Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Nimejifunza jambo moja hapa dodoma kuwa lowasa hakamati kabisa maana kwanza anawatu wengi

Ni kweli hakamatiki ana watu wengi sana hapo Dodoma ambao wamesombwa kutoka maeneo mbalimbali kucheza filamu kama ile ya Igunga ya kulia na kugaragara akivuliwa gamba!!!

Millya & Group at work. Jambo la msingi ambalo siwezi kushangaa na kumtisha Mwenyekiti wao na akatishika, japo sasa naona kama mkali kidogo. Kama nilivyosema awali, "mbele giza nyuma kaburi", wakiwavua watakua wameamua kwenda gizani maana hakuna ajuae kwa hakika plan 'B', 'C' na 'D' ya ENL, na pia hakuna ajuae yatakayotokea, lakini giza haina maana hakuna njia, ni kwamba tu hakuna mwanga ila njia ipo, lakini kurudi nyuma mwanga upo kuwa ni kaburi la uongozi wa juu wa CCM chini ya Kikwete na ushindi mkubwa kwa ENL na kundi lililo "tiifu" kwake, ambalo linaendeshwa kama 'serikali ya pembeni' maana lina bajeti iliyotuna,

lina watendaji mahiri, lina vijana 'watiifu' wanaofanya kazi usiku na mchana na humu JF wamejaa tele, wana vyombo vya habari na waandishi wa habari wengine na kikubwa kabisa na cha hatari wana mfumo hatari sana ambao uko kazini wakati wote na baadhi wamo ndani ya mfumo halali, na ingekua nchi nyingine hawa wangeitwa 'magaidi' maana 'mchana wanamulika, usiku wanachoma'.

Hawa 'magaidi' ni vigumu sana kuwatambua maana baadhi wanajifanya watiifu sana kwenye mfumo halali, baadhi wanajifanya hata kushambulia na kuhujumu kundi la ENL kiana. Haya yote JK anayajua, watu wake wa Usalama wanayajua, ndio maana nasema lolote laweza kutokea kama mkuu atasema, "sasa imetosha" kauli ambayo kwa sasa iko kinywani mwake.
 
Mr ENL anatumia mbinu ya mwisho ya kujinasua kwenye kaburi la kuvuliwa gamba kwa kuwatumia vijana wasiojua mbele ni wapi na nyuma ni wapi,wenyewe wanachoangalia ni chakula kidogo tu ya watoto.
Wataangamia bila kujua walipokosea!
Mkuu si kama hawajui, kama ulivyosema wanafikiri kwa tumbo na wengine hawaoni mbele bila ya ENL na kwa kweli ni vipofu na wana upofu wa ajabu. Hawataki kukubali kwamba kwa sasa ukimsimamisha ENL umepoteza mvuto kama chama. Uongo mwingi unatengenezwa kuonyesha kwamba ana wafuasi wengi katika jamii. Uongo mtupu maana ENL ndiye 'SI Unit' ya Ufisadi nchini tutake tusitake.
 
Naona Viongozi wengi Ndani ya CCM wamesahau yaliyowatokea KANU

Same stories looking for a crime inside a dark room...
 
Mkuu si kama hawajui, kama ulivyosema wanafikiri kwa tumbo na wengine hawaoni mbele bila ya ENL na kwa kweli ni vipofu na wana upofu wa ajabu. Hawataki kukubali kwamba kwa sasa ukimsimamisha ENL umepoteza mvuto kama chama. Uongo mwingi unatengenezwa kuonyesha kwamba ana wafuasi wengi katika jamii. Uongo mtupu maana ENL ndiye 'SI Unit' ya Ufisadi nchini tutake tusitake.

Tuwaache wenyeni waumane kwanza maana tunajua kwa uhakika wakimaliza kuumana wataanza kutafuta wengine wa kuwauma. EL na JK wanafahamiana na yawezekana mchezo unachezwa na wote kote kote kwa sababu sielewi kwanini walioko madarakani wanafanya kana kwamba hawako madarakani? Hivi kweli EL ana nguvu na mtandao kiasi hicho bila baraka za JK? Ujasiri wake anautoa wapi wakati hana chombo chochote rasmi ambacho kinapiga saluti kwake?
 
JK, rais na CCM chairman, enough is enough. Hakuna nchi inayoendeshwa huku watu walio nje ya serikali wakicontrol sehemu kubwa ya mamlaka.

Yaani Jk ameacha nchi imefika watu wanapledge allegiance kwa Lowassa na kumtetea waziwazi EL against Jk na kuendelea kupeta. Hell no, haiwezekani hata kidogo, kwa sababu je EL akiamua ambadilishe Jk itakuwa vipi??

Usalama kazi yake kubwa ni kuprotect institution ya Presidency, sasa usalama gani huu EL anaendesha nchi nje ya mfumo waziwazi??

Tutajua ukweli kuhusu mwelekeo wa nchi hiyo next week mungu akitupa uzima.

May Almighty God Bless Tanzania.
 
Hivi kweli EL ana nguvu na mtandao kiasi hicho bila baraka za JK? Ujasiri wake anautoa wapi wakati hana chombo chochote rasmi ambacho kinapiga saluti kwake?

Tatizo hapo ni kwamba inawawia vigumu ccm kumpiga chini EL kwa ufisadi kwa sababu yeye anajua kwamba JK naye ni fisadi. Hicho ndo kinachompa nguvu EL, na JK anajua kabisa kwamba EL anaujua ufisadi wake, kwa hiyo akimpiga chini anaweza kumuumbua.
 
Ushauri wa bure ccm wachague kaburi ili wafe kifo chema. Waiwafukuza magamba itakuwa mbaya sana. Kwanza vyovyote vile watafagiliwa wawe gizani ama kaburini. Hayo maelezo ya kututaka tutumie katiba mbovu kutengeneza katiba mpya labda akawambie mke wake na watoto. Sasa ccm wajiandae waone madhala ya upuuzi huu.
 
Tuwaache wenyeni waumane kwanza maana tunajua kwa uhakika wakimaliza kuumana wataanza kutafuta wengine wa kuwauma. EL na JK wanafahamiana na yawezekana mchezo unachezwa na wote kote kote kwa sababu sielewi kwanini walioko madarakani wanafanya kana kwamba hawako madarakani? Hivi kweli EL ana nguvu na mtandao kiasi hicho bila baraka za JK? Ujasiri wake anautoa wapi wakati hana chombo chochote rasmi ambacho kinapiga saluti kwake?
This is sensible.
 
Hii ni habari ambayo watu wameichangia usiku wote. mtoa habari asante kwa umakini wa kutoa maelezo ya kina. Tunakusubiri zaidi asubuhi hii, ni nini mwisho wa filamu hii?
 
Lolote litakaloamuliwa Dodoma, nimeshajua kuwa Kikwete hana ubavu wa kumvaa Lowasa. Inawezekana ni kuheshimu historia yao kisiasa pamoja au ni kwa sababu ya kumwogopa kwa kigezo chochote kiwacho.

Tatizo lililoko hapa siyo la Lowasa kuwa gamba bali ni la Kikwete mwenyewe kushindwa kujua anataka akipeleke chama chake wapi. Haja yake ilikuwa ni uraisi kusudi apate mianya ya biashara mbalimbali kwa ajili ya familia yake na ndugu zake, na vile vile kupata mwanya wa kuitembelea dunia nzima.

Alipoanza madaraka hayo alisema kuwa yeye siyo mfanya biashara na wala hana mpango wa kuanzia biashara ukubwani ingawa ana shamba la mananasi tu kule Bagamoyo. Leo hii sidhani kama bado anaongea hivyo tena, na sababu ya kushindwa kusema hivyo huenda ndiyo inayofamya aone ugumu wa kumvaa Lowasa.

Great power comes with responsibilities; hapa tuna mtu aliye na power lakini hataki responsibilities!!
 
Tuwaache wenyeni waumane kwanza maana tunajua kwa uhakika wakimaliza kuumana wataanza kutafuta wengine wa kuwauma. EL na JK wanafahamiana na yawezekana mchezo unachezwa na wote kote kote kwa sababu sielewi kwanini walioko madarakani wanafanya kana kwamba hawako madarakani? Hivi kweli EL ana nguvu na mtandao kiasi hicho bila baraka za JK? Ujasiri wake anautoa wapi wakati hana chombo chochote rasmi ambacho kinapiga saluti kwake?

And guess what huo mchezo ndiyo hasa ukombozi kwetu....

I have thrown a word of confusion in the camp of enemy na wote watajuwa hakika kwa Jehova kuna wokovu. Mara mnara wa babeli ukisambaratika wengine wao wataanguka chini kwa panic wakitegemea kuna wasaidizi wakuwa nyanyua kama ilivyo kawaida ya siku zote na kumbe watagundua kawaida imebadilika nao kwa presure kubwa iliyoambatana na sinto fahamu hiyo wata poteza fahamu zao.

Huku nyuma hao hao wawategemeao watawageuka na kuwa maliza wasi simame milele na kila moja atashangaa imekuwaje leo hawa wanatenda kinyume na matarajio? Ndipo kutakuwa na kimya cha ajabu kila moja asijue yupi ni rafiki na yupi ni adui ndipo wenye haki fahamu zao zitakapo warudia na kutenda sawasawa na mapenzi ya Mungu.....

Neno roho awaambia mafisadi tengenezeni nyumba zenu maana ugonjwa huu ni wa mauti!
 
Vyovyote iwavyo, Mimi ninachoomba hapa ni kuwa CCM waendelee kuvurugana tu ili mwisho wa siku watoke kirahisi, tuupoteze huu mfumo wa kifisadi kuanzia balozi hadi Ikulu. Hatuwezi kuendelea kama taifa kwa kuwa na viongozi wasiotaka kutafuta solutions za matatizo ya nchi badala yake wako busy kuangalia na kulinganisha nchi zingine harafu wanakaa chini wakiwa wameridhika.
 
Tuwaache wenyeni waumane kwanza maana tunajua kwa uhakika wakimaliza kuumana wataanza kutafuta wengine wa kuwauma. EL na JK wanafahamiana na yawezekana mchezo unachezwa na wote kote kote kwa sababu sielewi kwanini walioko madarakani wanafanya kana kwamba hawako madarakani? Hivi kweli EL ana nguvu na mtandao kiasi hicho bila baraka za JK? Ujasiri wake anautoa wapi wakati hana chombo chochote rasmi ambacho kinapiga saluti kwake?

yawezekana nguvu ya lowasa iko katika madhaifu nna madhambi ya jk ambayo ni yeye el pekee anayajua. Alishasema hawakukutana barabarani. Na kashfa za kisiasa ni mbaya sana. Yawezekana ccm wanaogopa kumdhuru el kwa kuwa kuna nyaraka imejificha nyuma yake na iko bayana kwa jk. Labda imefichwa benk fulani, so el akidhurika, anonymous anai release. Nidhuru nikulipue.
 
Kwa jinsi mambo yanavyoenda ndani ya chama, muda mfupi ujao chama kitasambaratika.
Sidhani kama chama kitasambaratika bali mafisadi; na baada ya hapo hata mm sijui kitakachotokea. Tatizo ni kuwa wengi watakuwa taken by surprise kwani hakuna hata mmoja anayewaza mafisadi na nguvu zao hizo nika tembo na sisimizi, japo mdogo lakini humwangusha tembo chini...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom