Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Vita ya Mengi na Lowassa mpaka JF, kazi kweli kweli. Hivi Mengi na Lowassa walikoseana kwenye nini? Au ni lile suala la hoteli ya Kilimanjaro?

Waacheni CCM wafanya maamuzi yao, haisaidii kwa JF kugeuka Hussein Yahaya. Kesho itafika na tutajua ukweli.

Hii hapa ni kuongezeana bytes tu kwenye kompyuta zetu.

Mengi anahusikaje hapo? Hiyo picha ya Lowassa, Kikwete, Makinda, Bilal, Hamad, Pinda, Msekwa na Mukama imepigwa leo huko Dodoma - zingine hizi hapa: H@ki Ngowi: Taswira Za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete Atua Mjini Dodoma Tayari Kabisa Kushiriki Vikao Maalum Vya Chama na Kushiriki Chakula Cha Jioni na Wabunge Wa CCM
 
Mkuu nadhani hujasoma maandiko na unajibu kijumla sana kwa maneno "hisia za chuki"... Jenga hoja. Ila time will tell, najua wapi umechomwa. Hoja nyingi nimeandika kwa kutumia marejeo yeni wenyewe. Bahati mbaya sana hujui naongea kutoka wapi, pengine ndani ya vikao ama pembeni yako. Kwanza angalia alama za nyakati, kwanza lugha ilikua haiwezekani lakini sasa "tutapambana"" hatukubali kuonewa" "tupelekwe mahakamani"... Oooh "zuma wa Tanzania"...."Malema wetu".... Sasa kiko wapi cha "hatujakutana barabarani"... Munashindana na nani? Nani aliyemwambia Lowassa aachie ujumbe wa NEC na hadi ss anasita? Imekuaje maandalizi ya maandamano kumpokea kishujaa akitoka au akipona kama hali ni shwari? Jambo la msingi ni kwamba tunachotaka ni taarifa za kutoka eneo la tukio, tujuze mikakati yenu ya mapokezi ya Zuma na Malema wenu!!!
Lowassa hatakuwa rais wa Tanzania whether yeye anataka au la. Tanzania ya 2015 ni tofauti sana; lazima mgombea wa CCM sio tu asiwe fisadi lakini pia kusiwe na perception yoyote ya kuonekana ni fisadi.

Ila pia Sitta anayepigiwa kampeni na vyombo vya Mengi hata kwenye tatu bora za kupelekwa mkutano mkuu 2015 hatakuwemo. Atakatwa kama alivyokatwa mzee wetu Malecela.

CCM wameshikwa pabaya, watapitisha jina la mtu asiye na kashfa na huenda akawa mwanamke.
 
Kwa mantiki hiyo Migiro ndio safi peke yake
 
Ha ha ha!Why Chenge doesn't clap for the chairman?Anaonekana anayo Gazabu...
d26.jpg

Nape vipi??Magamba yanavuka hayavuki?
d18.jpg

Awkward position?Kikao hiki ni cha watu nane?Kwa haraa niliowatambuwa ni EL,Pinda,JK,Msekwa,Makinda,Makamu wa Rais,Msekwa,mwingine sijamtambua,hata hivyo ni kikao cha watu nane hapo chini...
d14.jpg

Picha:Kwa hisani ya Haki Ngowi.
 
Vita ya Mengi na Lowassa mpaka JF, kazi kweli kweli. Hivi Mengi na Lowassa walikoseana kwenye nini? Au ni lile suala la hoteli ya Kilimanjaro?

Waacheni CCM wafanya maamuzi yao, haisaidii kwa JF kugeuka Hussein Yahaya. Kesho itafika na tutajua ukweli.

Hii hapa ni kuongezeana bytes tu kwenye kompyuta zetu.

Kazi kweli kweli... Great Thinker, now majina ya watu. Tujadilini hoja, Je, Lowassa hajaitwa? Hajaambiwa aachie NEC? Huo ugomvi anzisha thread yake hapa mkuu hakuna cha ugomvi wala nini, ni kujadili tu walioitwa na kuhojiwa Dodoma jana na leo! Wengine hatuwataji majina maana ni vijana tunaowategemea kuiongoza nchi yetu hawa wazee wakiondoka
 
Halisi,
Huhitaji hata kuwa Great Thinker kujua chuki za watu wawili ambao ni Mengi na Lowassa zimetawala thread hii. Kibaya wahusika wako mbali na wanatumia wengine kuwapigania mapambano yao.

Nchi haina umeme, haina ajira, magonjwa kila angle lakini watu tunahangaika na personalities tu kila siku wakati uchaguzi ni almost miaka minne kuanzia sasa.

Hakuna cha vijana wala wazee, wote akili zetu ziko sawa tu; zinafanana fanana. Tuchape kazi na kuheshimu sheria na ndizo zitatuokoa na sio hawa wanasiasa uchwara ambao kila siku ni migogoro tu huku watu wao hata mlo mmoja ni shida.

CCM wamejikuta wanacheza mchezo wa makundi wakati dhana ya kujivua gamba inatakiwa iendane na sera pamoja na maadili. Badala ya kujadili watu, wajadili ni maadili yapi yanatakiwa kufuatwa ndani ya chama? Wakisha kubaliana hayo basi watumie uchaguzi wa mwaka kesho kuondoa kwa njia ya demokrasia wale wote ambao hawakidhi haja katika muundo na maadili mapya ya chama.

Ndio hayo tu kwa leo.
 
Halisi,
Huhitaji hata kuwa Great Thinker kujua chuki za watu wawili ambao ni Mengi na Lowassa zimetawala thread hii. Kibaya wahusika wako mbali na wanatumia wengine kuwapigania mapambano yao.

Nchi haina umeme, haina ajira, magonjwa kila angle lakini watu tunahangaika na personalities tu kila siku wakati uchaguzi ni almost miaka minne kuanzia sasa.

Hakuna cha vijana wala wazee, wote akili zetu ziko sawa tu; zinafanana fanana. Tuchape kazi na kuheshimu sheria na ndizo zitatuokoa na sio hawa wanasiasa uchwara ambao kila siku ni migogoro tu huku watu wao hata mlo mmoja ni shida.

Ndio hayo tu kwa leo.

Pole sana. Nadhani kesho ukisoma magazeti ya Mwananchi na keshokutwa Habari leo na Mtanzania utasema nao wametumwa. Ni mawazo mgando sana. Jenga hoja, hakuna kikao Dodoma? Hawakuitwa watu maadili? Hawakuambiwa waachie NEC, wewe ndiye una chuki na unataka kuvuruga hoja kwa kuingiza majina ya watu wasiohusika. Bahati mbaya sana tunabanwa na maadili lakini kaka unakosea sana maneno yako haya si mahali pake, anzisha thread ya ugomvi wa Lowassa na Mengi na utaje waligombana wapi na kuhusu nini hata Lowassa atakushangaa maana najua hata hiyo hoja yako inamharibia, au umetumwa umharibie Lowassa? Sisi tunasema kuna uvuaji magamba Dodoma na wahusika wanapambana na wengine wameshaapa kama "noma na iwe noma" wewe unasema chuki binafsi ipi? Hivi hujui kinachoendelea?
 
Kwa kuangalia hiyo spika ya wanene hapo mwanzo, Spika Makinda anaweza kuwa neutral kweli kwenye vikao vya bunge? Kwa mfano kama hicho kikao chao wanakubaliana kutimiza jambo fulani bungeni hata kama halina maslahi kwa wananchi walio wengi Makinda atakwenda kinyume? Something is fundamentally wrong here!
 
Hakuna gamba litakalovuliwa vikao vya dodoma ni vya kumsafisha Lowassa itatafutwa lugha ya kuwapumbaza watu, kuna matatu ninayoyaona mimi, aidha watasema hakuna kikao kilichotaja majina ya watu au watapewa onyo au tutaambiwa mkutano mkuu wa 2012 ndio utakaoamua, vinginevyo mbali ya hayo patachimbika.
 
Nimeanzisha Hii Thread ili wapasha Habari wa ndani watupe yaliyojiri!
 
Aisee nilikuwa sijajua kuwa asilimia 95 ya hii Mijamaa ni Obese.....
Ona mavitambi....

Ha ha ha!Why Chenge doesn't clap for the chairman?Anaonekana anayo Gazabu...
d26.jpg

Nape vipi??Magamba yanavuka hayavuki?
d18.jpg

Awkward position?Kikao hiki ni cha watu nane?Kwa haraa niliowatambuwa ni EL,Pinda,JK,Msekwa,Makinda,Makamu wa Rais,Msekwa,mwingine sijamtambua,hata hivyo ni kikao cha watu nane hapo chini...
d14.jpg

Picha:Kwa hisani ya Haki Ngowi.
 
Kwa Hisani ya Hakingowiblog

Na Mwandishi Maalum, Dodoma, Jumamosi Nov. 19, 2011

Baada ya mapumziko mafupi katika Ikulu ndogo ya Dodoma Dkt Kikwete alielekea ukumbi wa St. Gaspers ambako aliongea na wabunge wa CCM na kupata nao chakula cha usiku.

Katika hotuba yake, Dkt Kikwete aliwapa changamoto wabunge hao wa CCM waende kwa wapiga kura wao na kuwaelemisha kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya uliopitishwa Jumamosi Bungeni Dodoma.

Dkt Kikwete aliwasisistizia wabunge hao umuhimu wa kupeleka elimu hiyo ya mchakato wa kupata katiba mpya kwani hivi karibuni kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wa nini kinachoendelea, na kusema kuwa wakiwa wabunge wa chama tawala ni wajibu wao kuelimisha umma kwamba kanuni na sheria zote zimefuatwa katika kupitisha muswada huo ambao umesomwa kwa mara ya pili, baada ya kusomwa mara ya kwanza kwa mujibu wa sheria.

Rais Kikwete aliwakumbusha wabunge hao kwamba mchakato huo si jambo geni na kwamba ndio uliofuatwa na Marais wote toka wa awamu ya Kwanza hadi ya tatu, akisisitiza kwamba ni muhimu wanancho wote wakaelewa hilo, ikizingatiwa kwamba kuna baadhi ya watu wachache wanaotaka kupotosha umma kwamba hatua hiyo ni batili wakati sio kweli, ikizingatiwa kwamba kila lililo katika katiba ya sasa limezingatiwa.

Pia aliwasihi Watanzania kujitokeza kutoa maoni yao ya ni katiba gani wanayoitaka pindi muda wa kufanya hivyo utapowadia, na wasikubali kughiribiwa na wachache waliopania kupindisha ukweli.

Kwa mujibu wa ratiba leo Jumapili kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ukumbi wa White House kitachofanyika kutwa nzima, kitachofuatiwa na kikao cha Kamati kuu ya CCM Jumatatu na Jumanne. Halmashauri kuu ya CCM itakutana kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.
 
Hivi kuna ulazima gani wa vikao vya magamba kufanyika usiku wa manane????
 
Wanajifanya eti wana bana matumizi ya per diem kwa chama kwa kufanya vikao usiku wakati serikalini wanaiba kama nini eg kafumu
 
ungeweka chochote cha maana kwanza kwenye uzi wako. Utherwise ungewaachia wenye data wabandike uzi
 
Inaelekea mkulima ndiyo ana ishu na Mengi, na yupo kambi flan ktk haya magamba....!! Malalamiko ya magazeti sio mapya....

Back
Top Bottom