Kinachoendelea mitaani kwa ajili ya kumpa support ZZK leo pale H.C

Kinachoendelea mitaani kwa ajili ya kumpa support ZZK leo pale H.C

Status
Not open for further replies.
Sasa wazi mmejiingiza msiochadema kwenye hii movie. Mbunge mzima unasiasa za kidwanzi hivyo? Haitamrudishia uanachama wake hata mngefanya nini¿
Zitto hataki uanachama anataka haki itendeke tu basi.
 
Kuepuka upotoshaji wa Yericko Msabila Yohana hakikisha unakuwapo pia mahakamani au anawepo mtu wa kuleta update mida ya saanane ikifika. sixgates.
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
View attachment 130613Huku kanda ya kaskazini ni kupiga kazi hatuna mda na wasaliti

Kamanda sasa hapo kuna kazi gani inapigwa?

Mbinu za Mwenyekiti hizo, piga kazi, piga kazi, piga kazi, piga kazi then PIGA MIMBA mfanyakazi mwenzako!

Angalia mkono wa kulia wa huyo mwanamke, upo juu ya sarawili ya Kamanda..

Bila shaka muda kama huu mwakani huyo binti atakuwa analea mtoto wa Kamanda kama mwenzake Joyce Mukya.
 
Mkuu mimi ni rafiki wa kila mtu, siasa sio uadui ndio maana napendwa, and gues what???? Nimekuwa proposed kuingia kwenye BUNGE la KATIBA, nikipitishwa historia ya kuitengeneza katiba ya nchi itanitaja kwa jina langu

Labda katiba ya MWANDIGA
 
Kunajimbo la mgimwa lipo wazi hatujutii kumpoteza mhuni zito bye bye 2najikita kwa mgimwa sasa mtaelewa 2
 
mngeandamana juu ya bei ya umeme kupanda,huduma mbovu hospitalin,wanafunz 90% kupata div 0,tembo wetu kuuwawa,wapitisha madawa ya kulevya,mafisad,kutokuwa na ajira kwa vijana,kukosekana kwa maji,mikataba mibovu ya madini,wananch kuporwa ardhi yao.wananch kuuliwa bila hatia(opereshen tokomeza) nk..nadhan hii nchi ingekuwa kama china kimaendeleo,cha ajabu vijana tumekuwa tukitumika kama 3 bomba......KIJANA UCWE WA BEI RAHISI KIIVI..THINK LOUD..
 
Kuepuka upotoshaji wa Yericko Msabila Yohana hakikisha unakuwapo pia mahakamani au anawepo mtu wa kuleta update mida ya saanane ikifika. sixgates.

Mkuu, kuna binti anaaelekea H.C yeye ndie atarusha updates za moja kwa moja toka H.C..tulikamatwa na polisi pale pugu road, wametupiga fine, kwa sasa naelekea ubungo nina kikao kifupi, kama sitachelewa nitakuja
 
Last edited by a moderator:
Anaitwa Caroline Michael... Umefurahi????..nenda facebook ukaangalie jinsi alivyokuwa anaitetea chadema, nenda Tanuru la fikra kaulize caroline michael.. Na ngoja nimwambie ajitokeze JF, na Facebook akajibu mapigo..

Kaniambia muulizeni Ben Saanane, Shardcole, @le mutuz et al

Kumbe emujiidentify mwenyewe?

Mbona siku zote ulipokuwa unajitoa CDM hukutaka ujulikane? Wewe ni nana CDM?
 
Sikuwahi kufikiri kwamba Zitto anaweza kudanganywa kirahisi hivi na yeye akadanganyika.

Nyerere aliwahi kusema hivi, Unakuta mswahili ana dhahabu halafu anakuja mzungu ana vipande vya chupa anamwambia mswahili kwamba hiyo ya kwako sio dhahabu ya kwangu ndiyo dhahabu, mzungu anamubadilishia mswahili anampatia chupa halafu huyo mswahili anatoka anacheka kama ZUZU!

Kama kweli wewe Zitto sio ZUZU maana unatumika na CCM. Unaamini una wafuasi wengi kiasi hicho, hebu toka CDM tuone kama utaendelea kuwa na wafuasi hao.

I'm telling hao wote unawaona ni wafuasi wa CCM waliokodiwa kukuhadaa. Kama huamini futa kesi mahakamani halafu anzisha chama chako tuone kama utapata diwani hata mmoja.

Acha UZUZU Zitto, Wewe ni uzuri wa mkakasi ndani ni kipande cha mti. Nje ya CDM wewe ni kipande cha mti. CCM na wafuasi wako hao feki watakutupa kama jongoo.
 
Kunajimbo la mgimwa lipo wazi hatujutii kumpoteza mhuni zito bye bye 2najikita kwa mgimwa sasa mtaelewa 2 pigen porojo zenu za buku 7 ila h ndo chadema ha2ofii kelele za ccm 2shazoea kwanzia udin ukabil ukanda 2meshinda zote zk m2mdogo 2namsahau leo
 
zitto na ccm wamekuwa kitu kimoja kwa sasa?
wenye akili zetu tunajua ni nini kinaendelea.
ngoja nimsubirie mkono.
 
Kumbe emujiidentify mwenyewe?

Mbona siku zote ulipokuwa unajitoa CDM hukutaka ujulikane? Wewe ni nana CDM?

Haina maana mimi ndie Caroline michael.. Uyu bado ni mwanachadema wa kutumainiwa ila kwahili anamuunga mkono Zitto.. Cc wilium j malecela
 
Last edited by a moderator:
mtahangaika sana mwaka huu sixgate habari za toka mwaka jana?naona lumumba 7mmerejea kutoka mapuziko ya kuuaga mwaka2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ambao najua utakuwa mgumu sana ktk kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa hatimaye uchaguzi mkuu mapema mwakani nawasihi muongeze juhudi hata hivyo mmechelewa peoples power inafanya kazi.
 
Baada ya hukumu ya pingamizi la Zzk kutosomwa jana kuaahirishwa mpaka leo saa nane mchana, hali ya taharuki kutokaana na matokeo ya hukumu hiyo imetanda, yamkini hukumu hiyo haikusomwa jana kw sababu ya tamko la mwanasheria wa CDM kuhusu uwepo wa Zitto CDM ni kw sababu ya kimahakama,kw hiyo mahakama inatambua impact ya maamuzi yaake leo.

Nimepita manzese nimepita buguruni, sasa tupo temeke mwisho tunatoka kuelekea mwembe yanga (sio viwanjani), yapo magari, na mapikipiki yamechomekeza bendera za chadema (wanasema wao ni wanachama,wanakuja H.C na kadi zao) woote ni #teamZitto ..nimepenyezewa ratiba ya wafuasi haawa wa Zitto naambiwa watawapitia wenzao wa buguruni, watapita manzese then wataingia mjini posta wakilakiwa na kundi jingine ambalo limejiandaa kuwafanyia mapokezi.

Historia inakwenda kuandikwa ambapo jiji la DSM litasimama kw muda kusubiri hukumu hiyo ya kihistoria mbayo itaandika dibaji katika harakati mpya za kidemocrasia.

-------------------------
-------------------------
More info:
Zitto anatarajiwa kuongea na wana wa hili taifa mida ya saa kumi, tutaawjulisha venue itaakuwa wapi..

---------------
---------------
Picha

Nitaendelea kuwaleteeni taarifa

attachment.php


--------------------------
--------------------------
Tumesimamishwa na polisi wale wa "pikipiki" (vodafasta) wanadai wametuona saa nyingi na hwatambui ni nini kinaendelea, wamekagua magari na pikipiki. Pikipiki zimeachiwa, gari niliopo aina ya Harrier limekutwa bima imeisha kama ina siku nne, wanapambana na dereva kidogo aliwajibu vibaya police kw hiyo wamekataaa gari isitoke wanataka tuende kituoni.

------------------
------------------
TAAHADHARI
Wapo kundi la vijana ambao ni wakutengenezwa nasikia wanasubiri tukifika HC waje kuanzisha fujo wajidai wanadai hela kutoka kwetu, eti tumewanunua n hatujawlipa..ninachosema hakuna anaetudai.


[h=2]Zitto: Sitogombea Urais wala Ubunge 2015[/h]
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.

Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.

Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.


Source: Majira​
 
kama ana wafuasi wengi na anajiamini kwamba anawanachama wengi..si ni bora akaanzisha chama chake..sasa hivi pale kashaonekana msaliti.hata kama mahakama ikimpatia ushindi haitamsaidia..kama kweli anajiamini aanzishe chama chake na nadhani atapata kuungwa mkono sana na wana ccm..

kibaka /mhuni akiingia ndani ya nyumba yako humkimbii, unabaki kukabiliana naye!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom