Kinatakiwa Chama kipya cha Siasa cha Ukombozi hasa. CHADEMA na CCM hamna kitu

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Hivi vyama vikubwa viwili vyote vipo hoi. Hoi sana. Kimoja kinashikiliwa na Dola na kikingine kinashikiliwa na Ukosefu wa Chama mbadala.

Utaniuliza ACT nitakujibu hamna kitu pale. Hamna chama cha ukombozi wa Mtanzania.

CHADEMA ya sasa Imekuwa Nyepesi sana. Uzito wa Unyoya. Haina nguvu ya kimapinduzi. Matamko hayana nguvu au back up. Na almost kila mtu ni msemaji. Ukimsikia Lema,ukimsikia Msigwa,ukimsikia Mnyika n.k

Huoni Combination. Kila mtu anakuja kivyake kwa kivuli cha chama. Hakuna ambalo wameweza fanikiwa iwe katika maandamano au migomo.

Yaani mnashauri watu wagomee tozo halafu mnatoa namba za simu kutaka mchangiwe kufaidisha tena Serikali kwa tozo hizohizo.

Mtu anaomba mchango kwa kutumia account yake binafsi kumfungulia Askari Kesi? Tutajuaje hizo pesa zimetumika kwa namna stahili? Hapana hii si sawa. Chama kilipaswa kukaa na ku organize nini kifanyike.

Ukija kwa CCM nako pumzi imekata sana.... Wanaruka tu na kukanyagana...hamna uelekeo. Wapo tu hata hoja hawajui kujenga wala kubomoa za wapinzani wao. Kimechooooooooooka mno.
 
Sema Chadema hamna kitu

Ccm ipo kitu ndio maana ipo dolani😅
 
Hata chama kutoka mbinguni kwa katiba na tume hii iliyojaa ma TISS hamna kitu
 
Back
Top Bottom