hahahahaaa Mpwa mie sio wa kukasirika hata siku moja, hahahaa nikasirishwe na siasa za JF? hapana kwangu hii ni part of leisure, ok back to the topic, kuna issues mbili au tatu hapa tuziweke sawa,
Moja; umesema wewe uko au huwa unapenda kuwa upande wa Opressed, hii sifa uliipata lini mana siku zote watu wanalia dhidi ya CCM kuanzia kwenye Tembo wetu, simu , umeme nakadhalika, lakini wewe ndio umekuwa ukisapoti Madudu haya ya CCM, na umekiri kuwa sisiemu na madudu ya miaka nenda miaka rudi
Pili, kwa ukiri wako kuwa CCM ina madudu huoni kuwa unadhihirisha huo Unafiki ninaouzungumzia? Uko sisiemu kuna madudu na unakiri hivyo, basi wewe ni Msaliti na Mnafiki, unawasaliti wadogo na watoto wetu ili kupata mkate wako wa kila siku tu, huna tofauti na CHICHIDODO asiependa harufu ya kinyesi japo chakula chake kikuu ni kinyesi.
Tatu, upendo wako kwa nchi yako ni UPI? huu wa kuchochea udhalimu wa CCM dhidi ya wananchi? Unakosea Mpwa wangu bhana hapa umeteleza, sioni dhambi kama utakubali kuwa umeteleza na ukatengeneza tukaendelea mbele
NNe, Mimi siko upande wa mtu yoyote na nilijipambanua tangu mwanzoni na wewe pia ulifanya hivyo na ukasema wazi kuwa uko upande wa Zitto halafu cha kushangaza unasema uko kwa ajili ya nchi yako, kama hivyo ndivyo kweli, Je unakubaliana na waraka ule wa aikna zito? je ndio njia sahihi ya kufanya magezui ya kidemkrasia ndani ya chama? Je madhara ya waraka ule na mageuzi hayo yangemuathiri CDM peke yake? Ukweli unao
La mwisho labda; kuwa mkweli kwa nafsi yako, weka wazi hilo ulilonalo moyoni mwako na sisi tulijue kama mimi nilivyoweka la kwangu.
Mwishoni kabisa, tukumbuke nyumbani kidogo sometimes tunasahau haya mambo ya siasa!! Undugu wetu haufi kwa ajili ya sisas, asante