Measuring Cup kwa upimaji mafuta ya kula duka la mangi

Measuring Cup kwa upimaji mafuta ya kula duka la mangi

Tumpara Dudu

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Posts
662
Reaction score
606
Salamu kwenu wakuu.
Ammaabaad. Wakuu mm nauza duka la mangi lkn Nina changamoto katika upimaji wa mafuta ya kula.

Kwenye mazingira lilipo duka langu wakazi wa huku wamezoea vipimo vya 300,500, robo nusu na Lita. Sasa robo,nusu na Lita si tatizo lakini changamoto ni vipimo vya TSH 300 na 500. Nimepiga hesabu vizuri Kwa Bei ya 5'000 Kwa Lita basi kipimo Cha 300 kutakuwa ni ml 60 na 500 ni ml 100.

Sasa naomba mnijulishe,wapi naweza kupata instrument za kupima kuanzia ml 60 kwenda juu Ili niepukane na maswala ya kukadiria yanayonipa hasara?
 
Vyote Hivyo Siyo Vipimo Ni Kangomba
Tumia Vipimo Sahihi Tofauti Na Hapo
Unafanya Makosa

Watembelee Mafundi Majiko
 
Salamu kwenu wakuu.
Ammaabaad. Wakuu mm nauza duka la mangi lkn Nina changamoto katika upimaji wa mafuta ya kula.
Kwenye mazingira lilipo duka langu wakazi wa huku wamezoea vipimo vya 300,500, robo nusu na Lita. Sasa robo,nusu na Lita si tatizo lakini changamoto ni vipimo vya TSH 300 na 500. Nimepiga hesabu vizuri Kwa Bei ya 5'000 Kwa Lita basi kipimo Cha 300 kutakuwa ni ml 60 na 500 ni ml 100.

Sasa naomba mnijulishe,wapi naweza kupata instrument za kupima kuanzia ml 60 kwenda juu Ili niepukane na maswala ya kukadiria yanayonipa hasara?
Ipo hivi koroboi 10 == 1/4 ya mafuta utakuta imeandikwa 0.025 kama hawajaandika usiwe na shaka kwahiyo angalia bei unayouza katika robo kisha ugawe mala 10 ndipo utajua mafuta ya 500 na 300 upime koroboi ngapi
 
Sijajua upo mkoa gani.... kwa hali ya sasa ukiendekeza mafuta ya 300 unaweza kuishia kuchezea hasara ! Huyo alonunua ya 300 anataka na nyongeza !

Ushauri, tafuta vikopo pima ya 500, 1000, robo nusu na kuendelea! Pima vikopo vingi vingi , uza vikiisha pima tena ! Faida yake vinasave muda, pia hakuna ule usumbufu wa nyongeza.... hii nyongeza inakata hela sana !!!!
 
vipimo vya size hiyo mara nyingi ni makadirio, chukua sampo kwa jirani huenda ikakulipa kuliko kutegemea huo ujazo unaoutafuta
 
Back
Top Bottom