Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Ngoma tunaicheza kwa viuno na mabega, sii ujaona kijiwe kilivyo noga!...Lowassa ni maarufu kuliko Sitta ndani ya chama na nje ya chama hilo usijidanganye...

d14.jpg

JK, EL et al @ DOM
 
Hoja kama hoja nimeipenda ila comment zako zinawalakini maana ukishaanza kutaja ukanda hapa maana yake unataka sasa tuingize rasimi kwenye katiba kuwa utawala wa nchi yetu niwakupokezana kikanda haijalishi sifa za mtu kiongozi mwenyewe, hii ni hatari sana.

Itakuwaje nyanda za juu kusini nao wakikomaa kuwa lazima rais ajaye atoke huko na kanda yenye neema ya ziwa victoria wakasema wanamtaka Magufuli, hapo si ndio mwanzo wa balaa! Take control of your comment mkuu

That's gud waambie nchi yetu haina ukabila
 
Ngoma tunaicheza kwa viuno na mabega, sii ujaona kijiwe kilivyo noga!...Lowassa ni maarufu kuliko Sitta ndani ya chama na nje ya chama hilo usijidanganye. Leo hii EL ikisimama na Sitta atamtoa nje kwa sababu Sitta hana mbinu za ushindi.. Kumbuka tu kwamba hata Uspika alipigwa changa la macho na EL..

Hivi unafikiri nguvu kubwa unayofanyika kumdhalilisha JK ina lengo gani? yaani leo EL ana uchungu sana na nchi yetu inakokwenda kuliko alivyokuwa waziri na waziri mkuu..tena watu wako radhi kumsamehe wengine wakidai arudi madarakani. Halafu JK amekaa kimya hata kujitetea hana moja isipokuwa wasizungumze CDM...Uchaguzi ulopita viongozi karibu wote walimkimbia JK akabakia nani? - EL na familia ya JK! EL ndiye aliyechakachua majina ya wagombea na kadhalika, hawa kweli maadui jamani au mnajichanganya...

Mkuu Mkandara nakuaminia sana kwa data. Baadhi ya mambo inabidi uangalia tena na vyanzo vyako. Si vyema kujadili humu hasa kwa mimi maana mjadala sasa kwa mimi mwanahabari ni kitu gani kinachoendelea ndani na nje ya vikao vya CCM Dodoma.

Kwanza, nilishasema hata kama ni kweli JK anataka kutuchezea tuamini kwamba wanagombana wakati wana mpango unaofanana "kubadilishana vijiti" bado kwa sasa nafasi hiyo haipo tena maana Watanzania wa sasa "si mabwege tena" wa kuvalishwa kofia na kulishwa pilao. Watanzania hawa wa 'dot com' ni hatari kuliko wale wa Tunisia, Misry, Libya na kwingineko. Tunawadharau sana kwa kuangalia rafiki zangu fulani wanaotumia nguvu kubwa kulazimisha nyeusi ionekane nyeupe, kama mfua kaniki kwa OMO na Blue akitaraji ing'ae matokeo yake itapauka tu. Lolote liwalo CCM imo ktk mtihani mgumu sana maana JK alisema wazi kwamba atapambana na matumizi ya fedha ktk uchaguzi, lakini alielemewa na sasa tunaona tunalazimishwa kuamini kwamba Lowassa ni msafi kuliko yeyote ndani ya CCM na kwamba sasa ndiye pekee anastahili kukabidhiwa nchi (naamini wewe si muumini wa hili). Ni kweli kwamba Lowassa amejenga mtandao mzito sana serikalini na ndani ya CCM lakini si kweli kwamba huo mtandao umejengwa kwa misimamo bali umejengwa kwa msingi, matofali, mbao na paa la fedha, ambalo duniani kote 'nyumba' inayojengwa kwa fedha na mabavu haitodumu. Hosni Mubarak alikua na fedha nyingi na alitumia mabavu, lakini alianguka. Najua wako wanaotaka kumfananisha JK na Mubarak, lakini Rais Lowassa (CCM wakimpitisha) ndiye atakayekua Mubarak wetu tuendako maana ni mwanasiasa anayeamini (na ametumia) katika fedha kwenye kila jambo, na anaamini yeyote ananunulika na kila jambo na kila mtu ana bei. Maana yake atashinda mbele ya wapinzani kwa gharama yoyote na atazima kila kitu kwa nguvu kubwa ya dola na fedha, na atahakikisha kila media inaimba sifa njema za mtawala kila kukicha (hata sasa ndio burudani yake).
Nina mifano mingi na JK anajua udhaifu huo wa Lowassa kuhusu kuamini kwenye fedha, japo inamuuma sana kwa kuwa alimsaidia ktika mambo mengi kwa kutumia mbinu hizo hizo chafu, ambazo sasa JK zinamtesa na ndio sababu ya kigugumizi cha muda mrefu cha kumchukulia hatua, lakini sasa imefika mahali inaonekana 'heri nusu shari' pamoja na kuwa "mbele giza nyuma kaburi" kwa mujibu wa mwandishi mahiri Msomaji Raia katika Raia Mwema.
 
Lowassa ni maarufu kuliko Sitta ndani ya chama na nje ya chama hilo usijidanganye. Leo hii EL ikisimama na Sitta atamtoa nje kwa sababu Sitta hana mbinu za ushindi.. Kumbuka tu kwamba hata Uspika alipigwa changa la macho na EL..
Hapa ndipo tunapotofautiana Mkuu, yaani Lowassa maarufu kuliko Sitta!! Yes and No. Lowassa maarufu kwa uzuri kwa anaowalipa lakini si kwa umma, labda wale wanaotengenezwa kama wale wanafunzi wa UDSM waliomfuata awasaidie kutatua tatizo la mikopo. Nilishasema SI Unit ya ufisadi ni Lowassa, lakini huwezi kumfananisha na Sitta hasa katika umma unaopenda haki hata kama Sitta ana udhaifu wake. Kwa suala la mbinu, yes Lowassa ana mbinu na kubwa ya mbinu zake ni kutumia udhaifu wetu wa kupenda mno vya dezo bila kufanya kazi na hivyo kununua kila aliye mbele yake, ukiacha wachache wenye misimamo. Kwamba atashinda CCM, si ajabu maana CCM wengi wameingia katika siasa kwa rushwa na hadi sasa maisha yao yote bila rushwa hayaendi, hawasomeshi watoto bila rushwa na wengine hata kula yao ni kwa rushwa, hawana kazi na wenye kazi ni kubangaiza ama kujibanza kwenye vijiwe ama vijimigahawa kama Mwenyekiti wa UVCCM wa Arusha anayeishi kwa Mzungu. Huo ndio ukweli watu kama Hamisi Mgeja hana kazi kutwa hakai Shinyanga anazurura mara atumie timu ya Kahama kula fedha za Vodacom za ligi hadi timu ikashuka, mara sasa atumie uenyekiti na watu kama Millya na Mgeja ni wengi CCM. Wako vijana wazuri na wenye uwezo ktk kambi ya Lowassa, hao naamini akianguka watasonga mbele maana wana maono, si wadandiaji wana mikakati na wana akili, lakini si wengi ni wachache sana na hata EL hawaamini sana japo anawatumia.
 
Lowassa anajisumbua sana ndio maana ataangushwa na chama..

Umaarufu anaoutafuta kwa hila na njama zote watu wameshamchoka, kibaya zaidi anawatumia watu ambao IQ zao ndogo.
 
Chochote kitakachotoke huko dom tunaomba amani. Miaka 50 bila vurugu inawezekana.

Vurugu zitatoka wapi? Kama kuna kundi limepelekwa Dodoma kufanya fujo wasahau, hakuna kitu kama hicho. Dodoma si mji wa fujo.
 
Kwanini watu wanafikiri Lowassa ana clout ya kuwashawishi wananchi wa Tanzania kuwa hayuko jinsi anavyodhaniwa au kujulikana? Ni kweli wapo watu wanaoweza kuapa kwa Lowassa lakini kweli hivi akisimama na kuanza kampeni ataahidi nini Watanzania ambacho hakijawahi kuahidiwa na viongozi wenzake wa CCM waliopo au waliopita? Naombeni kitu japo kimoja tu ambacho EL anaweza kusema ambacho hakijawahi kusemwwa na CCM.
 
Bahati mbaya sana mimi sina chama na vyama vyetu vya upinzani havina mbinu za kijasusi, ujasusi halali, kwa maana ya kupanga mikakati ya ushindi uchaguzi ujao. Chama kama Chadema hii ndio nafasi nzuri ya kucheza na mchezo unaoendelea CCM kujipanga kuchukua nchi 2015. Ni rahisi sana CCM kuingia mkenge na kuwabeba Chadema kwani inawezekana sana wakatoka Dodoma wakiwa 'CCM wamoja' na wakaimba na kukejeli wapinzani, wakafanya maandamano na mipasho nchi nzima na wakamuita Lowassa zuma wao na Benno Malisa Malema wao, na ndipo sasa akwa Mwenyekiti wa CCM na mgombea Urais 2015, bonge la mteremko kwa chama kilichojipembua kama wapambanaji wa ufisadi, hata bila kampeni haoooo, awe Slaa, Mbowe ama Zitto wataweka historia mpya kiulaini sana. Narudia huenda ndio nuru ing'aayo kwa Watanzania.
 
Kwanini watu wanafikiri Lowassa ana clout ya kuwashawishi wananchi wa Tanzania kuwa hayuko jinsi anavyodhaniwa au kujulikana? Ni kweli wapo watu wanaoweza kuapa kwa Lowassa lakini kweli hivi akisimama na kuanza kampeni ataahidi nini Watanzania ambacho hakijawahi kuahidiwa na viongozi wenzake wa CCM waliopo au waliopita? Naombeni kitu japo kimoja tu ambacho EL anaweza kusema ambacho hakijawahi kusemwwa na CCM.

Wafuasi wake wanajidanganya sana Lowassa is no longer presidential candidate kwa ccm..NO!

Anaweza kwenda chadema au NCCR lakini siyo ndani ya ccm watampiga chenga ambayo hajawahi kuona ..

CCM inajua kuhandle hao watu maarufu kwa utaratibu wa kujimaliza mwenyewe just wait..
 
wewe halisi unatoa coment zako kwa hisia za chuki huku ukweli unajua moyoni, tutawapiga pini hamtaamini tunarudi na ushindi wa ugenini toka dodoma na tunajiaandaa kuwapokea kwa kishindo hapa chuga town. tulifurahi pamoja, tulihuzika pamoja, tutafight pamoja na pamoja tutashinda. msipime kina cha bahari kwa kuingiza mguu
 
Wana janvini, kuna yeyote yule mwenye taarifa kuhusu vikao vya CCM vinavyoendelea DODOMA.
 
wewe halisi unatoa coment zako kwa hisia za chuki huku ukweli unajua moyoni, tutawapiga pini hamtaamini tunarudi na ushindi wa ugenini toka dodoma na tunajiaandaa kuwapokea kwa kishindo hapa chuga town. tulifurahi pamoja, tulihuzika pamoja, tutafight pamoja na pamoja tutashinda. msipime kina cha bahari kwa kuingiza mguu

Mkuu nadhani hujasoma maandiko na unajibu kijumla sana kwa maneno "hisia za chuki"... Jenga hoja. Ila time will tell, najua wapi umechomwa. Hoja nyingi nimeandika kwa kutumia marejeo yeni wenyewe. Bahati mbaya sana hujui naongea kutoka wapi, pengine ndani ya vikao ama pembeni yako. Kwanza angalia alama za nyakati, kwanza lugha ilikua haiwezekani lakini sasa "tutapambana"" hatukubali kuonewa" "tupelekwe mahakamani"... Oooh "zuma wa Tanzania"...."Malema wetu".... Sasa kiko wapi cha "hatujakutana barabarani"... Munashindana na nani? Nani aliyemwambia Lowassa aachie ujumbe wa NEC na hadi ss anasita? Imekuaje maandalizi ya maandamano kumpokea kishujaa akitoka au akipona kama hali ni shwari? Jambo la msingi ni kwamba tunachotaka ni taarifa za kutoka eneo la tukio, tujuze mikakati yenu ya mapokezi ya Zuma na Malema wenu!!!
 
Vita ya Mengi na Lowassa mpaka JF, kazi kweli kweli. Hivi Mengi na Lowassa walikoseana kwenye nini? Au ni lile suala la hoteli ya Kilimanjaro?

Waacheni CCM wafanya maamuzi yao, haisaidii kwa JF kugeuka Hussein Yahaya. Kesho itafika na tutajua ukweli.

Hii hapa ni kuongezeana bytes tu kwenye kompyuta zetu.
 
Back
Top Bottom