Kingunge amechanganyikiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingunge amechanganyikiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzeePunch, Aug 13, 2009.

 1. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.
   
 2. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Miaka mingi huyu Mzee wetu;) Alikuwa mtu wa kukaanga maneno tu kwa ajili ya sekretarieti:D ya CCM
  Kwanini usichanganyikiwe?

  Ameyatafuna weee... hivi sasa, kwa maoni yangu, anatapika...haelewi kama bado yupo kwenye era hizo zilizopita... au yupo kwenye ulingo mpya!

  Propaganda ni ngumu siku hizi! Labda anaichanganya na waraka wa enzi hizo...
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani tumsaidie mzee wetu huyu kwa kumshauri astaafu; kwa kweli hali aliyofikia sasa ni ile ya kukaa nursing home au kupata palliative care tu!!!

  Lazima akubali kwamba kila jambo na wakati wake, na kila binadamu ana life span... is has already passed the productive stage na sasa anaelekea destructive stage

  I still dont know why media inaendelea kumpa nafasi wakati wakijua wazi kwamba inaweza kuwa counter-productive kwa kingunge na CCM
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi nadhani kachanganikiwa.by the way anatumwa na nani kuzungumza haya?hivi huyu si ndio msgauri wa rais wa mambo ya siasa sijui au?kazi ipo mwaka huu
   
 5. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee kachanganyikiwa siku nyingi anadhani bado tupo kwenye zama za zidumu fikra za mwenyekiti. Viongozi wa dini wana nafasi yao katika uongozi wa nchi. Wananchi waachwe wao wanajua lipi zuri lipi baya.
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kingunge atangaza upya vita na Katoliki

  *ATAKA WAMUOMBE RADHI, WASAJILI CHAMA CHA SIASA

  Waandishi Wetu

  MWANASIASA Mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, ameendelea kuung'ang'ania waraka wa Kanisa Katoliki na sasa amelitaka kanisa hilo limwombe radhi kwa kumwita fisadi alipoupinga bungeni.

  Waraka huo uliotolewa Machi mwaka huu, ulilenga kuwapa mwongozo waumini wa Kanisa Katoliki wa namna ya kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao, vipaumbele vya kitaifa na aina ya kiongozi anayefaa kuchaguliwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, Kingunge alisema alishangaa kusikia kanisa hilo likisema wanaohofia waraka huo ni mafisadi baada ya yeye (Kingunge) kutoa angalizo bungeni katika Mkutano wa 16 uliomalizika Julai 31 mwaka huu.

  "Maaskofu wamenisikitisha sana katika hili. Hatuwezi tukakubali nchi ikapelekwa wanavyotaka wao, tunaomba waache," alisema Kingunge na kuongeza:

  "Nashangaa, askofu mzima akazungumza na kuniita fisadi, hiyo ni dhambi. Askofu huyo akaungame. Mimi sipendi neno fisadi ni afadhali kama rushwa iitwe rushwa".

  Hata hivyo, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Method Kilaini jana alikataa kujibu kauli hiyo ya Kingunge akisema hataki kulumbana na mkongwe huyo wa siasa.

  "Sitaki kulumbana naye, mzee wa watu ni mzee wa watu tu, hivyo sitaki kuendeleza malumbano naye,"alisema Kilaini.


  Kwa mujibu wa Kingunge, viongozi wa Kanisa Katoliki wamemkejeli na kumtukana kuwa hajasoma kwani anaamini kwamba aliusoma waraka huo vizuri na kuulewa kwa kina kabla hajatoa kauli hiyo.

  'Niliusoma vizuri na kuelewa. Hivi nitashindwa kuelewa walichoandika, nimesoma maandiko ya dini ya Kiislam, Kihindu na nyingine, siwezi kushindwa kusoma na kuelewa waraka huu." alisema Kingunge juzi alipokuwa akihojiwa na kituo cha Channel 10 na kuongeza:

  "Sikutaka kuingia katika maudhui, maana nikiingia katika maudhui ningelumbana nao kwamba dini inakuaje na ilani, ilani inapaswa kuandaliwa na vyama vya siasa tu na si vinginevyo," alisisitiza.

  Kingunge alisema ni vizuri kanisa likaelewa kuwa lenyewe sio chama cha siasa na kwamba, halina uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi.

  Alifafanua kwamba, wakati anazungumzia waraka huo bungeni hakuwa anataka uhasama na kanisa kwa kuwa anaheshimu imani, ila alikuwa akitoa angalizo kwa kuwa dini haiongozi nchi kama serikali.

  "Ukiona vyaelea, jua vimeundwa" angekuwepo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hapa, kanisa hilo lisingethubutu kuandaa waraka huo, mimi pia ni mkongwe, hivyo hakuna yeyote ambaye anaweza kusimama na mimi kuhusu historia ya nchi hii.

  Nataka niwaambie kwamba, tunajua mambo ya Kanisa Katoliki, lakini kwa bahati mbaya mwalimu hayupo,"alisema.

  Kingunge aliendelea kulishambulia kanisa hilo akidai kuwa linataka kuwatoa Watanzania katika utamaduni wao na kulishauri kuunda chama cha siasa kama linaona ni vyema.

  Alisisitiza kuwa dini si chombo cha kuunganisha watu, bali kuwatenganisha ndiyo maana kila mtu ana dini yake, lakini serikali ni moja, hivyo nchi yenye dini nyingi haiwezi kuunganishwa na dini bali siasa.

  Katika malumbano hayo yaliyodumu kwa muda sasa, kanisa liliutetea waraka huo likisema kuwa sio mara ya kwanza kuutoa kwa waumini wake.

  Lilisema huu umekuwa utaratibu wa kanisa hilo tangu mwaka 1995 ukiwa na lengo la kuwaelimisha waumini wake kuhusu namna ya kutekeleza haki yao ya kupiga kura.


  Habari hii imeandaliwa na Boniface Meena, Ramadhan Semtawa na Hussein Kauli
   
 8. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nafikiri niliwahi kushauri humu kazi hiyo apewe MMKJJ,kwani bado kijana:D just a jest

  MTM,
  Mzee Punch naye kaleta hii bila mpangilio!
  Hayo maneno , mpangilio ndio ya kushangaza? Mzee Punch kashindwa kuleta hayo maneno yenye mpangilio na mantiki...kinanishangaza pale napoanza kushangaa mtu aliyechanganyikiwa!(kingunge):D

  Nimechanganyikiwa nitarudi punde....
   
 9. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Ni yapi aliyoyasema...hakuna nukuu?
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Kwa umri wake alitakiwa awe amestaafu na kupumzika Kijijini, busara zake tunazikubali lakini hatakuwa na uwezo wa kupambana majukwaani.
   
 11. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #11
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kweli mzee anazeeka vibaya sana, eti anasema dini inaleta ubinafsi anavyodai yeye eti kwa sababu kila mtu ana dini yake so muda wa kwenda kusali/kuswali ukifika kila mtu anaenda kwenye dhehebu lake. kweli kazi ipo.
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  huyu mzee mpuuzi sana.kanaongea tu,
   
 13. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  masikini kingunge hoii anakataa kuitwa fisadi je ishu ya ubungo bus terminal anaiweka wapi namuonea huruma sababu ikitokea rais mpya ambaye atachaguliwa kwa msingi wa muongozo mzuri wa kanisa katoliki watu kama kingunge ndo wa kwanza kipelekwa segerea kwa ufisadi , ushirikina na unafiki wa siku nyingi thats why anaogopa kweli kweli , nawaomba tu watz wenzangu tuchague viongozi bora bila ushabikli wainyooshe hii nnchi na watu wa fitna kama mzee huyu wakomeshwe.
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wazee kama huyu walitakiwa wawekwe jumba-la-makumbusho pale k/nyama ili tuwe tunalipia kuwasikiliza na mitizamo yao ya ''enzi-za chama-na serikali''.watoto wetu wangefaulu vizuri tu
   
 15. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kingunge yuko sawa ila wenye ajenda za siri ndio wanaotaka kumchafua

  anasema kama mwalimu angedai uhuru kwa kutumia biblia au waislamu kwa kutumia quraan pasingepatikana umoja wa kitaifa

  nchi zenye dini nyingi dini haiwezi kutumika kama chombo cha kuwaunganisha WATU maana kila imani inaamini kivyake

  mambo ya ilani ni mambo ya vyama vya siasa wakubali wakatoliki wamechemsha
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mzee kwani hujui Kingunge ni fisadi papa?
  Uliza mapato ya pale Ubungo familia yake inakusanya kiasi gani report Mzee Pinda ameipindisha na kuikalia kaona uozo mtupu.
  Uliza maegesho mjini wewe bana wewe Nyamaza bwana wamepigwa Ikulu hawa janja yao tumewashtukia.
   
 17. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusimulaumu, ametuletea changamoto nzuri sana kwani wapiga kura walikuwa hawaelewi sasa hivi ndo watu watatafuta wapi uliko kusudi wasome na kuuelewa. Ni vizuri tena aendelee kufanya hivi pia na Maaskofu pia wajibu ndo watu waelewe kilichoandikwa humo ndani. Mwacheni aongee ni CHANGAMOTO NZURI SANA, watanzania hatusomi vitabu sasa ni wakati wa kutafuta waraka na kuusoma na kuuelewa.
   
 18. m

  mwalimu Jr. Member

  #18
  Aug 13, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Repent Kingunge now tells Catholics

  UNLIKE the hypocrites and demagogues in CCM and the parliament I am for the first time, fully behind Mzee Kingunge and now more ever than before believe in his sound judgement and admirable foresight.

  Countrymen, let us pull back, and take a looong look at the mishaps that have deliberately or accidentally befell our people and land because of SOME VERY CLERGY MEN who think they are anointed by God to be the choosers of our leaders.

  I say this because I have never seen anywhere in the world where a president, chairman of political party and the rulling party in fact being subordinated to the Church or any other religion for that matter in a true democractic country.

  There is no way in Africa where we can let sheikhs or bishops HAVE THE LAST say in how the government decides and operates and at the same time GUARD PEACE AND UNITY in a country?

  Wherever you see such thing happen, that is, a leader being led by those whom he is leading then the leader is weak and useless.

  For those CCM members and parliamentarians who believe there is nothing wrong with the recent position adopted by the Catholcs one thing is for sure -they are demagogues. They believe they can hunt with the foxes and run with the hare at the same time. Something neigh impossible....at least for me!

  If we let the church preach politics then what will political parties do? Become jobless? And which religion will ever back a man from a rival sect or faith order ? Will not things be like at TBC- a national broadcaster who is competing with religious station and actually is outdoing even the private faith station in spreading the word of God? Directionless? Overzealous Board members and Management at TBC ? Nowdays, after the 7 a.m. news the TBC has 5-7 minutes dedicated to a single religion announcements/advertisements. What is this Mr. Director? After the announcement expect one or two gospel songs? What an entertainment in a national broadcasting Organ ?

  Watanzania katika miaka hii ya vituko na maajabu ni kwamba mwizi mkubwa ndiye anayetaka kuwa Mkuu wa Polisi ili akiiba pasiwe na wa kumshuku; mzinzi mkubwa ndiye anayetaka kuwa mwalimu wa shule au chuo chenye wasichana wengi ili afanye biashara yake; wajinga, mabahili, wabinafsi wakubwa na mabaradhuli wasiokuwa na nia yoyote ya kumsaidia mwananchi wa kawaida wanakimbilia siasa ili kudanganya kuwa wana kitu wanachotoa; malaya mkubwa hutaka kuwa na kazi au cheo chenye heshima ili umalaya wake usijulikane; na ndivyo ilivyo kwa wauaji, wavunja nchi na wasambaratisha jamii wakubwa nao hutaka kuwa viongozi wa dini ili wanapofanya kazi yao ya kuikokota jamii kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe pasiwe na anayewashuku. Tujihadhari, tujihadhari, tujihadhari au tutakuja lia na kusaga meno kwa miaka mingi katika muda mrupi tu kutoka sasa!
   
 19. m

  mwalimu Jr. Member

  #19
  Aug 13, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  Tatizo la kufikiri kwa moyo badala ya akili ndilo linalowatatiza wengi 'wanaoharisha katika blogi na mitandao kama hii. Chukueni muda sio tu wa kujiona mna akili na mnaweza kusema lolote bali kubwa zaidi kulipima jambo kwa faida au hasara zake za leo na k esho- Mwalinu Jr. na ushauri wa Buuure!
   
 20. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ninaloliona ni kuwa Mzee Kingunge kweli apumzishwe na masuala ya nchi hii kwani haoni kina KK sasa wamejipumzikia? Kufikia hatua ya kulumbana na Maaskofu si ishara nzuri kwake. Wale maaskofu walikuwa na haki ya kusema walilosema kwani nao ni sehemu ya jamii ya Tanzania. Hakika ni kwenye tafsiri tu ndio tutaona udhaifu wa kila mmoja katika jamii. Baada ya kuona Taifa linaenda kusiko, Wakatoliki wakaona ni vema turudi kwenye mstari watu waweze kuchambua mapema mchele na makapi. Makapi yameanza kuonekana.
   
Loading...