Kingunge amechanganyikiwa?

Huyu Babu ajinyamazie tu mdomo utamponza ye andelee kula hela ya ubungo stand halafu mbona Boss wao kakaa kimya JK bana kila mara anachukua muda mrefu kureact na national issue labda arudi vatican akapate ushauri kwa Papa wakicheza chess
 
Attachments

  • jk.bmp
    70.4 KB · Views: 64
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu

SaidiSabke,
Taratibu ndugu. Hawa maaskofu na masheikh ni viongozi wa kiroho.Lakini kumbuka hakuna Roho inayoelea hewani, zote ziko kwenye miili. Hivyo ili utengeneze maisha ya kiroho, lazima uujali mwili. Hii ndio maana mchango wa viongozi wa dini katika siasa ni wa muhimu sana na wa kuheshimiwa. Dini katu haiwezi kutengana na siasa kama mwili usivyotengana na roho. Utengano huu ukitokea, cheo kinabadilika kutoka binadamu kuwa marehemu.
 
Mzee wetu amefikia mahali ambapo hekima inaisha na kurudia utoto. Vile vile anaanza kupoteza kumbukumbu bila kujua kuwa sasa ni wakati wa mabadiliko na sisiem haishiki hatamu tena. Hivyo anashindwa kuhimili wimbi la mabadiliko kuwa watanzania wanahitaji mwongozo nje ya CCM ili kuwa na uelewa mzuri wa mahitaji ya taifa. Yeye anataka CCM iendelee kuwadanganya watanzania.
 
TUNACHOTAKIWA Watanzania wote kwa pamoja ni kuamua je, tunachotaka kuweka mbele ni UTANZANIA na UAFRIKA wetu au kabila, dini, rangi, jinsia, usomi, vyeo, kazi, mali au ukoo wetu ?

Kama tumeamua kumpa MUNGU kilicho cha Kaizari sawa!!!

Kama tumeamua kwamba mpanda fahali wawili hawezi kupasuka msamba basi tuendelee na kupanda fahali wawili!

Kama tumeamua kwamba kujenga ufa ni kwa kuongeza ufa mwingine tufanye hivyo!

Kama tumeamua kwamba gauni au suruali mpya hupatikana kwa kushona kiraka juu ya kraka tuendelee vivyo hivyo!

Kama tumeamua kwamba akumulikaye mchana usiku hatakuchoma bali atakumwagia maji ya baridi kwanini tuogope maji ya baridi?

Kama akili ni nywele na kila askofu na sheikh ana mvi na sio nywele nyeusi na tumezipenda mvi zisizo na hekima wala busara kwanini tusizipende!!!

Kama tunadhani fataki hawezi kuwepo kwenye majengo ya makanisa na misikiti tuendelee kuruhusu hata wenda nusu uchi kuja kuswali.

Kama hatujui asiyekutaka au anayekutakia baya hawezi kukwambia toka au hawezi bayana bin bayana kukulaani ngoja asubihi ipishe mchana na jioni ipishe usiku.
 
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu

Jana kuna mtu alikwambia hivi:

Kingunge+Makwaia+Saidsabke=Udini

Nafikiri hakukosea.....vichwa vyenu naona vinawaza maovu or negative things tu.....mko very low you can't think positively!
 
Kweli mzee anazeeka vibaya sana, eti anasema dini inaleta ubinafsi anavyodai yeye eti kwa sababu kila mtu ana dini yake so muda wa kwenda kusali/kuswali ukifika kila mtu anaenda kwenye dhehebu lake. kweli kazi ipo.

Kwa kiigereza Mzee Kingunge " is chasing his own tail!" Yeye ndiye alianzisha zogo la Mahakama ya Kadhi katika ilani ya CCM 2005. Kama mtu ukienda kwa undani kuona kwa nini waraka wa uchaguzi wa kanisa katoliki chimbuko lake hasa ni hii ilani ya CCM kuhusu Mahakama ya Kadhi na mambo ya IOC. Kingunge anasema Kanisa litubu kwa kuandika waraka wakati yeye ndiye chimbuko na waraka huu kwa kuingiza mambo ya dini kwenye siasa! Nani wa kubutu kama sio yeye? Alianzisha zogo hili na ajilaumu yeye mwenyewe.
 
