Kilio na sala ya Lissu toka Ukonga: Watanzania mmelala? Mimi sijalala

Kilio na sala ya Lissu toka Ukonga: Watanzania mmelala? Mimi sijalala

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,136
Reaction score
96,161
Watanzania, mmelala?
Mimi sijalala hadi sasa! Hii si leo, hii si kesho – hii ni vita ya maisha na uhai wangu! Niko hapa peke yangu, njaa inaungua ndani yangu, sina chochote kinywani, wala sijui nini kinachoendelea kuhusu hatima yangu! Mimi si jambazi, si gaidi. Kama ni hivyo, nipelekeni mbele ya haki! Nipelekewe ili kuthibitishwa! Lakini hamnioni? Mnasikia sauti yangu? Au nyinyi mmelala?

Watanzania, ninyi ni ndugu zangu, ni damu yangu. Uzaliwa wangu Singida haunifanyi niwaone watu wa Morogoro, Tanga, au Dar es Salaam kuwa wageni. Sisi wote tu wa damu moja! Lakini kwa nini kimya hiki? Kwa nini hakuna anayesimama nami? Mmefumba macho? Au mmelala?

Mimi sijalala hadi sasa! Hii ni vita ya maisha na uhai wangu!

Watanzania, kama ninaweza kuteswa hivi, kuumizwa mpaka mwili wangu unakataa kunibeba, basi niambieni – mti mbichi watautendea vipi? Maana kama hoja yangu ni kupindua nchi, basi kesi iko wapi mahakamani? Mbona sipelekwi mbele ya sheria ili nami nione haki? Mbona mmekaa kimya? Mbona sauti zenu zimezibwa? Sijaogopa tuhuma! Zileteni hizo tuhuma! Hata kama ni kunyongwa, nijue hukumu yangu kwa macho yangu! Lakini hamtaki? Au bado mmelala?

Mimi sijalala hadi sasa – na hii vita inanichoma moyo!

Tazama, nazidi kuumwa, nazidi kulegea. Madawa yananiokonywa, huduma za afya zinaninyang’anywa. Unasema niko salama? Unasema nitapona? Siku moja ukija humu, utadhani wewe ni mti mbichi au mkavu? Unafikiri utatendewa vyema zaidi yangu? Kula kwangu ni mashaka kila siku, uhuru wangu umekandamizwa chini ya nyayo za giza. Na nyinyi mnaangalia tu? Machozi yangu yanamwagika kama mvua ya masika, lakini hakuna anayeona. Au mmelala?

Mimi sijalala hadi sasa – hii ni vita ya maisha na uhai wangu!
Njooni! Njooni mwone ninayopitia! Sikieni majozi yangu, enyi wana wa Tanzania! Kama bado mna moyo, kama bado mna damu inayowaka, simameni nami! Msiache nife kwa kimya!

---

NINI KIFANYIKE?

Kwanza, nimepangiwa utabiri wa kuletwa na nabii kuwa nitakaa hadi 2030. Natamani niseme nacheka, lakini machozi yananiuma. Wanataka kunifanyia pressure? Wanataka nijisikie nimefungwa muda wote huo? Hii set-up, kamwe sitaikubali! Nchi hii ya babu na bibi zetu ilipiganiwa kwa damu na machozi ili tuituze kwa vizazi vyetu! Sisi ndio wenye nchi! Tuikatae kwa nguvu zetu zote!

Tuanzishe michakato nje ya Tanzania. Maana ndani humu kote kumeoza. Kwa nyinyi mliopo nje na mliopo ndani – naombeni, waambieni dunia: “Mtu wetu ametupwa humu kwa dhuluma.” Siku moja wewe na kizazi chako mtaandikwa kwenye vitabu vya enzi: “Ulinitendea wema nilipokuwa vifungoni.”
Naweza kufa leo, naweza kufa kesho, lakini wema wenu hautasahaulika mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya historia.

Basi nyinyi rejeeni kulala kwa amani. Mimi nitaendelea kukesha. Nitasoma vitabu vyangu. Usingizi nitapata, lakini sasa si wakati wa kulala. Nipo hapa na kinyesi mbele yangu kama kukombolewa. Lakini mimi si mti mkavu – mimi ni binadamu, nina roho inayopiga kelele!

Kwaheri.
Na Eid njema kwenu nyote.
 

Attachments

  • IMG-20260322-WA0025.jpg
    IMG-20260322-WA0025.jpg
    52.7 KB · Views: 1
Inaumiza sana.

Siku upinzani mkichukua nchi hakikisheni mnawatafuta hawa mmoja baada ya mwingine au ndugu zao.

1. Viongozi wa serikali ya awamu ya tano iliyoongozwa na Pombe Magufuli.
2. Samia Suhulu
3. Jakaya Kikwete and co
4 Viongozi wa polisi.

Hawa ni wakuwapoteza hata kama watakuwa wazee na kama wamekufa ndugu na watoto wao wapo.

Itakuwa ujuha na dhihaka kwa watanzania kama hawa watu wataachwa.
 
Lissu anapigania watu wapumbavu

sijaelewa, kwa nini unawaita watu wapumbavu? tarehe 10/29 wametoka wameuliwa kama wanyama, ulitaka wafanye nini tena labda, wavamie jela kumtoa au? una idea yoyote labda badala ya kuita watu wapumbavu? vp khs waliouliwa 10/29 wakipigania haki? na wale wanaotekwa na kuteswa kila siku kila mahali, vipi wale wanaojitokeza kila Tundu Lisu akiletwa mahakamani na wengine kupigwa na kuumizwa na polisi this is what they get kwamba ni wapumbavu? ...
 
Basi nyinyi rejeeni kulala kwa amani. Mimi nitaendelea kukesha. Nitasoma vitabu vyangu. Usingizi nitapata, lakini sasa si wakati wa kulala. Nipo hapa na kinyesi mbele yangu kama kukombolewa. Lakini mimi si mti mkavu – mimi ni binadamu, nina roho inayopiga kelele!

Kwaheri.
Na Eid njema kwenu nyote.
Sina hakika kama huu ni "mwandiko na fikra" toka moja kwa moja kwa Tundu Lissu!

Mpumbavu yeyote, hata hao maadui wanaomnyanyasa Tundu Lissu wanaweza kuandika chochote humu JF kupima upepo unakovumia.

WaTanzania "hawalali na hawatalala". Ni juzi tu wazalendo wameweka damu yao chini kurutubisha ardhi hii isinajisiwe milele. Hawa huwezi kusema walilala; mapambano ndiyo kwanza yameanza.

Kunyanyaswa kwa Tundu Lissu ni sehemu na kichocheo kitakachozaa ukombozi wa taifa hili.

WatTanzania hawatalala; watasimama na Tundu Lissu mpaka ukombozi kamili utakapopatikana.
 
Kuna sehemu walipuuza mambo sasa anatafuta simpath kutoka kwa watu ilikua kama mzaha anashangilia, mara watu wazima wanapiga makelele kulia kwamba hajala.

Now anasema ndani kumeoza maana yake hana imani hata na viongozi wenzake. Walioko nje watasaidia nini kama wandani ushawaona uozo. Hakuna serikali popote duniani inayoona hatari mbele yale na wakakuchekea HAIPO NA HAITOKUJA KUWEPO.
 
sijaelewa, kwa nini unawaita watu wapumbavu? tarehe 10/29 wametoka wameuliwa kama wanyama, ulitaka wafanye nini tena labda, wavamie jela kumtoa au? una idea yoyote labda badala ya kuita watu wapumbavu? vp khs waliouliwa 10/29 wakipigania haki? na wale wanaotekwa na kuteswa kila siku kila mahali, vipi wale wanaojitokeza kila Tundu Lisu akiletwa mahakamani na wengine kupigwa na kuumizwa na polisi this is what they get kwamba ni wapumbavu? ...
miongoni mwa upumbavu ni kutoka okt 29 mkuu,
 
Back
Top Bottom