Ukitumia mbegu nzuri vinauwezo wa kukaa mpaka mwezi wa nne. Inamaana ivo unavoviona miezi ya nne ni stock ya kuanzia mwezi wa 10 na 11. Kwahiyo siri kubwa ya ukaaji wa kitunguu store ni mbegu nzuri kwani kitunguu kinakua na layer nyingi hivo kuweza kustahimili muda wote huo.

Aisee! Kumbe! Jamaa mwezi wa nne wamelamba pesa nzuri sana Dar, 160,000/= Kwa gunia. Ukiwa na magunia 300 Kwa ekari 4 hapo unakuwa milionea ghafla.
 
Vitunguu vinakubali maeneo mengi tu hapa nchini kwetu, kikubwa ni kuhakikisha udongo sio ule wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu kwani ikiwa utakua unahifadhi maji mengi basi utakuta kitunguu kinanawili majani tu ila tunda lenyewe haliongezeki kitu. Kwahiyo kujibu swali lako "kitunguu kinahitaji udongo wenye rutuba, eneo linalopata jua zuri na maji ya uhakika yawepo"

mapinga kitunguu kinastawi?
 
Mkubwa nina maswali mengi?....Tokea uanze kushughulika na kilimo cha vitunguu ni changamoto gani umekua ukipata katika biashara hiyo???

Changamoto zipo nyingi ila kubwa zaidi ni wafanyakazi na kwa sokoni mwanzoni utapata shida ya madalali wasiowaaminifu.
 
Aisee! Kumbe! Jamaa mwezi wa nne wamelamba pesa nzuri sana Dar, 160,000/= Kwa gunia. Ukiwa na magunia 300 Kwa ekari 4 hapo unakuwa milionea ghafla.

Ni kweli kitunguu cha msimu kina pesa nzuri sana. Ila pia kinahitaji umakini manake kuna misimu huwa mambo yanageuka. Mfano msimu wa mwaka juzi hadi mwezi wa 3 unafika bei ziligoma kupanda zaidi zikawa zinashuka. Kwahiyo umakini unahitajika
 
Sehemu ya shamba nnayotarajia kuanza kuvuna mwezi wa saba. Hapo vitunguu vilikua na umri wa week tatu tokea kupandikizwa. Nawashauri kutumia mbegu bora ili kupanda matokeo mazuri.
IMG_3130.JPG
 
Hii ndo gold ya mkulima, ila niko na maswali machache. Umeelezea vizuri ila hukufafanua/hukutoa mchepuo wote, yaani garama ya mbegu, garama za kutayalisha shamba na utunzaji wa shamba hadi kufikia kuvuna
sasa naomba utupe ufafanuzi ukizingatia point nilizoweka hapo juu
Shukrani
 
Natamani ningeweza kuweka maelezo yote hapa ila ni ngumu manake kuna vitu vingine ni rahisi kumuelezea mtu mkiwa face to face, pale nilijaribu tu kuweka kiasi cha pesa ambacho unatakiwa kukitumia kuhudumia acre 1 ambacho jumla ya gharama ni kama 2.5M ambayo inaweza kuzidi au kupungua kutokana na usimamizi wako wa shamba. Natumai nimejaribu kujibu swali lako kaka
Hii ndo gold ya mkulima, ila niko na maswali machache. Umeelezea vizuri ila hukufafanua/hukutoa mchepuo wote, yaani garama ya mbegu, garama za kutayalisha shamba na utunzaji wa shamba hadi kufikia kuvuna
sasa naomba utupe ufafanuzi ukizingatia point nilizoweka hapo juu
Shukrani
 
Ni mawazo mazuri kwa wote waliotoa, pongezi kwako mtoa mada na mlio changia, mhesima katoa ufafanuzi mfupi wa mbegu, ila kwenye kilimo kuna zaidi ya mbegu, hivyo kwa kuwa yeye ni mkulima mzoefu wa zao hili katoa mawasiliano yake pale, barua pepe na kilongalonga hivyo ukimtafuta auatapa maelekezo yote na kama una swali unamuuliza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom