Kingunge amechanganyikiwa?

Jamani tulishawahi kuujadili vyakutosha huko nyuma kuhusiana na waraka huu. Huyu mzee anajua tofauti kati ya waraka na ilani. Lakini kwa makusudi kabisa anaamua kutumia neno "ILANI" mahali pa "WARAKA" ili kuwapumbaza watu kuwa kanisa linaandaa ilani (manifesto) itakayofuatwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi ujao. Huu ni opotoshaji mkubwa ambao watu wenye mawazo na mtizamo chanya wanapaswa kumkemea huyu babu. Iweje watu waelekezwe namna ya kuchagua miongoni mwetu viongozi waadilifu iwe ni kuchochea udini? Au ni kwa namna gani watu wakumbushwe jinsi ya kujali utu na rasilimali za taifa iwe ni ubaguzi? Ni kwanini huyu mzee hataki kuonyesha kwenye huo waraka mahali ama vipengele vinavyohashiria udini ama machafuko katika jamii? Nafikiri kuna sababu ya kumpuuza kwa kukaa kimya kwani pia hiyo ni adhabu tosha.

Mkuu, binafsi sihangaiki sana na title ya waraka - Manifesto au Ilani - bali content. Swali: Je, ni kweli hakuna hata kipaumbele kimoja katika waraka huo kinachotufaa Watanzania? Swali hili limekuwa lininisumbua sana! Pili, Prof Lipumba aliulaani sana huo waraka lakini Rev Mtikila alipowahamasisha wanakanisa wake wasipige kura 2010 aliunga mkono! Je, kweli akili zinatutosha sisi Watz?
 
Mtu wa pwani
Baba wa Taifa mwl Nyerere angekuwepo kingunge asingekuwa anakusanya kusanya vikodi ,kodi pale ubungo, PInda !!..... pinda !!! tusomeeee basi hiyo ripoti ya kituo cha basi cha ubungo

Pinda hawezi kusoma au kutoa hiyo report, hiyo ndiyo imetoka. "Pinda! unataka dhalilisha wazee!!!?". kwanza hiyo report Kingunge atakuwa kishaiona na kamshauri rais wasiitoe kwa manufaa ya siasa za CCM. Unatarajia nini?, Kingunge kama angejua kuna bomu linakuja asingewavamia Kina Kilaini na kutaka wamwombe radhi kwa kumwita fisadi. Alikuwa anasubiri matokeo ya report kwanza ndiyo awavae. Hiyo report sahau, mtaona mabadiliko kimya kimya pale Ubungo.
 
This guy is just too old to be taken seriously. In fact he needs to undergo a psychiatric evaluation to determine his mental state.
 
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu
Sasa kama umemuelewa ebu tueleze tatizo analoliona kwenye Waraka wa Wakatoliki ni ipi?Wakatoliki wanawaelimisha waumini wao mambo mengi pamoja na namna ya kuwatambua Viongozi waadilifu,tatizo liko wapi?Somo la Civics linafundishwa mashuleni hapo vipi unajua hiyo?Si chama cha siasa tu ndio kina jukumu la kuwafundisha wananchi juu ya uadilifu wa Viongozi hata wewe ni jukumu lako.Viongozi wa Dini watawaongoza je waumini wanaonyonywa na masikini wa kutupwa bila kuwaepusha na unyanyaji huu?Upo hapo fafanua basi uelewa wako.
 
Mzee Kingunge ni hypocrite. Nasema hivyo kwa sababu kwenye mambo ambayo ni ya msingi kama vile ufisadi na swala la mahakama ya kadhi ambalo hasa ndio chimbuko halisi ya waraka huu unaopigiwa sana kelele hasemi kitu. Hivi kweli kuna swala linatishia kugawa nchi kama ufisadi, IOC na mahakama ya kadhi hapa nchini? Wakati tume ya Christian Proffesionals of Tanzania ( waasisi wa waraka wa wakatoliki) walipokwenda kuwaelezea wabunge Dodoma athari za IOC na mahakama ya kadhi Kingunge alikuwa usingizini? Anataka kutwambia hakujua kilichokuwa kinaendelea pale Dodoma au anagwaya kwa vile mambo aliyoweka kwenye ilani ya CCM 2005 matokeo yake ndio hayo!! AJILAUMU mwenyewe kwa kuwa myopic kwenye maswala ya kitaifa.
 