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu

Sina uhakika una umri gani, lakini inavyoelekea wewe umechanganyikiwa zaidi kuliko huyo Kingunge.
 
Niliwahi kuwaambia mkasome kitabu kinaitwa the root of all evil. Kama hamjui vita vingi vya wenyewe kwa wenyewe vina mkono wa Roman Catholic Church na sasa Tanzania ndipo inapolekea nyie subirini. Kingunge analosema ni kweli na hajakosea hata kidogo tunahitaji watu wenye ushupavu kama huo kunyooshea kidole Tabia kama hii.

Na tukiiachie Tanzania inaelekea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe
 
Ukichangia hoja ya waraka huu na wakati huohuo unaudini utaona Kingunge, Makwaia, Said Sabke wanapoint za kuchallenge waraka huu wa katoliki. Lakini ukiusoma na kuuelwa hamna cha kupinga na hakuna hata sehemu inayoweza kuleta mgawanyiko kama Kingunge anavyodai na utaona kweli huyu Kingunge amezeeka. Kiti kingine ni kuwa huyu Kingunge na mafisadi wenzake wamezoe kuingia madarakani kwa kutumia hila za uongo na kuhonga pilau, pombe, kanga, vitenge, vocha za simu etc. sasa huu waraka unatamka wazi watu wa namna hii wasivyofaa kuchaguliwa.
 
Huyu kikongwe hajaanza leo! Nanii asiyejua ufisadi wake? angalialini Mifano michache , tuanzie Uwakala wa kukusanya mapato Ubungo Terminal. Ni hivi majuzi waziri Mkuu kaishtukia Hiyo dili ya ufisadi ambayo inaeleweka wazi kuendeshwa na familia ya kikongwe huyu!
Tu Maegesho ja City centre nayo yanaendeshwa na familia ya huyuhuyu babu naisitoshe tender alipewa kwa kutumia mchezo mchafu! kampuni hakiuwa hata imesajiliwa wakati inapewa zabuni! hebu waziri Mkuu Tuulisie na huku wanakusanya kiasi gani?
Miaka ya nyuma mwanae huyu babu alishamgonga mtu na kumuua akitioka ulevini lakini cha kustajabisha aliweza kuwekwewa dhamana na kutotewa usikiu huohuo amba ilikuwa JUMAPILI
Kwahiyo mtu kama huyu unategemea anposikia neno FISADI anajisikiaje?
Wanapodai eti dini isichanganywe na siasa wao wanategemea madhehebu ya dini yawe pale kuwapamba! madhehebu hayohayo yanajenga Hospitali, shule, vyuo, na hata miundo mbinu kama barabara na vito vya kuzalisha umeme mbona hawajakataa na kusema hiyo sio kazi za madhehebu ya dini?
Enzi za KUDUMISHA FIKRA ZA MTU hazipo tena!
Mwabieni huyo babu huu ni wakati wa yeye kucheza na wajukuu na vitukuu!
 
Kweli mzee anazeeka vibaya sana, eti anasema dini inaleta ubinafsi anavyodai yeye eti kwa sababu kila mtu ana dini yake so muda wa kwenda kusali/kuswali ukifika kila mtu anaenda kwenye dhehebu lake. kweli kazi ipo.

Maneno ya Kingunge haya hapa kama yalivyoripotiwa na gazeti la Mwananchi la leo;

Kingunge alisema ni vizuri kanisa likaelewa kuwa lenyewe sio chama cha siasa na kwamba, halina uwezo wa kuandaa ilani ya uchaguzi.

Alifafanua kwamba, wakati anazungumzia waraka huo bungeni hakuwa anataka uhasama na kanisa kwa kuwa anaheshimu imani, ila alikuwa akitoa angalizo kwa kuwa dini haiongozi nchi kama serikali.

"Ukiona vyaelea, jua vimeundwa" angekuwepo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hapa, kanisa hilo lisingethubutu kuandaa waraka huo, mimi pia ni mkongwe, hivyo hakuna yeyote ambaye anaweza kusimama na mimi kuhusu historia ya nchi hii.

Nataka niwaambie kwamba, tunajua mambo ya Kanisa Katoliki, lakini kwa bahati mbaya mwalimu hayupo,"alisema.

