Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Mkuu Mkandara, Mpango wa Kuhamasisha Huduma ya Kichungaji si waraka kwa wananchi wote. Ni waraka kwa waumini wa Kanisa kuhusiana na namna wanavyoweza kushiriki katika kupata viongozi wenye kuweza kusaidia jamii nzima. Waraka huo kwa wakristu, unasema hivi "Programu yetu ya kulihamasisha Kanisa kutekeleza wito wa kichungaji katika mambo ya kijamii ni kuwatia moyo waamini wote kutambua na kukubali wito wao wa Kikristo, wito wa kuwapelekea watu habari njema ya Yesu katika mambo ya kijamii na ya kitaifa. Kutakatifuza malimwengu, kuifanya nchi yetu na watu wetu kuishi pamoja huku manufaa ya kila mmoja yakiwa yanatimizwa: kupata huduma msingi za maisha na kuheshimiwa utu wa kila mmoja. Hapa maslahi na manufaa ya wote na ya kila mmoja katika jamii yanapaswa kuzingatiwa. Huu ni wajibu wa kila mmoja."Mchukia Ufisadi,
Mkuu wangu nimekwisha sema sipendi kujihusisha na ubishi wa kidini hata kidogo lakini wazidi kunivuta tu ili mradi niingie upate kufurahi.. Ebu wewe mwenyewe soma tena huo waraka kisha nambie kuna sehemu ngapi wamenukuu Biblia na mafundisho yake ktk hujenga hoja nzima ya waraka huu...Kwanza tazama kichwa cha habari kinasema Mpango wa kuhamasisha HUDUMA YA KIUCHUNGAJI.. sasa ukisha elewa kwa nini Mkandara hakuwa mkristu ndipo utaelewa kwamba Mkandara hakubaliani na huduma za Kiuchungaji pamoja na kwamba lengo lake ni kutufikisha peponi..
Siku zote ktk waraka huru aya na sura hutumika kama mifano na sii sisitizo la waraka mzima, unless waraka huo umelenga waumini wake..
Mbali na hili nachokipinga mimi sio substance ya waraka mzima, isipokuwa uwakilishi wa waraka kama navyoikubali Biblia bila kuukubali uwakilishi wa kanisa Katoliki. Ukinielewa hapo tutakuwa msitari mmoja
Mkuu, inawezekana kabisa waraka kama huu usiwafae waumini wa madhehebu au imani nyingine yoyote isiyo ya kikristu. Ila kama mafundisho yoyote ya dini yoyote yalivyo wa waumini wake, waraka huu ni applicable tu kwa wakristu waliokusudiwa. Inaendelea kusisitizwa pia kuwamaslahi na manufaa ya wote ni lazima yazingatiwe (bila ubaguzi). Kama kuna tatizo tuelimishane ili tupate ufahamu zaidi. Maana naanza kuona matamanio ya watu kuomba Makanisa yaache kuhubiri.