Wanandugu poleni na mfadhaiko wa baba yetu ama babuuuuuuuuuuuuu
najua wengi tunaweza shindana nae kimwili lakini jana huyu babu nimemwona katika ulimwengu wa kiroho ameshachukuliwa kabisa kabisa na anaitaji kutolewa mabondeni...sasa basi huyu babu umri umeenda na kama anaitaji kusawazisha maisha yake aje amkpokee yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yake....ndipo atakapotolewa misukule yake....huyu sie yeye jamani.....tunaemjua yule kingunge wa kusapoti maaharamia a.k.a MAFISADI aaaaahhh hapana huuu ni msukule jamani sasa basi labda kama wewe ni ndugu ama jamaa ama rafiki mkaribishe kwenye kanisa lolote la kiroho ...ama kama yuko karibu na ubungo aje KANISA MOJA UNATOLEWA MISUKULE LIVE....AWE PINDA..KINGUNGE...UKIKANYAGA TU KAMA UMECHUKULIWA MSUKULE ....UNAKWENDA NA MAJI....NJOO UMLETE MZEE WETU AMALIZE MAISHA YAKE KWA UPENDO...LABDA NIWAPE USHUHUDA KIDOGO

KAMA UNA DISHI AMA UMESHAWAHI KUSIKIA MAHUBIRI YA PASTOR TD
JOSHUA

MWEZI WA NNE ALIHUBIRI LIVE KWENYE TV NA KUTOA MAONI KWA JAMAA YOYOTE AMA NDUGU WA KARIBU WA MICHAEL JACKSON WAJARIBU KUMHIMIZA AJE NIGERIA KUOMBEWA .....KUNANGUVU ZA GIZA ZINAMSUMBUA SANA...U KNOW WAT LAST AKAPIGIWA SIMU SIKU MOJA NA KUAMBIWA MICHAEL AMEJIU YUKO BUSY NA MATAYARISHO YA 50 SHOWS ENGLAND....AKAWAAAMBIA AMEMWACHIA MUNGU.....SO NI VYEMA KAMA UNAPENDA KUOKOA ROHO ZA HAWA WAZEE WETU TUWASAIDIE KWENDA MAOMBINI.....

MUNGU ATAMFUNGUANA KUJUA VILE VICENTI ANAVYOHONGWA NA WALE MAFISADI NI UCHAFU NA ZINAA....
 
Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.


Tafadhal apelekwe Hospitali ya Vichaa Milembe, Dodoma kabla hali haijazidi kuwa mbaya na akaanza kuwarushia wazalendo mawe!!! Tena Milembe ni karibu na ofisi za Chama atakaa hapo akisubiri vikao vya chama. Hivi hakuna wa kumwambia akae kimya!!!!! Ameishiwa agenda!!!
 
Swali ninalojiuliza ni kwa nini JK amekuwa kimya sana juu ya swala hili?ni kwa nini Pinda aliposema kule bungeni hakutoa kauli nyooofu?bila shaka watanzania wenzangu kuna jambo hapa linalofichwa hapa na serikali yetu....Hii ni dalili tosha ya aina ya viongozi tulionao
1) Huficha ukweli
2) Kila anayejitahidi kuleta mabadiliko hupigwa vita
3) Njia rahisi kwao ya kutatua matatizo ni kuyakwepa
 
Mzee Kingunge ni hypocrite. Nasema hivyo kwa sababu kwenye mambo ambayo ni ya msingi kama vile ufisadi na swala la mahakama ya kadhi ambalo hasa ndio chimbuko halisi ya waraka huu unaopigiwa sana kelele hasemi kitu. Hivi kweli kuna swala linatishia kugawa nchi kama ufisadi, IOC na mahakama ya kadhi hapa nchini? Wakati tume ya Christian Proffesionals of Tanzania ( waasisi wa waraka wa wakatoliki) walipokwenda kuwaelezea wabunge Dodoma athari za IOC na mahakama ya kadhi Kingunge alikuwa usingizini? Anataka kutwambia hakujua kilichokuwa kinaendelea pale Dodoma au anagwaya kwa vile mambo aliyoweka kwenye ilani ya CCM 2005 matokeo yake ndio hayo!! AJILAUMU mwenyewe kwa kuwa myopic kwenye maswala ya kitaifa.