Kingunge aliendelea kulishambulia kanisa hilo akidai kuwa linataka kuwatoa Watanzania katika utamaduni wao na kulishauri kuunda chama cha siasa kama linaona ni vyema.

Alisisitiza kuwa dini si chombo cha kuunganisha watu, bali kuwatenganisha ndiyo maana kila mtu ana dini yake, lakini serikali ni moja, hivyo nchi yenye dini nyingi haiwezi kuunganishwa na dini bali siasa.
 
Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu

Kwani una hakika si fisadi? Dhana nzima ni kwamba anayeuchukia waraka huu unamuumiza kwa namna fulani au na wewe ndio wale wale? Makamba kaukubali kwani yeye mkatoliki. hata waziri mkuu alipotembelea stendi ya ubungo alinusa harufu ya ufisadi na kumuagiza CAG afanye kazi na imekamilika tunasubiri ripoti. Mbona suala la mahakama ya kadhi hakusema litaigawa nchi au kwa sababu haliwagusi mafisadi?

Said Sabke utafute waraka uusome then utuambie wapi waraka unazungumzia dini. Pia uelewe moja ya majukumu ya dini ni kukemea uovu pale unapoonekana. Dini zikikaa kimya hazitakuwa zinatimiza wajibu wake na wataulizwa kwa Mungu.

Mahakama ya kadhi mkasema mtahubiri misikitini waisuse CCM, lakini waraka ndio udini. Tuache ushabiki usio na mantiki
 
Jana Mzee wetu alitoa nafasi nzuri sana kwa Waandishi wetu kwa niaba ya Watanzania kumuuliza maswali mazuri na mazito ambayo pengine yangetusaidia kuelewa tamko lake lile kule Bungeni lilikuwa na maana gani. Nahisi nafasi ile haikutumika vizuri aidha kwa kuwa waandishi waliokwenda pale hawakujiandaa kwa lolote upande wao zaidi ya yale mazoea ya kwenda kuwasikiliza viongozi wetu na kesho yake kuwanukuu kwenye magazeti au Wahariri wetu waliudharau mkutano ule wakawatumaa waandishi-wanafunzi wengi.
Nasema hivyo kwa kuwa nimepitia magazeti kadhaa asubuhi hii sijaona swali zito na la maana aliloulizwa Kingunge kama vile:
1. Mahakama ya KADHI iliingiaje kwenye ILANI ya uchaguzi ya CCM 2005?
2. Waraka ule umeandaliwa na MAASKOFU au CPT?
3. Nini hasa kilichomo kwenye waraka ule ambacho ni cha KIDINI?
4. Waraka hu ni wa kwanza kutolewa na CPT?
5. Utajiri wa kupindukia walio nao baadhi ya wanasiasa unatokana na nini?
6. Utajiri wa mwanae Kinjekitile hauna uhusiano na yeye anayekataa kuwa sio FISADI
Na mengine mengi tu. Waandishi ambao sasa mnajiita MHIMILI wa NNE wa DOLA zitumieni vizuri nafasi hizi kwa niaba yetu.
 
Wild Card

EXELLENT!
 
Tehe teh kuna siri kali kati ya serikali na Kingunge, sijui ni ndondocha la ikulu likitoka mambo yatadoda. Hivi nchi gani unaweza kuta kizee kama kile kinaendelea kuongoza wat na akili zao. wale ni watu wa kukaa nyumbani na kutembelewa huku wakihojiwa nini kifanyike sehemu fulani na siyo kwenye system.

RC wamefulia point, maoni wasitoe wa mapadri wao au kujishauri wenyewe wafanyeji na issue ya kuoa wanaanza kuingilia yasiyowahusu.
 
Mwanasiasa mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru, amewajia juu baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki nchini waliodai kuwa yeye ni fisadi na kuwataka wanaodhani kuwa ni wasafi kumzidi, wajitokeze hadharani.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Kingunge alisema wakati anatoa angalizo juu ya Waraka na Ilani ya Kanisa hilo bungeni, hakuwa anatafuta ugomvi na viongozi hao wa kidini, ndiyo maana alilizungumza kwa adabu na kwa heshima ili kuepuka kuingia kwenye malumbano. Alisema alitarajia maaskofu wangetafakari angalizo lake kwa makini, lakini kwa bahati mbaya hawakufanya hivyo; badala yake wakamkejeli, wakamtukana na wengine kudiriki kumwita kuwa fisadi.

