Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 533
- 1,110
Wakubwa jamvini, nilikuwa napekua pekua nimekutana na thread hii imenishitua sana nimeona nijisalimishe kwenu wakuu kwani hapa JF kumejaa wazoefu mliotapakaa kila kona duniani mnitoe ushamba!Wakuu
Nimepita Kibiri kwenye kile kikundi cha wakulima wa kitalu cha embe. I tell you wako vizuri saaaaaaana kuliko hata nilivyo tarajia.
Wameanzisha kampeni yao ya '' Lima miti kumi ya embe upate Shillingi millioni moja. Kampeni yao ni kwamba nunua miche kumi (30,000) chimba mashimo na kuweka samadi (5,000x10= 50,000), mwagilia kwa mwaka ni assumption dumu moja miche 5 na dumu moja la maji ni TZS 300 na kwa wiki nyeshea mara 2 (2x2x300x52 = 62,400) na garama nyinginezo 30,000. Jumla 172,400
Mapato: kila mti unayo potential ya kuzaa hadi embe 3,000 kwa msimu lakini wao wamechukua average ya 500/tree
hivyo unaweza kupata embe 5,000 kwa miche kumi na kila mmoja unaweza kuuza kwa sh 300 = 1,500,000 ukitoa garama laki 2 unapata faida ya sh 1.3million minimum.
Eneo kwenye compaign yao wanasema hata kama kuna eneo la bustani kima 5 meters kuzunguka nyumba yao unaweza kuotesha embe utapata kivuli lakini pia matunda yake ni fedha.
Naomba tuwaunge mkono. wao ni wakulima wadogo wa miche bora ya embe (Dodo, bolibo, Tommy, Keit, Kent, Alfonso, red Indian, Palmer, n.k) pia wanatoa ushauri kwa kweli nimevutiwa nao saaaaaaaaaaaaaana.
sikutarajia kama ningeweza kupta elimu niliyopata kwao, ukipata nafasi ya kuwa KIBITI
please pita kwenye hiki kikundi ujionee.
Hivi hii miembe yenye uzazi mkubwa hivi ni ile yeye umri wa miaka kumi hadi ishirini au ni hii mifupi ya kupandisha tunayoijua jamani? Hiyo potential ya kuzaa embe hadi 3000 kwa msimu ni kwa ile miembe mikubwa ambayo mikutano ya kijiji hufanyika chini yake?
Au ni miembe ya hivi viembe sindano vidogo vidogo? Kwa hii miembe ya kisasa mifupi ya kupandisha napata kazi kuamini! Kwa vile nilishakutana na figure za machungwa 4000 kwa mti humu JF inanibidi nijiulize sana kabla sijahamasika! Kwenye promotion ya vitu watu wanakuja na very inflated figures which are always unrealistic!
Mimi sibishi kabisa kwa vile sina uhakika na kilimo cha miembe ila kwa wenye uzoefu nawaomba mnihakikishie iwapo mdau hajapitiliza kupigia debe biashara yake ya miche!