Kimataifa takwimu zinambeba sana Rais Samia. Awe makini ili kuwepo na consistence

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Ukisoma vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi hali inaonekana nzuri sana kwa Tanzania chini ya Rais Samia.

Wawekezaji wanaonekana kuwa na imani nae sana na hadi wanapohojiwa na makampuni makubwa wanasema wazi wako tayari kuwekeza Tanzania zaidi ya maeneo mengine.

Kwenye utalii nako si haba, nchi yetu inasemwa kuwa inafanya vizuri sana kwa kuwa top tourist destination kwa Afrika Mashariki.

Haya hayatokei kwa bahati mbaya. Sababu kuu ni namna Samia alivyojitanabaisha kuwa ni Pro investment na Rais ambaye hayuko negative na wawekezaji.

Rais Samia akiendelea hivi anaweza kuja kufanya maajabu makubwa zaidi hadi kufikia 2030 ambapo anatarajiwa kumaliza muda wake.

Hofu yangu kubwa naona kama anataka kutoka nje ya reli kwa Kuanza kuwarudisha watu ambao walisemwa kuwanyanyasa wawekezaji na wafanyabiashara mf. Paul Makonda.

Rais wangu Samia anapaswa kukumbuka kuwa ili afanye mazuri kweli lazima awe consistent kwenye mambo anayofanya. Kurudi nyuma kupoteza confidence kwa wawekezaji na wafanyabiashara haliwezi kuwa jambo jema kwake na hata kwa Tanzania kama nchi.

Ili tuendelee kweli inabidi haya yanayofanyika sasa yaendelee kufanyika bila kukoma tena kwa miongo mingi sana ndo tutafikia kuwa the economic powerhouse kwa Afrika.

Tunapoweza kushauri tusiache kushauri. Nchi inapofanya vizuri ni faida kwa wote na inapokuwa vibaya ni hasara kwa wote
20231024_205724.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom