Bahati mbaya sana mimi sina chama na vyama vyetu vya upinzani havina mbinu za kijasusi, ujasusi halali, kwa maana ya kupanga mikakati ya ushindi uchaguzi ujao. Chama kama Chadema hii ndio nafasi nzuri ya kucheza na mchezo unaoendelea CCM kujipanga kuchukua nchi 2015. Ni rahisi sana CCM kuingia mkenge na kuwabeba Chadema kwani inawezekana sana wakatoka Dodoma wakiwa 'CCM wamoja' na wakaimba na kukejeli wapinzani, wakafanya maandamano na mipasho nchi nzima na wakamuita Lowassa zuma wao na Benno Malisa Malema wao, na ndipo sasa akwa Mwenyekiti wa CCM na mgombea Urais 2015, bonge la mteremko kwa chama kilichojipembua kama wapambanaji wa ufisadi, hata bila kampeni haoooo, awe Slaa, Mbowe ama Zitto wataweka historia mpya kiulaini sana. Narudia huenda ndio nuru ing'aayo kwa Watanzania.
Amina.Mungu endelea kuinusuru TanzaniaMungu saidia Tanzania,wape uelewa watu wapate tambua kinachoendelea nchini!!!!
Kuna taarifa kwamba, vikao vya awali vya CCM mjini Dodoma vimeanza kwa kuwahoji vijana kadhaa wa UVCCM wanaotajwa kuwa karibu na Watuhumiwa wa ufisadi walotakiwa kujivua gamba.
Haijafahamika kama vijana hao watakua kafara la baba zao ama ndio kipima joto cha maamuzi magumu yanayotarajiwa kufanywa wiki hii. Hakika mwandishi mahiri wa makala katika Raia Mwema alisema, "mbele giza nyuma kaburi" na sasa uamuzi wa kurudi nyuma ni CCM kuingia kaburini na kwenda mbele ni gizani maana magamba yana nguvu za ajabu na kila kukicha yanakua magumu.
Je, CCM itaamua kuingia gizani kuvua magamba ama kurudi nyuma na kuyaacha iwe ni kaburi la CCM?
Taarifa zaidi baadae.
![]()
Nawafahamu Kalanga na Kadogo, hawana lolote, wababaishaji tu ni nguvu ya pesa wanaweza kuitumia lakini hawana nguvu ya kuwafanya watu wabadilishe msimamo.Fred Lowasa, Julius Kalanga ( chair uvccm monduli), Isack Kadogoo ( Diwan Monduli), James Millya (chair uvccm mkoa arusha) wako kazini mjini Dodoma
Hivi kuna ulazima gani wa vikao vya magamba kufanyika usiku wa manane????
Usiku Lucifer anakuwa ana operate vizuri sana. (mkuu wa giza!)
Mkuu Halisi,
Kazi unayo na sidhani kama hata nguvu unayotumia kumponda Lowassa na kundi lake kama unapata return ya kulingana.
Mie bado naamini Lowassa ndie anafaa kuwa President ajaye. Kwa kifupi mtu anakua na hatia kama mahakama imemuona hivyo na sio MAGAZETI na mitandao ya computer na simu.. Kumbuka SAS alivyosemwa na kuhusishwa na kikundi kimoja Zenji miaka hiyoo mpaka tukaanza kuamini.
Hizo propaganda fanyeni lakini mwisho wake utakua sio mzuri. Mkimwekea FITINA Lowassa musahau kabisa mikoa ya Arusha, Manyara na Knjaro. Itaenda kwa wapinzani milele. Kaskazini mtabakia na Tanga ambao wanaeleweka kama Pemba ilivyo kwa CUF.
Karata inabidi ichezwe vizuri na sio kishabiki. Pia inaonekana una chuki ya wazi sana na EL. Hii itafanya kila unachoandika kuhusu EL tujiulize mara mbili.
Jaribu kidogo kuficha HISIA zako juu ya EL. EL bado tunampenda na anaweza kuthubutu..
Asante
Positive yote, Halisi kaanzisha thread hii si kwa sababu ya kutuhabarisha yanayojiri ila ni kumponda Lowassa purposely, lakini naomba Halisi ajue kuwa yule jamaa ni mashine kubwa kuliko inasaga na kukoboa at the same time mtahangaika sana na habari za magazeti lakini ukienda on ground level haiko kivile they have to compromise naye. Nawaambia subirini muone pamoja na chuki za kina Halisi za kumuita eti SI unit ya ufisadi na kumuacha fisadi papa atatoka kidedea na msione ajabu akawa m/kiti wa chama come 2012.Mkuu Halisi,