Nini kitasaidia mti wa mwembe kuzaa matunda?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Mwaka Jana, miwili iliweka matunda machache. Mti wa kwanza ulizaa embe 1 na wa pili maembe 2. Ilikuwa mitamu sana.

Nilitarajia mwaka huu miti yote 5 ingezaa, tena matunda mengi kuzidi ya mwaka Jana. Imekuwa kinyume chake.

Katika miembe yote 5 iliyopo, ni mmoja tu ndiyo uliozaa, tena matunda mawili tu.

Kwa nini haizai? Ni kawaida?
 
Attachments

  • IMG_20240228_103513_876.jpg
    IMG_20240228_103513_876.jpg
    5.5 MB · Views: 10
  • IMG_20240228_103505_631.jpg
    IMG_20240228_103505_631.jpg
    5.8 MB · Views: 8
Tafuta bwana shamba watauangalia na kukushauri "bure". Kuna aina fulani ya wadudu ushambulia maua yakichomoza. Pili, upungufu wa madini fulani na ukame. Mwembe unaweza kuonekana green lakini ukawa na upungufu mkubwa wa maji kuotesha matunda.
Labda matatizo mengine mkuu lakini siyo ukame! Haukuwahi kukaukiwa maji. Wakati wa kiangazi ulikuwa ukimwagiliziwa kila siku.
 
huo muembe utoboe tundu alafu unyandue utazaa kama unavyotaka..

ushauziwa embe pori mchanganyiko mkiambiwa mtafute wataalamu wa kupandikiza mnanunua miembe ya afutano 😂😂😂
 
Mwaka Jana, miwili iliweka matunda machache. Mti wa kwanza ulizaa embe 1 na wa pili maembe 2. Ilikuwa mitamu sana.

Nilitarajia mwaka huu miti yote 5 ingezaa, tena matunda mengi kuzidi ya mwaka Jana. Imekuwa kinyume chake.

Katika miembe yote 5 iliyopo, ni mmoja tu ndiyo uliozaa, tena matunda mawili tu.

Kwa nini haizai? Ni kawaida?
Kinachosababisha hiyo hali ya mwembe kutokuzaa ni aina ya wadudu wanafanana na sisimizi ambao mwembe ukianza kutoa maua hao wadudu wanaenda kula maua hivyo kupelekea mwembe kushindwa kuzaa.

Jambo la kufanya ni kuhakikisha unapiga dawa katika miembe yako kila miembe ikikaribia kutoa maua au kumwagia mafuta ya taa au oil chafu kwenye shina la mwembe ili hao wadudu washindwe kupanda juu kula maua.
 
Uko mkoa gani? Kama ni Pwani msimu wa maembe uliopita haukufanya vizuri sana kutokana na hali ya hewa na pia mlipuko wa nzi wa maembe wanaoshambulia maua na embe kwa ujumla.
 
Mwaka Jana, miwili iliweka matunda machache. Mti wa kwanza ulizaa embe 1 na wa pili maembe 2. Ilikuwa mitamu sana.

Nilitarajia mwaka huu miti yote 5 ingezaa, tena matunda mengi kuzidi ya mwaka Jana. Imekuwa kinyume chake.

Katika miembe yote 5 iliyopo, ni mmoja tu ndiyo uliozaa, tena matunda mawili tu.

Kwa nini haizai? Ni kawaida?
Mwembe kuzaa ni katika jitihada za kujihami na ukame/kiangazi/jua
kama mwembe unapata maji ya kutosha hauta zaa sana
hivo mkuu msimu wenye mvua nyingi usitarajie maembe mengi
ndo maana maembe ni mengi sehemu zenye ukame
 
Palizi
Maji
Muda/wakati wake sahihi wa kuzaa
Pulizia dawa
Rutuba
Nimelichukua la upuliziaji wa dawa.

Hayo mengine yote sina mashaka nayo:
1. Umekuwa ukipata maji ya kutosha hata kiangazi

2. Umewekewa samadi ya kutosha

3. Magugu hayajawahi kuruhusiwa kushindana nao.
 
Kinachosababisha hiyo hali ya mwembe kutokuzaa ni aina ya wadudu wanafanana na sisimizi ambao mwembe ukianza kutoa maua hao wadudu wanaenda kula maua hivyo kupelekea mwembe kushindwa kuzaa.

Jambo la kufanya ni kuhakikisha unapiga dawa katika miembe yako kila miembe ikikaribia kutoa maua au kumwagia mafuta ya taa au oil chafu kwenye shina la mwembe ili hao wadudu washindwe kupanda juu kula maua.
Nashukuru sana mkuu. Nitafanya hivyo.
 
Mwembe kuzaa ni katika jitihada za kujihami na ukame/kiangazi/jua
kama mwembe unapata maji ya kutosha hauta zaa sana
hivo mkuu msimu wenye mvua nyingi usitarajie maembe mengi
ndo maana maembe ni mengi sehemu zenye ukame
Shukran mkuu. Nilikuwa sijui hili.
 
Zingatia pia kupuliza dawa wakati muembe umechanua maua, itasaidia kuboresha maua yasipukutike.

Pia dawa za wadudu, kuna nzi wa matunda(washenzi sana hawa). Sisimizi, buibui na wadudu wengine. Hawa wote usipowadhibiti, wataharibu maua na wengine wataharibu maembe.

Samadi ni muhimu pia, usimwagilie kupitiliza, kama ni muembe wa kisasa na ni mkubwa. Basi maji lita 20 kwa wiki yanatosha kabisa. Cha muhimu, kuwa na unyevu wa kutosha. Embe za kisasa hata mvua zikiwa nyingi zinazaa vizuri kabisa, shida ni mvua zikiwa nyingi wakati muembe umeweka maua.
 
Mwaka Jana, miwili iliweka matunda machache. Mti wa kwanza ulizaa embe 1 na wa pili maembe 2. Ilikuwa mitamu sana.

Nilitarajia mwaka huu miti yote 5 ingezaa, tena matunda mengi kuzidi ya mwaka Jana. Imekuwa kinyume chake.

Katika miembe yote 5 iliyopo, ni mmoja tu ndiyo uliozaa, tena matunda mawili tu.

Kwa nini haizai? Ni kawaida?
Chukua misumali ya size ya kati (isiwe mikubwa sana kuzidi unene wa shina la mti). Ukikaribia msimu wa maembe, pigilia msumali kwenye Kila mtu, kisha wait n see.
 
Back
Top Bottom