisi kama vile mtu anakuangalia ingawa humuoni?

Duh, ngoja nitafanya uchunguzi, Lol!
 
Neno asante/ Ahsante, hujitokeza katika mazingira maalumu, ambapo huwa ya labda kufariji, kupoza,Kukribisha, kushukuru, na kutaka radhi.
Kinyume chake ni maneno kama
Pole
Nashukuru
Karibu
 
Back
Top Bottom