“Hawa walioniita mimi fisadi ni vyema wakaenda kuungama na kufanya toba maana wamefanya dhambi kubwa kuniita fisadi… walitaka nisihoji hiki walichofanya, hilo linawezekana wapi?

“Kama kuna hoja ni vyema waijibu, wasitutishe tunaohoji kwa kutuita mafisadi, hivi ni nani ndani ya Kanisa hilo anaweza kusimama na kusema historia yake kuwa ni msafi kuliko mimi? “Wasifikiri kama watu hatuwajui mambo yao, tunayajua, ila hatutaki kuyasema. Mimi sijaiba kitu cha mtu hata siku moja, bahati mbaya Mwalimu Nyerere (Julius) hayupo angenishuhudia,” alisema.

Mwanasiasa huyo alikwenda mbali zaidi kuwa wakati viongozi wa dini wanachambua maoni yake, kuna baadhi ya watu walitumia fedha chafu kuwahonga baadhi ili wamtukane na kumchafua mbele ya jamii.

“Najua kuna watu waliohongwa wanichafue, ila nawasikitikia zaidi waliokuwa wanatoa hizo fedha chafu, kwani mwisho wao unakuja, watasema wapi wamezitoa fedha hizo,” alisema mwanasiasa huyo bila kufafanua kwa kina suala hilo.

Kingunge ambaye kabla ya kuanza mazungumzo yake alitoa historia yake ya uongozi ndani ya chama na serikalini na namna alivyoshiriki kuijenga nchi hii tangu mwaka 1954, alisema analifahamu Kanisa Katoliki tangu enzi za Mkoloni na jinsi lilivyokuwa linatumia nguvu kuwakamata wale waliolipinga.

“Wakati nasoma Msimbazi nikiwa kidato cha pili, walitaka kunifukuza shule, kisa nilihoji sababu ya Padri Mzungu kututukana sisi wanafunzi weusi, niliepuka kufukuzwa kwa sababu Makamu Mkuu wa Shule hakuwa Mkatoliki.

“Tunakumbuka uasi wa Padri Martin Luther, ulitokana na mabavu ya Kanisa hili, walitaka kinachozalishwa katika nchi za Ulaya kipelekwe Vatican, Padri akahoji, wakataka kumkamata akawakwepa… sasa hawa wasiturudishe huko nyuma, sasa hivi hili haliwezekani ni lazima tukemee wanapokiuka misingi yetu ya kitaifa,” alisema.

Alisema yeye alitoa ushauri juu ya waraka baada ya kuusoma, kwani asingekuwa ameusoma asingezungumza bungeni. Aliwashukuru wale ambao walimuunga mkono akiwamo Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad, kuwa ni mtu makini mwenye msimamo, ndiyo maana akaupinga Waraka huo.

Kingunge alisema yeye akiwa mzee ndani ya CCM na mzee katika nchi, anapoona kuna jambo ambalo linahatarisha amani na mshikamano wa Taifa ni lazima akemee. Alisema waasisi wa Taifa hili walilijenga kwa kutumia siasa na si dini wala kabila.

“Dini haiunganishi watu, inatenganisha watu ndiyo maana waasisi wa Taifa hili wakatumia siasa,” alisema Kingunge na kusisitiza kuwa laiti Mwalimu Nyerere angekuwa hai, Kanisa lisingethubutu kutoa Waraka huo.

Alisema vyama vya siasa ndivyo vyenye kazi ya kutunga Ilani na si Kanisa, kwani halijaandikishwa kama chama cha siasa. “Watuambie hili Kanisa ni chama cha siasa au kama wana chama chao cha siasa waseme, ndiyo maana wanashauri kwenye Ilani yao kuwa Katiba ya nchi iandikwe upya.” Kingunge aliwashangaa hata viongozi wa Serikali aliosema wanashabikia waraka huo wa Kanisa.

“Hawa nawashangaa sana… hawajui CCM ilikotoka, ndio maana wanazungumza mambo wasiyoyajua, ni heri wanyamaze kuliko kiongozi mkubwa serikalini kuunga mkono waraka ule.” Alisema Kanisa hilo wanachotaka kufanya ni kurithisha watoto udini, jambo alilodai kuwa ni hatari kubwa kwa Taifa na yeye akiwa mzee, kamwe hatakubali nchi ipelekwe kwenye udini.

“Kwa kweli nimesikitika sana na jinsi maaskofu walivyonitendea, ila nitaendelea kuwaheshimu kwani wana majukumu makubwa ya kidini, ila sitakubali watupeleke kwenye udini,” alisisitiza mwanasiasa huyo.

Akichangia Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Kingunge alilitaka Kanisa Katoliki kufuta waraka na ilani lilivyovisambaza kwa maelezo kuwa vinahatarisha amani ya nchi na kuligeuza Taifa kuwa sawa na Lebanon.

Baada ya kutoa maoni hayo, Kingunge aliandamwa na wanasiasa, wanazuoni na wachambuzi wa mambo ya siasa, kwa maelezo kuwa waraka huo hauna dosari kwani ulikuwa unatoa elimu kwa waumini ya namna ya kuchagua viongozi waadilifu. Katika hali isiyotarajiwa, Kingunge alisema viongozi ndani ya CCM wamejaa ubinafsi, jambo ambalo alisema linaathiri kwa kiasi kikubwa uongozi wa nchi.

Alisema ubinafsi huo umesababisha nidhamu ndani ya CCM kushuka na ndiyo maana viongozi wa chama hicho wanajibizana hadharani. Mwanasiasa huyo mkongwe alisema chanzo cha nidhamu kushuka ni kutokana na viongozi wa chama hicho kutanguliza maslahi binafsi zaidi na kuacha kuwatumikia wananchi.

“Ukiwa mbinafsi nafasi ya kuwajali wenzako haipo, uongozi bila mizania unafuta sura ya kuwatumikia watu wengine, unakuta kiongozi anafikiri ya kwake tu… mimi nitapata nini?,” alisema.

“Kuna walioingia kwenye chama kwa malengo ya kupata vyeo, hao ni lazima wafanye mambo ya ajabu ili wapate uongozi, kwani ndilo lengo lao,” alisema. Aliongeza kuwa kushuka nidhamu kwa viongozi hao kunafanya hata vikao vya chama visiwe vya siri tena kwani ndio wako mstari wa mbele kutoa siri kwa wanahabari.

“Zamani nidhamu ilikuwepo, huwezi kusikia watu wanajibizana ovyo kama ilivyo sasa, tulikuwa tunasemana kwenye vikao zaidi, lakini leo hii nidhamu hakuna viongozi wetu wamejaa ubinafsi, hilo halipo tena,” alisema.
 
kimsingi kwa ujumla kingunge hajaona la kukosoa na wala hapingi waraka...Maana mtu ukipinga lazima useme unapinga nini,sio kupinga waraka tu bila kusema unapinga kitu gani.hasemi anapinga point zipi,na ni zipi ni za kidini.

Kwa mtu mzima unaona kabisa kwamba huyu hana la kupinga,ndo maana anakuja na hoja za kutukanwa na kuombwa msamaha.

hana sera mzee wa watu...anaendelea kuutangaza waraka
 
Wakiacha ufisadi hakutakuwa na haja ya waraka na nyaraka! Nashauri na JF itoe waraka wenye Kaulimbiu hii: UFISADI KWANGU NI MWIKO, SITAFANYA WALA KUFANYIWA UFISADI KAMWE! Nawasilisha.
 
Niliwahi kuwaambia mkasome kitabu kinaitwa the root of all evil. Kama hamjui vita vingi vya wenyewe kwa wenyewe vina mkono wa Roman Catholic Church na sasa Tanzania ndipo inapolekea nyie subirini. Kingunge analosema ni kweli na hajakosea hata kidogo tunahitaji watu wenye ushupavu kama huo kunyooshea kidole Tabia kama hii.

Na tukiiachie Tanzania inaelekea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe

Hivi wewe unafikiri kinyume nyume,je umeusoma huo waraka au umekurupuka tuu na kuleta madai kwamba Roman Catholic Church inataka kuleta vurugu.Kama huna hoja na uthibitisho juu ya hili bora ukae kimya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom