CHAI CHUNGU
JF-Expert Member
- Feb 20, 2012
- 7,113
- 930
Wapo maeneo gani kwa morogoro mkuu?Ukiwa Morogoro tembelea Magadu Officers mess. Ni club nzuri sana na wana garden ya maembe kama ekar 2. pale utakosha macho yako.
Wapo maeneo gani kwa morogoro mkuu?Ukiwa Morogoro tembelea Magadu Officers mess. Ni club nzuri sana na wana garden ya maembe kama ekar 2. pale utakosha macho yako.
KUBOTA,
Tembea uone, hasa wakulima kuona ndio kuamini. Kuna hata parachichi kubwa kama mti wa mchungwa unazaa embe hadi elfu tano sikuamini mpaka nilipoona, mti huo wa parachichi unaanza kuzaa baada ya miezi 16, tunda lake(parachichi) linaweza kukaa hadi siku 21 bila kuoza kwenye mazingira ya kawaida (nje ya fridge). Nenda wilaya ya SIHA kwenye shamba la AFRICADO LTD utaona.
Kwa upande wa embe kati ya mwaka wa 3 hadi wa 7 ndio inafikia hiyo potential na kama pruning yake inafanyika vizuri
usiuachie ukue mkubwa kama mnayofanyia vikao vya kijiji. Reccommended height sio zaidi ya 5m.
Yapo mashamba mengi na kwa bahati mbaya hukuweza kuhudhuria week ya kuonja embe ilifanya mnazi mmoja week ya kwanza January mwaka huu ungepata maelezo zaidi.
Hilo jibu hapo chini ni location ya shamba la miembe , nikimjibu muuliza swali
Kama jamaa atachelewa kutoa contacts zake, mtwangie huyu jamaa wa SUA, kwake kuna miche ya matunda hadi karanga miti 0712099434 au hapa Dar mtwangie huyu 0784284800, wote wana vitalu vya uhakika. Yule wa pale Mapinga sina simu yake, lakini naye yuko vizuri.
Ukiwa Morogoro tembelea Magadu Officers mess. Ni club nzuri sana na wana garden ya maembe kama ekar 2. pale utakosha macho yako.
nikipata nitakupaMalila,
Huyo wa Mapinga contacts zake zingepatikana ingekuwa poa sana maana mi napita sana pande hizo
Miaka mitatu, hapo utapata kiasi tu, miaka mitano ndo unaanza kupata faida kamili, hapo ndo unaweza kupata hadi matunda 3000 kwa mti mmoja
Asante mheshimiwa! Maelezo yako yanatoa mwanga na ninaiona picha ya kilimo hiki vizuri. Ninavutiwa sana na kilimo cha miembe! Nitakutafuta unielimishe zaidi sina uzoefu na hasa uzaaji wa miembe hasa hii aina ya miembe ya kupandisha (grafted). Hivi unayajua mashamba ya miembe ya kupigiwa mfano ambayo ninaweza kwenda kujionea nikavutiwa, yako maeneo gani?
Kaka matanuru ya mkaa yamenifikisha level nyingine, nimeagiza mashine ya kutengenezea mkaa unaotokana na pumba za mpunga (rice hull briquettes), nimechoshwa na kelele za bwana miti. Nitakuwa na-pack fresh na kusambaza hadi supermarkets. Kaka kwenye biashara ya nishati hakuna anayelala njaa kuanzia muuza kuni, mkaa, gesi, petrolleum products hadi Tanesco, nishati ni pesa mara moja !! Aaah sitasahau matanulu........Mkuu upo mpaka huku??
Vipi matanuru yako ya kuchoma mka mkuu bado unaendea nayo???
Kaka matanuru ya mkaa yamenifikisha level nyingine, nimeagiza mashine ya kutengenezea mkaa unaotokana na pumba za mpunga (rice hull briquettes), nimechoshwa na kelele za bwana miti. Nitakuwa na-pack fresh na kusambaza hadi supermarkets. Kaka kwenye biashara ya nishati hakuna anayelala njaa kuanzia muuza kuni, mkaa, gesi, petrolleum products hadi Tanesco, nishati ni pesa mara moja !! Aaah sitasahau matanulu........
naomba kujua jinsi ya kupanda mmea wa emba hasa umbali kutoka mmea mmja hadi mwingi, ni mita ngapi?
Naomba kujua jinsi ya kupanda mmea wa emba hasa umbali kutoka mmea mmja hadi mwingi, ni mita ngapi?
Naweza kupata mawasiliano yaoWakuu
Nimepita Kibiri kwenye kile kikundi cha wakulima wa kitalu cha embe. I tell you wako vizuri saaaaaaana kuliko hata nilivyo tarajia.
Wameanzisha kampeni yao ya '' Lima miti kumi ya embe upate Shillingi millioni moja. Kampeni yao ni kwamba nunua miche kumi (30,000) chimba mashimo na kuweka samadi (5,000x10= 50,000), mwagilia kwa mwaka ni assumption dumu moja miche 5 na dumu moja la maji ni TZS 300 na kwa wiki nyeshea mara 2 (2x2x300x52 = 62,400) na garama nyinginezo 30,000. Jumla 172,400
Mapato: kila mti unayo potential ya kuzaa hadi embe 3,000 kwa msimu lakini wao wamechukua average ya 500/tree
hivyo unaweza kupata embe 5,000 kwa miche kumi na kila mmoja unaweza kuuza kwa sh 300 = 1,500,000 ukitoa garama laki 2 unapata faida ya sh 1.3million minimum.
Eneo kwenye compaign yao wanasema hata kama kuna eneo la bustani kima 5 meters kuzunguka nyumba yao unaweza kuotesha embe utapata kivuli lakini pia matunda yake ni fedha.
Naomba tuwaunge mkono. wao ni wakulima wadogo wa miche bora ya embe (Dodo, bolibo, Tommy, Keit, Kent, Alfonso, red Indian, Palmer, n.k) pia wanatoa ushauri kwa kweli nimevutiwa nao saaaaaaaaaaaaaana.
sikutarajia kama ningeweza kupta elimu niliyopata kwao, ukipata nafasi ya kuwa KIBITI
please pita kwenye hiki kikundi ujionee.
Cross pollination inafanyika vipi?Panda miembe ya kawaida inayokubali eneo ulipo halafu ndo uwaite jamaa wakufanyie cross-pollination. Hii ni cost effective and sustainable pia. Mimi nimefanya hivyo