ASANTE SANA MKUU KWA INPUT HII..you real touches what i wanted to say..waraka wa katoliki safi sana tena mi nadhani wangeuweka katika kilugha cha makabila yote ya tanzania ili watu hata kule kwetu tanangozi wasome...Ufisadi ndo isshue ya msingi hapa na ndio threat kwa umoja na ustawi wa nchi yeye anakazania waraka ..he cannot talk about ufisadi maana mihela ya ubungo anayokusanya si midogo ...
 
Mzee Kingunge ni hypocrite. Hivi kweli kuna swala linatishia kugawa nchi kama ufisadi, IOC na mahakama ya kadhi hapa nchini? AJILAUMU mwenyewe kwa kuwa myopic kwenye maswala ya kitaifa.

Ninakubaliana na wewe kuwa Kigunge ni hypocrite. Katika hali ya kawaida hautegemei Kigunge auone waraka wa Katoriki ambao umetolewa kuelimisha umma wa Watanzania kama ilivyo matakwa ya Katiba ibara ya 18 unashambuliwa lakini suala la mahakama ya kadhi la kidini kutaka kuingizwa kwenye katiba alikaa kimya. Tena yeye alihusika kuingiza udini kwenye ilani yao kwa manufaa ya kisiasa ya CCM. Tena hajafungua kinywa chake juu ya OIC. Kwa hiyo Kigunge, Makwaia, Seif, Lipumba na wengine wana ajenda yao ya siri ambayo watanzania hatutathubutu kuwaachia kuitimiza kwa kuvunja katiba na kuleta udini.
 
Swali ninalojiuliza ni kwa nini JK amekuwa kimya sana juu ya swala hili?ni kwa nini Pinda aliposema kule bungeni hakutoa kauli nyooofu?bila shaka watanzania wenzangu kuna jambo hapa linalofichwa hapa na serikali yetu....Hii ni dalili tosha ya aina ya viongozi tulionao
1) Huficha ukweli
2) Kila anayejitahidi kuleta mabadiliko hupigwa vita
3) Njia rahisi kwao ya kutatua matatizo ni kuyakwepa

swali linakuja kwamba watakwepa kusema ukweli hadi lini?? Napata kichefuchefu kuwa na viongozi kama tulionao sasa. mbona OIC, Kadhi hili lizee halikusema kitu lakini issue ya waraka linakuja juu, pumbafu kabisa...aha......anakera.
 
Kingunge kama Mtanzania mwengine (bila kujali umri wake) ana haki ya kutoa maoni yake na kushawishi kwa hoja kile anachoamini (in this case yuko kinyume na Kanisa kuhusu waraka). Haki hiyo ya kutoa maoni yake haizeeki au kupungua kwa kadiri mtu anavyoingia uzee. Na kimsingi haipimiki kwa umri, usomi, n.k

Ni vizuri basi tukahukumu hoja zake na kuzionesha jinsi gani zilivyo dhaifu bila ulazima wa kuziunganisha hoja hizo na umri wake kwani kwa kufanya hivyo tunatengeneza ubaguzi wa kiumri - kuwa wazee hawatakiwi kutoa maoni yao!

Na vile vile wale ambao ni wazee wasitumie uzee wao kufikiri ya kwamba ndio kunawapa haki zaidi ya kutoa maoni au kwa sababu ya umri basi maoni yao yana nguvu zaidi au yasikilizwe zaidi. Kila maoni au hoja ipimwe kwa ushahidi wake wa kimantiki na mvuto wake wa vithibitisho vyake.
 
Licha ya kwamba nakubaliana na assessment kwamba Kingunge amedhihirisha amechoka na amechanganyikiwa, nakubaliana na msimamo kwamba dini zisijiingize katika siasa.

Hata kama kimantiki, Waraka wa Wakatoliki unazungumzia uraia mwema na jinsi wananchi watakavyoweza kupata viongozi bora, ukweli upo pale pale kwamba "muwamba ngozi huvutia kwake"; na kama kila dhehebu litatoa waraka kwa waumini wake mwishowe tutakuwa na wawakilishi wa kidhehebu.

Serikali inapaswa kutoa mwongozo kwamba siasa zisiwe jambo la mahubiri katika vikao vya dini ama katika nyaraka zao. Hilo halitakuwa jambo jipya. Hata Katiba ya Tanzania, Ibara 19 inatamka dini itakuwa sio shughuli za Serikali. Kwa hiyo dini zisiingilie katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali.
 
Binafsi nimemuelewa anacho kiongelea huyu ni kiongozi wa nchi na ni miongoni mwa walezi waliobakia ,amesha ona athari za kanisa watakazokuja leta huko usoni ,nafikiri busara zake na maoni yake we should take into very very good consideration. la sio hivyo tutakuja jikuta tunaingia katika matatizo ya Udini na ukabila ambao unafuatana na udini.
 
Last edited:
kingunge amefulia,

anazungumzia kutaka kufukuzwa shule wakati amasoma msimbazi,,,kwamba mapadri walikuwa wanamwonea. ameona alitoe hili leo baada ya kuona huo waraka???.

ni kweli huyu babu anahaki ya kutoa maoni kama watanzania wengine. sijausoma huo waraka , na sitaki kuzungumzia uhalali/ si halali wake. isipokuwa nadhani kwakutumia nafasi yake, ningetarajia kingunge angetafuta mkutano na hao watoaji wa huo waraka, akaaelimisha au kutoa dukuduku zake juu ya athari za huo waraka kwa watanzzania kwa ujumla. huenda hawa wenye waraka wangelielewa na kufuta huo waraka, lakini waraka kama huo inadaiwa na waandaaji kuwa ulishatolewa mwaka 1995, kingunge hakusema. halafu leo kwa kujiita yeye ni mwona mbali na amekula chumvi nyingi, anaibuka tu bungeni na kuwashauri wenye waraka waufute, ktk hali ya kawaida hawawezi kumwelewa. kwa upande wa serikali, nakubaliana na namna wanavyolichukulia hilo suala, kama kweli wanachokisema ndiyo kinafanyika,- kuchunguza na kufanya majadiliano na watoa waraka- hilo ni jema. kingunge anajiweka ktk wakati mgumu. leo anasema dini zinachochea ubinafsi na kuligawa taifa- ivi hiyo kauli mtanzania wa kawaida anaielewaje??. ninamhurumia kwa kuwa siku za uzee wake zinakuwa ngumu. kama kweli kanisa ni tishio, basi serikali iamuru kuwa waraka huo usionekane mtaani. kama kweli ni wa uchochezi, basi utafutika tu, namna nyingine utaendelea kuwepo; tazama komandoo wa shida-dr. salmin amour juma, aliamuru gazeti la majira lisiingie zanzibar, kuwa ni la kichochezi, alifanikiwa???, je leo hii si tunasoma majira zanzibar???.
 
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu
SAIDSABKE
Nadhani wewe ndiye uliyepotoka kuliko huyu mzee.

Waraka wa Waroman naomba uutafute na uusome na hapo ndipo utakuja kugundua kuwa huyu mzee ameishiwa fikra na hoja pia.

Watu wanamwita fisadi kwa vile waraka ule umebeba mahudhui ya kushauri na kukataza watu wasiwachague mafisadi, sasa kama yeye anapinga hilo unataka aitwe nani kama sio fisadi? Mwizi ukimgusa tu anakuja juu.

Anaongelea sana maadili ya Mwalimu Nyerere, lakini anasahau kuwa waraka ule umezungumzia hayo hayo, sasa utata wake uko wapi? Lazima tuwe wakweli hapa bila kuangalia umetoka kwenye dhehebu gani, zaidi ni kuangalia masirahi ya taifa kwanza.

Kama anataka mambo ya dini yasichanganywe kwenye siasa basi agepinga suala la Mahakama ya kadhi maana hili liko kwenye hassard za bnuge ambalo linalipiwa kodi na hata wapagani ambao hawana dini, lakini huu waraka haujapelekwa bungeni na ni kama vipeperushi tu vingine, ndio maana walimwambia kuwa anashambulia bila kuusoma.

Hana hoja, tuache ushabiki wa kinafiki bila kuwa na machaganuo halisia.

Waraka ni mzuri na wala hauna dosari zozote, na pia Wakatoliki hawajaomba pesa bungeni za kuchapishia machapisho ya waraka huu, wametumia pesa zao.

Kgwamaka
 
Nilijaribu kumsikiliza kwa makini sana mzee wangu Kingunge wakati anajibu hoja mbali mbali zilizoletwa na viongozi wa dini na wananchi wengine kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki. Sikuona sehemu anayosema kuwa waraka huo ni mbaya, lakini aliendelea kudai kuwa waraka huo utatugawa. Inawezekana mzee Kingunge ana siri nzito ambayo hatuijui.

Kwa jinsi nilivyoelewa mimi ni kuwa, waraka huo haujawalenga waumini wa dini moja tu, ni waraka unaotoa mwelekeo wa kuwachagua viongozi bora ktk nafasi mbali mbali za siasa. Kwa mtizamo wangu, mimi nilidhani kuwa waraka huo utaongeza nguvu kubwa sana pale ambapo CCM imeishia.

CCM ina nia ya kupitisha utaratibu wa kuwashirikisha wanachama wake wote kuwachagua viongozi watakaogombea nafasi za Udiwani na Ubunge. Hatua hii imefikiwa baada ya kuonekana kuwa kuna malalamiko mengi sana, na hasa pale mtu waliyemtaka wanachama wengi kutokupitishwa jina lake.

Maana ya zoezi hili ni kutaka kuwaengua wale wajanja waliochukua kadi za papo kwa papo, na kutumia pesa zao kuwarubuni viongozi wachache wawachague. Kuna sheria inakuja, ambayo inamtaka mgombea yeyote kutoka chama chochote cha siasa kufanyiwa mahesabu ya gharama alizozitumia ktk uchaguzi. Sasa, waraka unapokuja, unaongeza maana ya malengo halisi ya kupambana na kuzuia kupata "bora viongozi" badala ya "viongozi bora".

Nadhani mzee Kingunge angetufafanulia vizuri, ni kwa namna gani waraka huo utatuletea matatizo? Akumbuke kuwa waraka huo umewashirikisha watu mbali mbali ikiwa ni pamoja na wawakilishi toka vyama vya siasa na madhehebu mengine ya dini hapa nchini.
 
Nitaendelea kuungana na wale wote wanaoona kuwa mzee Kingunge ameanza kuchanganyikiwa mpaka atakapotuambia TATIZO la huo WARAKA ni nini, na utatuletea matatizo kivipi? Huyu mzee ana heshima kubwa sana ndani ya chama cha mapinduzi, heshima hiyo kaijenga kwa muda mrefu sana, nitasikitika sana kama ataipoteza wakati huu wa "lala salama", kwani hatakuwa na muda wa kurekebisha tena.

Mitizamo ya mzee Kingunge ya hivi karibuni imeanza kututia wasi wasi mkubwa ambao unatuachia maswali mengi sana kuliko majibu.
 
Malaria Sugu, ni vizuri ukausome waraka huo kwanza badala ya kuja na hisia. Kama wote tutakuwa tunajenga hoja kwa kuhisia, basi kuna hatari ya kufanya maamuzi ya kihisia.

Nimeusoma waraka huo, sikumbuki kusoma kipengele kinachosema maneno hayo. Mimi naona waraka huo hauna matatizo kwa mtu safi anayetaka kugombea nafasi za uongozi ktk duru za kisiasa. Waraka unamtaka Mtanzania kuchagua kiongozi ambaye ni mwadilifu bila kujali dini yake, kabila lake, rangi yake wala jinsia yake, sasa tatizo liko wapi? Kama tukibadilisha mtizamo na kuangalia UJUMBE uliobebwa ktk WARAKA huo bila kupoteza muda wa kuangalia NANI ameleta UJUMBE huo, nina imani tutakuwa tunawatendea haki kubwa sana watanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom