Ninayo miche ya miembe aina zote. Kila mche ni shs 2500 na ninaizalishia Morogoro. Kwa upande wa Dar es salaam ninaye mzambazaji ambaye ni JB farms . yupo Kibaha kwa Matias. Kunashamba moja ambalo lina mapicha ya mbwa kwa mbele na limeandikwa JB farm. Hapo utapata miche yangu kwa bei hiyo hiyo. Kama up morogoro, unaweza chukulia direct toka shambani kwangu.
Upandaji wa miembe ni meter 10 mche hadi mche na meta 10 mstari hadi mstari. Hii itakupa miche 100 kwa ha moja au miche 40 kwa ekari moja. Usishawishike kupanda zaidi ya hapo kwa aka kwani baada ya miaka mitatu iakuwa kwa kuingiliana na mavuno hayatakuwa mazuri.
Kwa kawaida miche hutoa maua msimu wa maua unaofuata tangu upande. Mfano, ukipanda Mach mwaka huu, july itatoa maua hata kama bado mche haujawa na umbo la kutosha kubeba maembe. haya maua yatoe mara moja na usiruhusu kuwa maembe. Hali kadhalika msimu utakaofuata. Mwaka wapili hup mwembe utakupa kati ya maembe 70-100. Baada ya hapo, maembe yataendela kuongezeka kila mwaka na kama umeutunza vizuri unaweza fika hata mia tano. Hapo utatakiwa kuwa makini maana matawi yatakwanyka kwa kuzidiwa. Utatakiwa wakati mwingine kuyapunguza ili kila tawi libebe uzito litakao uwezo, ila hutakosa maembe 200 hadi 250.
Kwa ajili ya muda naishia hapo, ila tunaweza kuelimishana memgi kuhusu maembe. Mfano magonjwa, pruning, nk. jaribu kuni pm na nitawezakuelimishana zaidi.