Mkuu ni kweli
tindo ana kili sana ni tofauti na wanachdema walio wengi
Mimi niwashukuru wato Sixgates na Berenya, tuwe wakweli tu na ukweli utatuweka huru, Mimi baada ya kumfuatilia Dr. Slaa nimegundua ni kiongozi ambaye anapokuwa na hasira ni rahisi sana kuchukua maamuzi yasiyo na busara. Kwa Mh.Mbowe nimeona ni mtu ambaye hataki kuachia madaraka hata kama kuwepo kwake madarakanani kunaleta mpasuko. Kiongozi bora ni yule anayekubali kupisha wengine hata kama bado yeye ni bora. Inawezekana Mh. Mbowe hana washauri wazuri ama wapambe wamemzidi.
Sasa tuje kwa Zito, yeye nilikuwa namuamini tena huku akijinadi ni msomi, lakini nimegundua na yeye hana tofauti sana na hao hapo juu. Wakati wa sakata hili ndio ungekua hasa wakati wa yeye kuonyesha ukomavu wake wa kisiasa na elimu yake ionekane, mama yangu we kwa muda wa hizi siku saba baada ya kufanyiwa kile asichokipenda ndio mapungufu yake yote yameonekana. Ameongea mambo mengi sana ambayo kwa wachambuzi wa mambo atajikuta kwenye wakati mgumu huko mbeleni tuendako hata akifanikiwa kuwa mwenyekiti wa cdm kwani naye anaoenana hana uvumilivu na anachukua maamizi ya jazba.
Mimi naomba tena kuhusu Dr. Kitila, wote ni mashahidi toka kuanza kwa sakata hili, Dr.Kitila ndio ameonyesha kuwa ana msimamo, mvumilivu anakubaliana na hoja tofauti na hana jazba. Hatujamuona akijihushisha na makundi yoyote wala ushabiki usio na tija. Kama ni mtu anayefaa kuwa kiongozi wa cdm basi ni huyu Dr.Kitila kwani wote hata tukiweka pande zote mbili hasimu ndiye pekee anayeweza kukubalika kwa upande wa Zitto ama Slaa +Mbowe. Cdm ijitafakari na wakae meza moja tena kwani naamini wagombanao ndio wapatanao na kuheshimiana pia, japo damage waliyoitengeneza kwa muda huu mfupi ni kubwa.
Mimi sitaki kuamini kwamba milango imefungwa kwa Dr.Kitila kurejea cdm. Dr. Kitila anaweza kuomba kurejea tena cdm japo sijui yeye kama yeye atalichukulia hili vipi. Ama viongozi wa juu wa cdm au watu wote wenye ushawishi katika cdm wanaweza kumshawishi arejee na apendekezwe kugombea nafasi za juu kwani naamini kwa mwenendo wake anaweza kuleta utengamano tena cdm. Kila ajikwezwaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa. Dr. Kitila tupende tusipende ana mapungufu yake lakini maamuzi yaliyomkuta ya kuvuliwa uanachama yamechangiwa sana kwa mtazamo wangu na emotions and feelings zilizopo chamani kwa sasa kwa watu kuonyeshana ubavu, matokeo yake imekuwa ni vita vya panzi furaha kwa kunguru.
Nikijaribu kuangalia joto walilokuwa wamelipata CCM kutokana na uwezo na ushawishi wa cdm kwa wananchi mpaka wakawa wanachukua hatua chache japo kwa shingo upande, leo hii serekali inapandisha umeme kwa asilimia 85% huku watatetezi wa wananchi yaani Cdm wanaandama saa 3 asubuhi kwenda mahakamani kufanya ushabiki wa kesi yao wenyewe aibu gani hii. Naomba cdm na wanaoitakia cdm mema muingiapo vitandani kulala jiulizeni tena hili jukumu la kutetea wananchi wanyonge wa taifa hili mmeliweka pembeni mmeamua kucheza mechi ya Madrid na Barcelona mahakamani tena wenyewe kwa wenyewe. Mmeruhusu magazeti yetu kubaki yanaongelea upumbavu wa mahakama na kuacha suala la kupanga gas na umeme ambalo linagusa maisha ya wananchi na uchumi wa watanzania wote mnajadili madaraka!!!!
Naongea kwa uchungu suala hili kwani cdm ndio wangalau ilikuwa inatusaidia kupewa majibu ya matatizo yetu na serekali hata kama ni kwa kubabiababia, lakini haidhuru. Leo tunataka madaraka ili tuje tuwaongoze wananchi maskini wasio na elimu, maji safi, afya bora, gesi na umeme juu. Tunamuacha mshindani wetu Ccm akifanya apendalo wakati uwezo wake wa kuongoza umekwisha na sisi wenye afadhali tunagombea madaraka, aibu gani hii!!